Ujenzi Jiji la Dar unafuata Master City Plan? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujenzi Jiji la Dar unafuata Master City Plan?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by August, Jul 14, 2009.

 1. A

  August JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Hivui karibuni kumezuka mtindo wa kubomoa majengo ya zamani ambayo yalikuwa ghorofa nnne au chini ya hapo na kujenga mapya yenye ghorofa 8 kwenda juu, sasa ningependa kujua kwamba, wataalamu wetu pamoja na viongozi wanao toa building permit, je ujenzi huo unafuatana na city master plan au ndio bora liende?
  Pili ujenzi huo unaenda na uwezo wa miundo mbinu yetu? au na hapa ndio hivyo kifo cha wengi , maana sasa hivi tu bila kuongeza hayo majengo kuingia au kutoka city centre ni shughuli.
  Kwanini tusifuate mfano wa Stanbic ambao atleast wamejaribu kutoka katika msongamano wa city centre. Je wenzetu wakienda hizo study tour huwa wanajifunza nini?
  Kwa mfano kwa wenzetu mtu akitaka kujenga au kubadili jengo, kwanza lazima awaeleze majirani ili mwenye duku duku atalitoa, pili linahusu aina ya majengo yanayo ruhusiwa sehemu fulani eg jengo lisizide ghorofa 4 au tano ukitilia maanani ongezeko la watu na huduma nyingine ikiwa jengo litakuwa la ghorofa 8 na kuendelea.
   
  Last edited by a moderator: Jul 14, 2009
 2. zomba

  zomba JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: Nov 27, 2007
  Messages: 17,081
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 0
  Hakuna cha city plan wala nini, na kama kuna city plan, basi ni plan bomu. Hivi msongamano uliopo pale kati ya jiji la Dar na Kariakoo, halafu bado unaruhusu kujenga migirofa isiyo na parking, barabara ndogo, infrastructure mbovu. Halafu hiyo ni city planning, Kama amri yangu, hawa ma city engineers waliopo Dar. wote nawasulubu.
   
 3. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,399
  Likes Received: 432
  Trophy Points: 180
  And a very striking feature of that "very old masterplan"; there is no proper sewerage system. Two thirds of Dar Es Salaam proper is unplanned. Angalia ule mto msimbazi; halafu lile bomba la ocean road hospital. Hawa watawala kazi kula dona na kulala; vichwa hamna kitu!!
   
 4. A

  August JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  na kama hao city fathers etc etc wanaona kunaumuhimu wa kuendelea kujenga basi angalau wangeua upande moja wa mtaa kwa kuondoa hayo majengo ili kupisha upanuzi wa barabara, na upande mwingine ndio wajenge hayo maghorofa yao, mfano samora avenue wanaweza kuua majengo upande wa extelcoms na kuendeleza majengo marefu upande wa Twiga Bank, yaani kila mtaa finyu waamue kuondosha majengo upande moja na kuwekeza upande wa pili, ili bara bara ziweze kuongezwa upana.
   
 5. Mwalimu

  Mwalimu JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 1,475
  Likes Received: 227
  Trophy Points: 160
  Hivi kwani ni lazima kujenga city center? Kwa nini tusiiache kama ilivyo na majengo yake ya zamani iwe Old Dar es salaam then tuwe na mji mpya eneo jingine? Yaani utafikiri mkoa wa Dar es salaam ni city center peke yake?
   
 6. F

  Fratern Member

  #6
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 18, 2009
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Kama zilivyosera nyingine hapa nchini, ramani za mipango miji mfano wa jiji la Dar es Salaam bado ni ileile tuliyorithi kutoka kwa mkoloni na tatizo letu kubwa ni ukosefu wa utashi wa kisiasa wa kuboresha mipango miji yetu. Utashi wa kisiasa ungelikuwepo kama uliveyoweka kwenye michezo mh!! 'of all the development ailments in this country' Jiji la Dar lingelikuwa limeendelea na lingelikuwa mfano wa kuigwa nchini na Africa Mashariki.

  Miaka ya 1990s, wadau wa Tanzania kimaendeleo, hasa Japan, walikuja na pendekezo la kujenga barabara ya juu eneo la posta mpya, ukienda hadi ufukweni mwa bahari mpaka eneo la stationi (bandarini). Ukweli ni kwamba tatizo tunaloliona leo, foleni ya kukera hadi mtu unatamani kufa, wenzetu walivyo viona mbali, walishaliona miaka kumi kabla. Na, tukumbuke wakati huo ndio Tanzania ilianza kuibukia kuwa mteja wa magari mengi ya Kijapani; na kwa kasi tuliyokuwa nayo ya kuagiza magari kutoka Japan, wao wakaona kwa kasi hiyo, miaka kumi ijayo kama miundo mbinu haitaboreshwa basi, Dar City Center patakuwa hapatoshi. Na kweli, hii ndio hali tuliyonayo leo hii. Tulikuwa vipofu! Na badala yake, tuliwaomba fedha hizo zikatengeneze barabara za manispaa zikiwemo za jiji (City Center) na Kariakoo - ukarabati uliojumuisha matengenezo ya mafereji ya maji machafu, ambao bado nawalaumu Mainginia wetu kwa kutokubuni miundombinu mibovu. Na hii inatokana na wao kutohuisha kisomo chao na uhalisia wa mazingira ya kazi. Ki vipi?

  Dar es Salaam ni eneo ambalo ardhi yake ni ya mchango kwa asilimia 90+! Mchanga unatabia ya kusafirishwa kwa maji na upepo kirahisi sana. Hivyo utengenezaji wa miundo mbinu lazima uzingatie hili kwa kuunda miundo mbinu ambayo ambayo INA SLOPU AU "30 - 60 DEGREES GRADIEN" hasa eneo la CITY CENTER. Yaani ningelikuwa ni mimi mbunifu wa miundo mbinu hiyo, kuanzia Kariakoo, miundo mbinu yote ya maji machafu ingelizingatia hili na iwe na upana & urefu wa mita tatu (i.e. 3sqm) ikiambatana "soak-pits/cess-pits kwa ajili ya kuchuja mchanga na mifuniko mikubwa kwa lengo la kurahisisha uzibuaji au utoaji wa taka ngumu.Kwa mfumo huu, tunategemea maji kutoka Karikoo au City Center yawe yamefika Baharini (kwa wana mazingira niwieni radhi - I do understand your environmental concerns) ndani ya dakika kumi hadi kumi na tano.

  Kwa vile Dar es Salaam, iko kwenye usawa wa bahari na kwa vile mandhari yake ni ya tambarare nadhani utengenezaji wa barabara za juu unaweza ukawa wa garama kubwa sana lakini hata hivyo kwa hali ilivyo City Center, garama haikwepeki. Na hata hivyo, Dar es Salaam inaongoza kwa ukusanyanyi wa kodi nchini. Na, kwa mantiki hiyo, naomba nitoe mfano huu. Kwa mfugaji mwenye ng'ombe wa maziwa, yule ng'ombe ambaye anakamuliwa maziwa mengi huwa anampa majani kwa wingi pamoja na virutubisho vyenye madini ili aendelee kumkamua na kumwepusha na maradhi hasa ya upungufu wa chokaa! Hivyo, na kwa Dar es Salaam, ingelitakiwa ipewe 'majani kwa wingi' yaani kwa kuboresha miundo mbinu yake hasa ya usafiri ili wananchi na wafanyakazi waendelee kuzalisha zaidi. Kwa hili, naomba niseme, nchi kama nchi imeshindwa kutumia rasilimali watu ipasavyo. Ki vipi?

  Sehemu kubwa ya muda wa wafanyakazi unapotea njiani kwenye usafiri, muda ambao ukithaminiwa kifedha, nchi inapotesa fedha nyingi sana. Hii ni sehemu moja ya kufanyia utafiti wa kina na ukweli utajulikana. Watu wengi wanaanza kazi zao saa mbili kamili. Lakini ili mtu aweze kufika ofisini na kuanza kazi muda huo inambidi aamke saa kumi na moja kamili kwa wale wa karibu na kwa wale wanaokaa mbali kama Tegeta na Kibaha/Kibamba au Mbagala, inawabidi wengine waamke saa kumi usiku. Mpe mtu huyu lisaa limoja la kujiandaa na kuwaandalia watoto wake kitu cha kula mchana. Ina maana watu wengi wanakuwepo barabarani kati ya saa kumi na moja hadi kumi na mbili asubuhi kwenda kazini ambako atafika kati ya saa mbili na nusu saa tatu! Kwa vile alitoka nyumbani bila kifungua kinywa, itambidi saa nne au saa tano akanywe chai. Akirudi, ukichukulia uchovu wa kukaa kwenye foleni, wengine kutoka walikotoka hadi wamefika kazini alikuwa amesimama kwenye basi au kunasehemu imembidi atembee, hivyo kafika kazini yuko hoi, kesha choka tayari! Akinywa chai kidogo tu, lazima atasinzia, mpe nusu saa au lisaa; hata kama atakuwa macho, basi mwili/akili imechoka atakuwa yupoyupo tu ama apiga gumzo au anajisomea gazeti. Muda wa mwajiri unatumika huo! Itafika saa sita, atajisikia ahueni kidogo atafanya atakachoweza kufanya kwa muda wa lisaa limoja au pungufu; saa saba huyu, 'lunch-time!' Mpe lisaa limoja, akirudi, mwili unasema asante, atapumzika au atakuwepo tu kwa muda; kisha atafanya kazi kwa lisaa limoja tena. Saa tisa, mawazo yanahama na anaanza kufikiria jinsi ya kurudi nyumbani hasa kwa wale wanaofunga ofisi saa kumi. Wengi wanaofunga ofisi saa kumi na moja ndio hivyo, mwendo mdundo usafiri wa tabu kama tulivyokuja, atarudi nyumbani ambako atafika kati ya saa moja na saa mbili au saa tatu usiku; kwa wengi ni saa mbili! INACHOSHA JAMANI, NA HII HAIJALISHI ETI UNA GARI AU HUNA; LEO HII MWENYE GARI NA ASIYEKUWA NALO DAR, WOTE NI SAWA! TENA MWENYE GARI ANAHASARA KUBWA ZAIDI. Wachumi mnalijua hili!

  Literally speaking, the life in Dar is nothing but visious cirle of poverty - all because of POOR CITY PLANNING and TECHNOCRATS WHO HAVE REFUSED TO THINK because they have brought the 'village thinking' to live with it in the CITY. Philosophically, this is a fact. Think of it, and if need be please, register your objection.

  Kwa hali hii ilivyo Dar, waajiri wanaingia hasara sana, tena mwajiri mkuu akiwa ni serikali! NO! WE HAVE TO DO SOMETHING.

  "Tumia fedha upate fedha." Cha kuwashauri viongozi wetu wa nchi juu ya hili ni wao kujitwika moyo wa kuthubu na kulivalia njuga swala la usafiri Dar. Kuwepo na utashi wa kisiasa wa kuboresha miundo mbinu ya barabara kwenye Jiji la Dar es Salaam. Hata kama ni kukopa, kwa mfano Benki ya Dunia, tufanye hiyo, tujenge barabara zetu na kidhamiria tutafanikisha hili, watu wetu watafanya kazi, na fedha tuliyokopa tutarudisha. Tukope leo na sio kesho kwani bei ya leo ni tofauti na ya kesho. "Let us be STRATEGIC" - kwani unaposimamia taasisi au nchi, si kitu ambacho kitakufa kesho kutwa bali kikiangaliwa vizuri inaweza kuwepo mika miambili ijayo, na maisha yake kama kiongozi "is just a fraction." So, ethically, what we ought to do is to contribute the best we can in the already established and newly established strategic encounters as this is the only way one leaves behind a 'legacy' for others to emulate on otherwise, we stand a chance not to be remember for anything for having subscribed our pursuts to daily events, which hadly last long as they can and passby the wind!

  Tusiogope kukopa ili kuboresha Jiji, bali tukope na sisi wenyewe na vizazi vyetu watalipa. Kwani kung'ang'ani hili ni kujichimbia kaburi la umaskini wenyewe, na watoto wetu watakao salia watatushangaa kwa kutokufikiria kwa umakini. Afadhali ukakopa leo ukatozwa riba ya shilingi hamsini (whatever this means in cash today), na ukaboresha mambo yako ili mtoto wako akikua akiyakuta atakushukuru na kukuona baba ulifanya jambo la maana na ataiona garama uliyotumia ni rahisi kuliko ya wakati huo, mtoto wako atakapoenda kukopa na kutozwa riba ya shilingi 600. Hivyo, afadhali tunaloweza kulifanya leo tulifanye lisisubiri kesho. Hatuwezi kuendelea bila kukopa, bali tukope ila tukumbuke maadili ya kukopa ni KUPANGA NA KUTUMIA VIZURI TULICHOKOPA, ili tuwe na udhibitisho wa kuwaonyesha watoto wetu na wajukuu zetu kuwa - Jiji tunaloliona zuri hivi leo hii (wakati huo huko mbeleni), lilikuwa hivi ikatulazimu kukopa, na mkopo huu tunaoulipa ndio ulitutoa tulikokuwa hadi hapa tulipo.

  Hii inamaanisha kwamba, ili hili litimie, lazima tuwe WASAFI na WAKWELI kwenye utendaji wetu kwani "truthfulness and objectivity are the essential componets in creating a Legacy or rather a lasting Impact."

  Tena, viongozi wetu wa Tanzania wajitahidi pamoja na mambo mengine, kurudia kuchora mchakato mpya wa jiji la Dar es Salaam, na tuwe na mipango mahususi ya kuyafanyia kazi yale tunayoyapanga. Miaka 30 na ushee inafika sasa tangu Mbezi Beach ianze kujengwa, lakini hakuna sehemu yenye miundo mbinu mibovu kama huko, ikifuatiwa na Mikocheni na kinachonishangaza ni bei ya juu nyumba kwenye maeneo haya! Hivi, thamani ya nyumba si pamoja na uhalisia wa upatikanaji wa huduma ya maji safi & taka. na barabara? Another instance, where our technocrats have refused to think!

  Uboreshaji wa miundo mbinu ya jiji hasa barabara inasua kutokana na GARAMA KUBWA ZA UJENZI WA BARABARA! Lakini inakuwaje garama ya kujenga barabara Tanzania ni kubwa kuliko Uganda ambayo haipakani na bahari na tena haijajaliwa kuwa na rasilimali za ujenzi wa kama vile mawe kama ilivyo Tanzania! Kuna kitu, na bila shaka hili ni sehemu moja inayonukia rushwa ya kisomi! Tunaziomba mamlaka husika zifanyie kazi hizi na ikibidi watoe mchanganuo-kazi na garama ya kila kitu kinachohitajika kujenga kilomita moja ya barabara kwa kila mkoa. Siamini, na wala haiingii akilini kuwa kujenga barabara sehemu ya tambarare kama Dar es Salaam ni sawa au zaidi ya kujenga kilometa moja hiyohiyo mkoani Kilimanjaro au Mwanza?? Bila shaka hii ni rushwa, na lazima iangaliwe la sivyo, WE ARE RUINING THIS COUNTRY WITH OUR OWN HANDS! THEN, WHAT WHAT HERITAGE ARE WE LEAVING BEHING FOR OUR CHILDREN AND GRAND-GRAND CHILDREN.

  My brother and Sister, I am worning out!

  See you next time, (Let me concentrate on my Master - Dissertation).

  Bye.
   
 7. M

  Morani75 JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 1, 2007
  Messages: 619
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Heshima mbele wakuu.... ni kwamba kitu inaitwa "Masterplan" haipo kwenye misamiati/kamusi ya waheshimiwa wenye kufanya maamuzi..... pita Kariakoo kisha uje uniambie kuna mipango miji mule ndani......
   
 8. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Dar city plan ipo isipokuwa hakuna mtu anaweza kuifuata iwe serikali au watu binafsi kwa ufupi no implementation!
  Ukinunua kiwanja popote Dar (kwa watu binafsi) ukienda ardhi na halmashauri watakwambia eneo hilo limetengwa kwa kazi fulani maalum lakini maofisa wanakwambia unaweza kubadilisha the plan kama unataka!!! so plan nzima imeharibika nakuwa meaning less kwasababu ya corruption shame!, kila siku inabadilishwa kwa matumizi mapya ya serikali na watu binafsi "bora kuwahi" ndio maisha yetu.
   
 9. A

  August JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 18, 2007
  Messages: 4,505
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  naona imefika wakati sasa hivi serikali/ wahusika kusimamisha ujenzi wa maghorofa kariakoo, city centre na majenzi mengine sehemu yoyote tanzania ambayo yata pingana na kuwepo kwa miundo mbinu inayo weza kuhimili maendeleo hayo, ama sivyo itatu gharimu zaidi siku zijazo, angalia Mji/Mkoa wa Arusha na Uhuru Road, pale inabidi majengo ya upande moja yaondoke ili barara ipanuliwe au mji uhamishwe kabisa.
   
 10. e

  eddy JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2009
  Joined: Dec 26, 2007
  Messages: 9,361
  Likes Received: 3,761
  Trophy Points: 280
  hivi ule mradi wa ex-balozi wa usa na magufuli wa kujenga homes 75,000 uliishia wapi?
   
Loading...