Ujenzi reli ya kisasa Dar es Salaam - Morogoro wafikia asilimia 70

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
FEBRUARI 7 2020.

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha Dar es Salaam- Morogoro chenye urefu wa kilomita 300 umekamilika kwa asilimia 70.

Amesema hatua hiyo ni miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa bajeti ya Serikali iliyopitishwa na Bunge.

Ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Februari 7, 2020 wakati akiahirisha mkutano wa 18 wa Bunge la 11 mjini Dodoma.

Amesema ujenzi kwa sehemu ya Morogoro – Makutupora (kilometa 422) unaendelea.

Ametaja mafanikio mengine kuwa ni kuendelea na ujenzi wa mradi wa kufua umeme wa maji wa Julius Nyerere ambako kazi zilizokamilika ni pamoja na ujenzi wa daraja la muda, utafiti wa miamba na udongo na uchimbaji wa mtaro wa chini kwa chini wenye urefu wa mita 147.6.

Amebainisha kuwa Serikali imefanikiwa kuendeleza mradi wa umeme vijijini (REA), kwamba hadi Desemba 2019 vijiji 8,236 kati ya 12,268 vya Tanzania Bara vilikuwa vimeunganishwa na umeme, sawa na asilimia 67.1.
 
Hiyo REA kuna ubabaishaji mwingi sana.

Mfano kuna vijiji vinahesabiwa kuunganishwa lakini unakuta nguzo zimepita tu kijijini hapo pasipo kuunganishwa hata kaya/mji mmoja isipokuwa shule au zahanati pekee.
 
Bila picha, itakuwa porojo...


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Hii reli kwa mujibu wa tangazo lililowekwa pale gerezani wakati inaanza ilikua iwe November 2019. Inamaana miezi 38 ni asilimia 70.
Ukichanganya na hizi mvua zisizo na ratiba bado mbombo ngafu
 
Tuliambiwa treni ingeenda Dodoma Nov mwaka jana. Mara hii imefika 70%. Muda haugandi. Uongo wenu utafika mwisho tu
 
Si umeambiwa kabla haijafika morogoro ni asilimia sabini sijui na bado asilimia 6000
Yani bora wangempa mchina angeichapa haraka mturuki mpaka sasa hajafika hata Morogoro na ni KM 300 tu Dodoma anazingine 400+ atazifikisha lini
 
Back
Top Bottom