Ujenzi Mkubwa unaoendelea Kigamboni(Dege Eco Village), ni mradi wa nani?

Binafsi nimeshatembelea miradi yote miwili yaani DEGE na AVIC.
AVIC unaeleweka zaidi na nyumba zao zimekaa vizuri ni bungalows na villas, DEGE naona kama wanajenga hostels. Anyway, take your time utembelee ufanye uamuzi mwenyewe.
Mkuu ni wapi zilipo ofisi zao naomba website zao
 
Uc
Dawa ya Huyo Akbaru ni kuyachukua kinguvu hayo maeneo au kupeleka shauri kwenye mahakama za zinazoshughulikia ardhi ili anyang'anywe maana hayajaendeleza kwa zaidi ya miaka mi3,serikali inasisitiza kilimo kwanza huku wao wenyewe hawa walk the talk!
Uchukue kwa nguvu halafu uende mahakamani. Si ndio akili za yule mnyama tukiwaita tunapigwa ban. Akili za makalioni zina athar kubwa sana
 
Huu mradi wa ECO Village uliishia wapi? Waturuki walikimbia baada ya JPM kukamata nchi na kutuma mjumbe pale kuulizia mmiliki wa mradi kwa kuwa alipokuwa waziri alipewa majibu ya kunangwa. Asante sana Mh. Rais kimbizana na hawa wawekezaji wanaopitia kodi na mafao ya wananchi kwa kampuni za kuficha majina yao kupitia kwa washika pembe tu. Kila namba itasomwa awamu hiii.
 
Ni mradi wa ujenzi wa nyumba takribani 7,000. Mradi huu ni ubia kati ya kampuni ya Azimio na NSSF.

Bw Iqbal ni mwenye eneo hilo na mmoja wa wakurugenzi wa kampuni ya Azimio.

Dkt Faustine Ndugulile
MB-Mbunge Kigamboni

Mbunge,
Sina matatizo yeyote na bw. Iqbal kuwa ndiye mtamalaki wa eneo hilo. Tatizo langu ni kuwa kwa asli eneo hilo lilikuwa la wananchi wa sehemu hiyo. Ulifanya nini kuyalinda maslahi yao na kuhakikisha wanapewa bei ya ardhi muwafaka? Naamini wananchi hao bado ni maskini wa kutupwa. Na hivi ndivyo ilivyo kwa miji yetu yote. Wenyeji wanasukumwa zaidi kwenye ncha bila ya kufaidika na hodhi zao, wakati wenye madaraka wanaangalia tu. Lakini acha nisi jump to the conclusion, hebu tuambie majaaliwa ya wananchi wa asili ya eneo hilo?
 
Si tembo nauliza akina Tembo, ni ukoo huo walikuwa hapo Dundani na Kariakoo, Udoe street. Maana Udoe naona nyumba yao waliiuza limekuwa ghorofa.

Ndiyo nauliza Dundani bado wapo? Au na huko wameshavuta ndefu?

Hapa kazi na kasi tu....
 
Hata iwe ya nani,

Natumaini bei za mauzo ya hizo yatashuka na kuwa chini kulingana kama zingeuzwa enzi za awamu iliyopita.
 
Huo mradi wenyewe mbona kama umekwama maana ukilinganisha na ule wa wachina huu ndio ulitangulia kuanza kujengwa na sasa kama umesimama!
 
Mbunge,
Sina matatizo yeyote na bw. Iqbal kuwa ndiye mtamalaki wa eneo hilo. Tatizo langu ni kuwa kwa asli eneo hilo lilikuwa la wananchi wa sehemu hiyo. Ulifanya nini kuyalinda maslahi yao na kuhakikisha wanapewa bei ya ardhi muwafaka? Naamini wananchi hao bado ni maskini wa kutupwa. Na hivi ndivyo ilivyo kwa miji yetu yote. Wenyeji wanasukumwa zaidi kwenye ncha bila ya kufaidika na hodhi zao, wakati wenye madaraka wanaangalia tu. Lakini acha nisi jump to the conclusion, hebu tuambie majaaliwa ya wananchi wa asili ya eneo hilo?

Asili ni akili.
 
Uc

Uchukue kwa nguvu halafu uende mahakamani. Si ndio akili za yule mnyama tukiwaita tunapigwa ban. Akili za makalioni zina athar kubwa sana
Sheria inasema kama haujaendeleza eneo kwa mda wa miaka mi3 serikali inalichukua na kuligawa kwa watumiaji wengine.
 
Wabongo miji yetu bado sana tuchukue kama changamoto na kwenda Dodoma kujenga miji. Tuwaulize wanapataje fund sio kuwatafuta uchokonozi.
 
Wana jamvi,

Kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa magorofa unaendelea Kigamboni. Ni Kigamboni ndandani mbele Zoo na naambiwa unaitwa "Dege Eco Village".

View attachment 419269

Wengi wa wafanyakazi ni wazungu wenye asili ya Kituruki. Kazi inafanyika usiku na mchana.

Wenye ukweli kuhusu mradi huo mtujuze.

Karibuni wanajamvi.

=====
BAADHI YA MAJIBU:
MBUNGE:

====
MDAU:
Ukishajua mwenyewe ni nani utafaidi nini, kwanini usiwaze yako?story za kijiweni hizo
 
Wana jamvi,

Kuna mradi mkubwa wa ujenzi wa magorofa unaendelea Kigamboni. Ni Kigamboni ndandani mbele Zoo na naambiwa unaitwa "Dege Eco Village".

View attachment 419269

Wengi wa wafanyakazi ni wazungu wenye asili ya Kituruki. Kazi inafanyika usiku na mchana.

Wenye ukweli kuhusu mradi huo mtujuze.

Karibuni wanajamvi.

=====
BAADHI YA MAJIBU:
MBUNGE:

====
MDAU:
Kwanza kabisa Waturuki sio Wazungu na wala sio Waarabu .Waturuki ni Waturuki tu Je Serikali ya Rais Magufuli haina habari?
 
Binafsi nimeshatembelea miradi yote miwili yaani DEGE na AVIC.
AVIC unaeleweka zaidi na nyumba zao zimekaa vizuri ni bungalows na villas, DEGE naona kama wanajenga hostels. Anyway, take your time utembelee ufanye uamuzi mwenyewe.
zitakuwa ni sehemu za kuishi watz au kutakutakuwa wageni wawekezaji...........nakumbuka mradi huu ulianza enz za jk..sijawahi kupata maelezo ya kina kuhusu hii miradi
 
Back
Top Bottom