Ujauzito umenivunja nguvu na je pilipili ni salama kwa mwanamke mjamzito?

Pretty

JF-Expert Member
Mar 19, 2009
2,575
552
............Mwenzenu Mungu amenishushia baraka za ujauzito, lakini imenivunja nguvu sana. Yaani muda wote naishiwa nguvu na njaa kuuma kila wakati. Kila baada ya nusu saa nahisi njaa kali sana.........hata nikila vp lakini muda mfupi tu njaa.Huu ndio ujauzito wangu wa kwanza basi naogopa huko kula kula nisije kunenepa bure.
..........3 weeks ago nilikuwa hoi, chakula changu kilikuwa ni drip tu, maana nilikuwa nasikia njaa lakini chakula hakiliki hadi ikabidi niwe admitted hospital.Nashukuru nimeshatoka hospital lakini sasa hivi ni njaa kwenda mbele. Nimeanza second trimester sasa lakini bado tu naishiwa nguvu, sijui hata nifanyeje?
Mimba kumbe ni shughuli jamani...........watu tumetolewa mbali kumbe.Na hivi nimenasa huku nipo masomoni mhhhhhhh!!

Hivi pilipili ni salama kwa kwa mwanamke mjamzito? Kuna wadada hapa ambao labda kipindi cha ujauzito mlikula pilipili vipi hazikuwadhuru? Mie mwenzenu mpenzi sana wa pili pili na katika hali hii bado nakula, nakatazwa kula lakini wala siachi.Je pili pili ina madhara yoyote kwa unborn child?
 
Hongera sana dadangu,
ndio kwa mara ya kwanza kuona mtu hapa JF akijielezea yeye mwenyewe na wala sio MDOGOANGU, DADANGU, RAFIKIANGU
 
Pretty! Wanawake wengi sana huheshimu mama zao zaidi pale wapitiapo haya! Sasa mrembo acha huo wasiwasi wa kunenepa...kwa sasa kula na hasa vyakula vinavyojenga huo mwili, mboga za majani kwa wingi na matunda. By the way nashangaa bado una wasiwasi wa kunenepa huku unasema chakula hakiliki! Unahitaji vyakula vinavyojenga mwili na hasa vile vinavyohakikisha damu ipo ya kutosha. Kumbuka wakati huu ni hatari sana kwako kupata malaria kwani mwili ni dhaifu. Ikikupitia moja ya nguvu hali itakuwa ni mashaka zaidi.

Hiyo njaa ya kila saa unaweza kuhakikisha unakuwa na matunda jirani ya kuituliza. Usiendekeze chips mayai, urojo, ice cream, mishikaki na yanayofanana na hayo. Hivi ndio vitauvuruga mwili by the time unajifungua umevimba kila upande. Kula proper meals kwa wakati na njaa za katikati kula healthy snacks.

Pilipili inaweza kukusababishia kiungulia (heartbun), Ningekuwa wewe ningejitahidi kuiepuka lakini kama haikusumbui na inakusaidia kula basi iwe ya kiasi.
 
Pole mama mtarajiwa. Haidhuru ndio kibin'adamu tangia Hawa alipokula tunda alilokwatazwa shurba shurti zitupate.
 
Pole na hongera, nadhani haya matatizo huwa ya kawaida hasa kama mimba ni ya kwanza, vumilia dada miezi tisa si mingi sana! Jipe moyo utashinda!
 
usione tabu kunenepa ukamdhulumu mtoto ...........kula mpenzi, ukishajifungua utafanya mazowezi kupunguza unene kama utanenepa.

pilipili ni chanzo kizuri sana cha vitamin c ila sijui kama ina matatizo kwa ujauzito au la......lkn sidhani. tusubiri madaktari waje watoe maelezo
 
Vumila Pretty mimba sio ugonjwa itapita na shukurur Mungu sana amekujalia baraka ya pekee kuna watu wanasafiri dunia yote kutafuta hio hali yako. Bora wewe unakula pilipili rafiki yangu alioa mke wa miraba minne na yeye alikuwa mwembamba sana alipopata ujauzito alikuwa anampiga kila arudipo kutoka kazini anamvizia anampiga na chuma kichwani mpaka akalazwa hospital siku 1 kwa kushonwa nyuzi 8 kisogoni. alivyozaa tu wa kwanza kumuulizia ni mume wake ilihali alikuwa ataki hata kumwona na mpaka huyo rafiki angu atamani tena mtoto wa 2.
 
Hongera sana Mama Mtarajiwa... Pole na ikiwezekana kula kila kinachoweza kuingia mdomoni. Kunenepa sio shida wakati wa ujauzito. Ni bora kunenea kuliko kukonda Mama.
 
Vumila Pretty mimba sio ugonjwa itapita na shukurur Mungu sana amekujalia baraka ya pekee kuna watu wanasafiri dunia yote kutafuta hio hali yako. Bora wewe unakula pilipili rafiki yangu alioa mke wa miraba minne na yeye alikuwa mwembamba sana alipopata ujauzito alikuwa anampiga kila arudipo kutoka kazini anamvizia anampiga na chuma kichwani mpaka akalazwa hospital siku 1 kwa kushonwa nyuzi 8 kisogoni. alivyozaa tu wa kwanza kumuulizia ni mume wake ilihali alikuwa ataki hata kumwona na mpaka huyo rafiki angu atamani tena mtoto wa 2.
Hahahahahahaa.Nguli acha vituko.Hii mimba gani ya kupiga mumewe? Labda alikuwa amempania.Na huyo mtoto vipi ,si atakuwa kama Evander H ?
 
Hii story ni ya kweli kabisa nitakukutanisha naye na alama atakuonyesha. Baada ya kujifungua tulimuuliza kwa nini alikuwa anampa kipigo mumewe akasema alikuwa anapata jazba na wivu mkali sana. Kila amuonapo mumewe anahisi katoka kwa mwanamke mwingine kama haitoshi alichukia sana harufu yake.
 
............Mwenzenu Mungu amenishushia baraka za ujauzito, lakini imenivunja nguvu sana. Yaani muda wote naishiwa nguvu na njaa kuuma kila wakati. Kila baada ya nusu saa nahisi njaa kali sana.........hata nikila vp lakini muda mfupi tu njaa.Huu ndio ujauzito wangu wa kwanza basi naogopa huko kula kula nisije kunenepa bure.
..........3 weeks ago nilikuwa hoi, chakula changu kilikuwa ni drip tu, maana nilikuwa nasikia njaa lakini chakula hakiliki hadi ikabidi niwe admitted hospital.Nashukuru nimeshatoka hospital lakini sasa hivi ni njaa kwenda mbele. Nimeanza second trimester sasa lakini bado tu naishiwa nguvu, sijui hata nifanyeje?
Mimba kumbe ni shughuli jamani...........watu tumetolewa mbali kumbe.Na hivi nimenasa huku nipo masomoni mhhhhhhh!!

Hivi pilipili ni salama kwa kwa mwanamke mjamzito? Kuna wadada hapa ambao labda kipindi cha ujauzito mlikula pilipili vipi hazikuwadhuru? Mie mwenzenu mpenzi sana wa pili pili na katika hali hii bado nakula, nakatazwa kula lakini wala siachi.Je pili pili ina madhara yoyote kwa unborn child?
soma hapo juu,nadhani hukusema post yake vizuri

Lakini hajasema kama huu ni ujauzito wa kwanza!
 
Hii story ni ya kweli kabisa nitakukutanisha naye na alama atakuonyesha. Baada ya kujifungua tulimuuliza kwa nini alikuwa anampa kipigo mumewe akasema alikuwa anapata jazba na wivu mkali sana. Kila amuonapo mumewe anahisi katoka kwa mwanamke mwingine kama haitoshi alichukia sana harufu yake.
Basi hiyo kweli balaa.Alikuwa anahitaji kanseling ya kisaikolojia
 
Mimi nilikuwa na kibarua cha kumchomea mama matesha mahindi.
Alikuwa ananunua mahindi anayaleta home, ananisubiri nimchomee. Nisipoyachoma mimi hali, na nyumbani palikuwa hapakaliki.
Mimba za kwanza noma asee.
 
Ha ha ha! Ina raha yake hiyo...Doh! na hapo wanaume adabu inakuwepo ya kutosha
 
Mimi nilikuwa na kibarua cha kumchomea mama matesha mahindi.
Alikuwa ananunua mahindi anayaleta home, ananisubiri nimchomee. Nisipoyachoma mimi hali, na nyumbani palikuwa hapakaliki.
Mimba za kwanza noma asee.

Leo unahengiova? umesahau kuwa mimi ndo mama matesha?
 
Back
Top Bottom