Ujenzi: Kipi kinaanza, plaster au ceiling joists?

Ramthods

JF-Expert Member
Jun 2, 2009
515
186
Wadau,

Nipo kwenye mchakato wa kujenga kwa sasa. Nimekwisha paua tayari.

Nimeuliza mafundi, ni nini kinafuata kati ya kupiga paster au ceiling structure (vile vimbao vidogo vidogo vya 2x2 inch kwa ajili ya ceiling), na kila fundi ana mtazamo wake tofauti.

Wengine wanasema unabidi uanze na plaster kwanza, na wengine wanasema ni lazima nianze na ceiling.

Kuna fundi amesema nikianza na ceiling, ntakapokuja kupiga plaster ile structure ya ceiling itakaa imara zaidi.

Nilikua nahitaji kusikia toka kwenye watu wenye uzoefu na hili. Kwa kawaida ni nini kinaanza?

Pia, naomba namba ya fundi wa plaster na floor.

Natanguliza shukrani.

Ram
 
plasta inaanza
 
Mkuu,

Kama fundi huyo alivyokujibu,kawaida ni kwamba lazima ceiling joists zianze ndipo plaster ipigwe.

Hii ni kwa sababu pamoja na kwamba ceiling itakuwa na support kutoka rafters,ukiweka joists kwanza ukija kuweka plaster ikikauka itasaidia ku-support mzigo mkubwa wa uzito wa ceiling.
 
Ili kupunguza uwezekano wa kuacha nafasi kati ya ukuta na mbao za ceiling, ni vizuri kuweka mbao za ceiling kwanza na kisha kupiga plaster. Halafu unaweka ceiling boards au gypsum boards na kuziba kabisa nyufa zote kwa kutumie cement nyeupe au materials nyingine.

Hapo nimeongea kwa uzoefu wangu na siyo ufundi wa ujenzi.

Kama uko Dar na unatafuta fundi basi wasiliana na Fundi Bakari, 0754 498893.
 
Mkuu,

Kama fundi huyo alivyokujibu,kawaida ni kwamba lazima ceiling joists zianze ndipo plaster ipigwe.

Hii ni kwa sababu pamoja na kwamba ceiling itakuwa na support kutoka rafters,ukiweka joists kwanza ukija kuweka plaster ikikauka itasaidia ku-support mzigo mkubwa wa uzito wa ceiling.

There you are expert.
 
Wasikudanganye fundi mtaaramu hawezi kukushauri eti uanze na Plaster. kwavigezo gani?. mimi nakushauri kitaaramu. anza na B/ring, ili utakapo kuja kupiga Plaster ubao wa B/ring, ubebwe na Plaster na hapatakuwa na uwazi ( upenyo ) kati ya ukuta na ubao wa ukutani
 
unaanza kutandaza kwanza mbao za ceiling halafu plaster inaanzia hapo kwenye ubao uliolala ukutani (wa 3x2) kushuka chini. ukianza na plaster ni kama unaforge.
 
Wadau,

Nipo kwenye mchakato wa kujenga kwa sasa. Nimekwisha paua tayari.

Nimeuliza mafundi, ni nini kinafuata kati ya kupiga paster au ceiling structure (vile vimbao vidogo vidogo vya 2x2 inch kwa ajili ya ceiling), na kila fundi ana mtazamo wake tofauti.

Wengine wanasema unabidi uanze na plaster kwanza, na wengine wanasema ni lazima nianze na ceiling.

Kuna fundi amesema nikianza na ceiling, ntakapokuja kupiga plaster ile structure ya ceiling itakaa imara zaidi.

Nilikua nahitaji kusikia toka kwenye watu wenye uzoefu na hili. Kwa kawaida ni nini kinaanza?

Pia, naomba namba ya fundi wa plaster na floor.

Natanguliza shukrani.

Ram

Hao waliokushauri uanze na plaster watakuwa siyo mafundi bali ni makanjanja!!

Waliokushauri uanze na ceiling joists watakuwa wamekushauri vizuri. Kawaida tunaanza na ule ubao wa kuzunguka ukuta ambako ndo zile draft za mbao za ceiling huwa zinakuja kuunganishwa (mafundi wengine wanaita blandaring). Ila huwa hatupigi zile draft zote kuzuia kuzichafua wakati tunapiga plaster! Ila ule ubao wa kuzunguka ukipigwa kabla ya plaster itasaidia kuziba ile mianya kati ya ubao na ukuta hivyo kusaidia kuzuia uchafu utakaokuwa kule darini kudondoka kwenye sakafu pia plaster husaidia kubeba uzito wa ceiling structure (maana unene wa plaster utakuwa karibia 1.5").

Baada ya plaster ndo unapiga zile draft, baadaye ceiling board.
 
Mkuu hata ukipiga draft yote, hakuna uwezekano wa kuchafua sana kwani bado ceiling board inakuwa bado haijatandazwa. Pia nadhani inasaidia kutosumbua plaster wakati wa kuunganisha mbao endapo plaster itakuwa imeshapigwa.

Mara zote huwa napiga draft yote ya ceiling kisha nafuatisha plaster. Sababu za msingi ni kama ambavyo wewe na wadau wengine wameshasema.

Ila kuna kitu kingine ambacho kwa maoni yangu watu huwa wanakosea. Nacho ni pale ambapo nyumba yenye veranda mbele au nyuma basi hufunga box usawa wa linter ya nyumba nzima na kupandisha tofali juu yake. Hii inasababisha kuwepo n kitu kama box/shimo. Mimi huinua box na kulifungia kwenye usawa wa kupaulia. That way, huwezi kuona box kwenye veranda!
 
Kwani zile draft zikichafuka kuna tatizo gani?
 
Hapa sijaelewa.Naomba nifafanulie, ikibidi kwa picha.
Vipi ka mtu keshakosea, unamshauri afanye nini kwenye veranda yake ili box lisioneka.
 
Sina picha kwa sasa ila kama nikipata muda au kama ukipenda tunaweza kuwasiliana kwa njia nyingine ili nikupe maelezo zaidi.

Ila kama mtu keshaweka box kwenye veranda, nahisi itakuwa ngumu kwa sababu linta box itakuwa imefungwa kwa nyumba nzima.
 
Thax.

Hapo unaposema box ndo sielewi pia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom