Ujauzito umenivunja nguvu na je pilipili ni salama kwa mwanamke mjamzito?

............Mwenzenu Mungu amenishushia baraka za ujauzito, lakini imenivunja nguvu sana.

Duh hii mimba yako ya ngapi kudaka? Kwanza pole,
Mimba bana huwa zinakuwa zinavituko kuna mke mmoja wa rafiki yangu mimba yake ilikuwa inanipenda kweli kweli mm asipo niona anajisikia upweke na asipo sikia sauti yangu halali alafu ikamchukia kweli kweli mme wake hizi mimba unaweza poteza urafiki bure hivi hivi lakini jamaa alikuwa anaelewa kwa kupewa ushauri na wakubwa.
Kama wewe imependa pilipili basi kazana kula ili ikue na kustawi vizuri, lakini angalia mtoto nae anaweza zaliwa akawa mkali kama pilipili.Lini utajikomboa tuanze kuandaa baby show na nepi?
 
Na wewe walewale.si kasema ujauzito wa kwanza? arrrrrgh.
 
hongera Pretty, lakini pia vumilia tu yataisha hayo yote siku utakapomhold baby wako mikononi, utasahau kila aina ya maumivu in just a sec. pilipili sidhani kama ni mbaya kitaaalamu ila tu punguza, uwe na kiasi. all the best.
 
hongera mwaya!!! nadhani ni kawaida tu kwa mimba kuja na vimbwanga kama hivyo!!!
kula mamii wala usijali, si kuna mazoezi ya wajawazito?? either case hata ukijifungua pia bado unaweza kufanya mazoezi ukarudi into shape!!

dadaangu alikuwa anamfungisha safari mumewe toka King'oko mpaka upanga kununa mishikaki ya sh. 20 yenye, there was no cheating maana anagundua!!! halafu akikutaka uende kwake she didnt care uko wapi na usipoenda siku nyingine ukijipeleka tu anakufukuza au ananuna mpaka unaondoka!!!!!!!!

alikuwa anakula pilipili sana hadi kwenye mkate, Jr. alipozaliwa macho yalikuwa yanatoka machozi ila mi sijui kama ni sababu

Wewe jaribu kupunguza pilipili
 
mimba zina vimbwanga sana, mie ya kwanza ilivyoingia tu nilimchukia mr balaa, yaani nilikuwa nikimuona nakacrka naliaa tu, mama yake alimshauri anihame kwa muda, na akikaa wiki huko cjamuona naliaaa nataka nimuone akija tu lisaa nimeshamchoka ctaki kumuona...khaaa jamani wacheni tu....
 
hongera sana, mimba huwa zina complecation hasa za kwanza. Na hapo ndio utaona hekima ya kuwaheshimu wazazni hasa mama zetu. umetuambia uko masomoni, ila hujatuambia mzazi mwenzako yuko wapi au naye ni mwnafunzi? ni mumeo au umepata kwa bahati mbaya? lakini pengine haya maswali sio ya msingi sana, turudi kwenye mada, wataalamu wa sayansi wanasema uhitaji wa chakula wa kiumbe kilicopo tumboni (fetal enegry requirement) ni mkubwa sana. mfano kati ya 50-60 ya glucose hupelekwa kwenye fetal (Sjaastad, 2003). pia kiwango kikubwa cha chakula (protein) kinahitajika kuandaa maziwa kwa ajili ya mtoto akishazaliwa (mathew & Van Holde 2005). ndio maana unajisikia njaa sana, kwa sababu mahitaji yameongezeka mara dufu

wewe una bahati kama unakula, maana kuna baadhi ya watu huwa wanakataa kula (hali hii husababisha hypoglycemia) ambayo kiafya si nzuri. kuhusu pilipili sina uhakika wa madhara yake, ila nakushauri upunguze. sambamba na hili nakushauri ule kwa wingi samaki (wana Decosahexanoic acid) ambayo ni nzuri kwa brain ya mtoto (inajenga uwezo wa kumbukumbu-cerebral cortex). pia mwambie mzee ajitahidi kunununulia mboga mboga za majani, wanut oil, na rapeseed oil (zina omega 3 kwa wingi) ambayo ni raw material ya ecosanoids na inazuia kuzalishwa kwa harmful ecosanoids kutoka kwenye omega 6. samahani nimetumia lungha nyingine ya kitaalam (nimeshindwa kupata tafasiri nzuri) kama hutojali unaweza ukanitumia PM nikakufafanulia zaidi.
 
.............Mzazi mwenzangu wala sio dent na ni mume wangu halali hivyo mimba nimepata kwa bahati nzuri kabisaaa.
 
............Mwenzenu Mungu amenishushia baraka za ujauzito

Hivi pilipili ni salama kwa kwa mwanamke mjamzito? Kuna wadada hapa ambao labda kipindi cha ujauzito mlikula pilipili vipi hazikuwadhuru? Mie mwenzenu mpenzi sana wa pili pili na katika hali hii bado nakula, nakatazwa kula lakini wala siachi.Je pili pili ina madhara yoyote kwa unborn child?
Dada Pretty kama umeolewa ongera sana, ushauri wangu punguza kula pilipili zinaweza kumuathiri/kumdhuru mtoto akazaliwa na matatizo ya macho! Maana unachokula ndicho anachokula.
 
Hongera mpz, Mola akuongoze ujifungue salama..Yanayojiri wakati wa ujauzito ni kati ya matatizo tunayopitia wanawake wengi, vumilia na muhimu ni kuwa karibu na docta kimawasiliano ukiona una tatizo kubwa..
Mie sikupenda kabisa pilau,halafu chipsi nilikuwa nataka za pale panaitwa 'american chips' na 'wizard camp' tena naenda mwenyewe,coca ndo usiseme sikuiacha kabisaa..kwingine zilikuwa hazipandi,leo hii nacheka nasema sijui nilikuwa nawaza nini..
 
Mimba, mimba mimba, ndio furaha ya wanandoa ingaa ina usumbufu wake. Uzuri usumbufu huo ni wa mpito tu kwani hata kwenda Mbinguni ni lazima ufe kwanza bila kujali kifo hicho ni cha namna gani. Hongera mrembo (Pretty) kwa kudaka vizuri mdako wa husband nakuombea kwa Yehovah Mungu akujalie janadume. AMEEEEEEEEEEEEN.
 
............Mwenzenu Mungu amenishushia baraka za ujauzito, lakini imenivunja nguvu sana. Yaani muda wote naishiwa nguvu na njaa kuuma kila wakati. Kila baada ya nusu saa nahisi njaa kali sana.........hata nikila vp lakini muda mfupi tu njaa.Huu ndio ujauzito wangu wa kwanza basi naogopa huko kula kula nisije kunenepa bure.
..........3 weeks ago nilikuwa hoi, chakula changu kilikuwa ni drip tu, maana nilikuwa nasikia njaa lakini chakula hakiliki hadi ikabidi niwe admitted hospital.Nashukuru nimeshatoka hospital lakini sasa hivi ni njaa kwenda mbele. Nimeanza second trimester sasa lakini bado tu naishiwa nguvu, sijui hata nifanyeje?
Mimba kumbe ni shughuli jamani...........watu tumetolewa mbali kumbe.Na hivi nimenasa huku nipo masomoni mhhhhhhh!!

Hivi pilipili ni salama kwa kwa mwanamke mjamzito? Kuna wadada hapa ambao labda kipindi cha ujauzito mlikula pilipili vipi hazikuwadhuru? Mie mwenzenu mpenzi sana wa pili pili na katika hali hii bado nakula, nakatazwa kula lakini wala siachi.Je pili pili ina madhara yoyote kwa unborn child?

Kwanza hongera sana Mrembo....inaelekea ulikuwa so busy LOL! na ndiyo maana kuna kipindi ulikuwa unapotea hapa mtaani hahahahahah I am just joking....LOL! na hatimaye mambo yamejipa. Nakumbuka dada mmoja ni mpenzi sana wa pilipili sasa kila apolkuwa mjamzito alikuwa hawezi kula chochote mpaka kuwe na pilipili kama tano au zaidi. Kama unazijua pilipili kichaa vidogo dogo lakini vikali sana unaweza kula nusu tu na usikimalize sasa yeye alikuwa anaweza kula vitano au hata zaidi kwa mlo mmoja. Mama yake alikuwa anamkanya sana kwamba apunguze kula mapilipili maana kwenye ujauzito zinaweza kuwa na athari, lakini watoto wote walizaliwa salama salmini bila matatizo yoyote, lakini kumbuka too much of anything is harmful...hivyo jitahidi kupunguza pilipili kidogo na pia usisahau kula vitamins zenye umuhimu mkubwa kwa mama wajawazito ili kuhakikisha mtoto anazaliwa na afya njema. Once again congratulations and all the best.
 
Hongera sana na kila kheri. Mungu akubariki uzae mtoto masculine kama Luca Brasi
 
Hongera sana, tunamngoja kwa hamu huyo mjomba wetu, usiogope kula ukipata hamu we kula tu.
 
Back
Top Bottom