Ujenzi barabara za mji wa Kahama ufisadi mtupu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujenzi barabara za mji wa Kahama ufisadi mtupu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pambe S, Apr 10, 2012.

 1. P

  Pambe S Member

  #1
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Leo kwenye kipindi cha maswali na majibu bungeni, James Lembeli, yule mbunge wa Kahama aliuliza swali akitaka kujua ni kwanini moja ya barabara katika mji wa Kahama imejengwa chini ya kiwango, kiasi gani mkandarasi kalipwa na hatua gani zimechukuliwa dhidi ya mkandarasi.

  Katika majibu yake waziri katika ofisi ya waziri mkuu amesema mkandarasi yeyote anayefanya kazi chini ya kiwango huchukuliwa hatua kali, na kwamba kipande cha barabara kilichojengwa ni km 1.5 na tayari serikali imelipa zaidi ya tsh billion 1 na mkandarasi kaamuriwa kurekebisha sehemu korofi kwa gharama zake.

  Mimi ni mkazi wa mji huu wa Kahama, kwa kweli ni aibu tupu. Barabara hii tuliambiwa inajengwa kwa kiwango cha lami, (barabara imara ina layer zaidi ya 3 za material mbali mbali) kilichofanyika ni kuweka layer moja ya moramu na kunyunyizia MCO(kimiminika cheusi kinachowekwa kabla ya lami) halafu serikali ya ccm ikapitisha malipo ya mamilioni ya shilingi kwa mkandarasi- Jasco Construction ya jiji Mwanza kwamba kipanda hicho ujenzi tayari.

  Hali ilivyo kwa sasa ni aibu, barabara tayari ina mashimo na kingo (shoulders) zilishazolewa na maji hata mwaka haujaisha.

  Kahama ni wilaya yenye hazina kubwa ya madini, Migodi mikubwa miwili Buzwagi na Bulyanhulu ipo katika wilaya hii lakini huduma za jamii ni duni kupita maelezo, umeme si wa uhakika hata kwenye maeneo nyeti kama hospitalini wakati katika migodi, kwa matapeli wanaojiita wawekezaji (Barrick) ni wa masaa 24, barabara za mjini na vijijini zina hali mbaya wakati helikopta moja tu huja kuchukua dhahabu yetu yenye thamani ya zaidi ya billion 43 (rejea taarifa ya TRA kuhusu wazalendo wapenda nchi yao waliojaribu kuteka helikopta katika mgodi wa Geita mwaka jana) helikopta hizi huja zaidi ya mara 3 kwa mwezi kwa kila mgodi kuchukua dhahabu, fanya hesabu kuna migodi zaidi ya 5 kanda ya ziwa pekee.

  Kwa ujumla kila mahali ni ufisadi! CCM hii inatufilisi hata maliasili zetu, lakini wasubiri 2015
   
 2. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #2
  Apr 10, 2012
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 802
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Mpaka ifike 2015, mtabakiwa na mapango na si mashimo!
   
 3. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #3
  Apr 10, 2012
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 13,953
  Likes Received: 1,279
  Trophy Points: 280
  sure jirani yangu, barabara hiyo haiendani na kiwango cha pesa. Ukandarasi ni ufisadi. Mabonde kwenye 'kilami'
   
 4. Ta Kamugisha

  Ta Kamugisha JF-Expert Member

  #4
  Apr 10, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 3,003
  Likes Received: 1,077
  Trophy Points: 280
  unataka tufanyeje sasa? si ndo serikali yako?
   
 5. c

  collezione JF-Expert Member

  #5
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 360
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Aje Mwigulu atujibu hapa. Juzi alikua anatumbumbaza, eti kila mtu afanye kazi.

  Utafanyaje kazi, hakuna barabara, umeme shida, maji shida. Afu wenyewe wanakula hela za kifisadi. Afu eti sisi wananchi chini, tunapaswa kufanya kazi kwa bidii tuuuu(wenyewe kula, sisi kazi)...duh
   
 6. Hute

  Hute JF-Expert Member

  #6
  Apr 10, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,059
  Likes Received: 3,923
  Trophy Points: 280
  ni kweli unalolisema, mimi nipo kahama leo hii, barabara za vumbi pamoja na kwamba mzunguko wa pesa hapa ni mkubwa kuliko dar. ni mji wa kibiashara sana, ukipangiwa kufanya kazi kahama, shukuru Mungu. lkni serikali imepasahau sijui au ndo ufisadi anaousema jamaaangu?
   
 7. Kimbunga

  Kimbunga Platinum Member

  #7
  Apr 10, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 13,012
  Likes Received: 1,817
  Trophy Points: 280
  Hapo kwenye barabara kama ni kweli kwamba amefanya priming badala ya lami basi huyo Mkurugenzi ana moyo kama wa kishujaa!
   
Loading...