Ujenzi barabara ya Mwenge - Morocco washika kasi Tigo HQ parking hali tete, hongera mbunge Mdee kwa kusimamia ilani ya CCM

Katika suala la miundombinu, Magufuli ni wakupigiwa mfano barani Afrika kwa sasa. Hapo nampa "kudos" Rais wangu. Kweli kabisa anajitahidi mno maeneo mengi, tena yenye kuonekana kwa dhahiri kabisa. Nahisi hii itakuwa kete yake muhimu itakayo mpambanua kipekee kuelekea chaguzi za 2019 na 2020.
Dar barabara za ndani mitaani ni full lami mpaka barabara kuu....hata ukiwa na gari iliho chini sio ishu tena. Unapêta tu.
 
1. Hivi upande ule wa CoICT kijitonyaa wanajenga nini maana nimeona wamechimba kama handaki reeeefu na wameweka scaffolds...

2. Barabara ya kutoa mwenge uelekeo wa tegeta upande wa kushoto sijaona bango a nì shughuli gani inaendelea upande huo ila inaonekana kama kuna barabara inajengwa...

3. Hiyo hiyo tegeta, wiki iloisha walikuwa waatifua ile hifadhi ya mwendokasi..sijajua nini kiaendelea.
Mwenye kujua ...
 
Katika suala la miundombinu, Magufuli ni wakupigiwa mfano barani Afrika kwa sasa. Hapo nampa "kudos" Rais wangu. Kweli kabisa anajitahidi mno maeneo mengi, tena yenye kuonekana kwa dhahiri kabisa. Nahisi hii itakuwa kete yake muhimu itakayo mpambanua kipekee kuelekea chaguzi za 2019 na 2020.

Ni kweli hili ni kete yake muhimu, ila kete yake ya uhakika ni vyombo vya dola!
 
Hahahaa.......mabadiliko!
Ok basi nikajua tayari
downloadfile.jpeg
 
Kiukweli mabadilko makubwa yameanza kuonekana na hasa kuanzia Mwenge hadi Bamaga. Nadhani pale zinajengwa njia 8 maana jengo la Nakiete limenusa barabara kabisa.

Pale Tigo HQ makumbusho ndio hakuna parking ya magari kabisa barabara iko jirani na ngazi za kuingilia mjengoni. Binafsi nafurahishwa sana na maendeleo haya.

Pongezi ziwaendee Rais Magufuli, waziri wa ujenzi mh Kamwele, RC Makonda na mbunge Mtulia na Halima Mdee kwa usimamizi na utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM.

Maendeleo hayana vyama!
Hizi barabara 8 zikifika pale mwenge kwenye robots(mataa) zina converge au inakuwaje? Au panajengwa flyover?
 
Pale ni mataa na ndio maana foleni itazidi kuwepo. Yaani hii mwenge morocco ilikua haina haja ya kupanua...wangepiga flyover morocco na nyingine mwenge wangemaliza shida ya foleni dakika hiyo hiyo.
Hizi barabara 8 zikifika pale mwenge kwenye robots(mataa) zina converge au inakuwaje? Au panajengwa flyover?
 
Mheshimiwa tafadhali afikirie wa Makongo juu wanaoteseka nana vumbi kila siku badala ya kujenga za..baharini zinazokwendaga Masaki tu. Wale ndio wanyonge??????? Jamani. Makongo magari yanatoka kimara, salasala, mbezi beach, tegeta,etc!
Kweli waonewe huruma! Vumbi siyo masiara!
 
Pale ni mataa na ndio maana foleni itazidi kuwepo. Yaani hii mwenge morocco ilikua haina haja ya kupanua...wangepiga flyover morocco na nyingine mwenge wangemaliza shida ya foleni dakika hiyo hiyo.

Nchi hii kila mtu ni Engineer
 
Ni kweli hili ni kete yake muhimu, ila kete yake ya uhakika ni vyombo vya dola!
Mkuu, issue ya vyombo vya dola siyo tu ni kete yake ya kipekee, bali pia ni kombora la maangamizi achilia mbali silaha ya kinyuklia ya masafa marefu, yaani NEC. Ha ha ha....
 
Dar barabara za ndani mitaani ni full lami mpaka barabara kuu....hata ukiwa na gari iliho chini sio ishu tena. Unapêta tu.
Mbunge wangu mnyika tu ndio naona katususa hii mbezi ya msigani mpk malamba mawili,njia nyingi za ndani ndani bado azieleweki!
 
Mheshimiwa tafadhali afikirie wa Makongo juu wanaoteseka nana vumbi kila siku badala ya kujenga za..baharini zinazokwendaga Masaki tu. Wale ndio wanyonge??????? Jamani. Makongo magari yanatoka kimara, salasala, mbezi beach, tegeta,etc!
Kweli waonewe huruma! Vumbi siyo masiara!
Huko mbunge wenu ni Dr Shukuru Kawambwa au ni nani?!...... Siwajui vizuri wabunge wa Coast region!
 
Sijajua nini kitafanyika kuwasaidia waenda kwa miguu kuvuka hii barabara. Njia nane kuvuka sio jambo dogo, linaweza kusababisha majanga.
 
Ni muda sasa wa kujenga barabara za juu, hizi za chini zimekuwa shubiri kwa wenye majengo maana ili kufanya upanuzi lazima watu waondolewe kutoka maeneo yao...
 
Back
Top Bottom