Ujauzito kwa miaka mitatu?

Preta

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
24,323
18,791
jamani hii hainiingii akilini.....kuna mwanamke mmoja anayeishi Arusha maeneo ya Maji ya Chai amekuwa akibeba mimba miaka mitatu badala ya miezi tisa,anasema alipopata mtoto wa 5 ndipo matatizo yalianza....baada ya kuzaa huyo mtoto mimba nyingine ilibaki ndani ya kizazi....ki ufupi alipata watoto 17 kwa mtindo huo, wanne walifariki wakabaki 13 na sasa ninapoandika hapa ana mimba nyingine ina miaka miwili na nusu....kilichoniacha hoi kabisa ni kuwa, anapata mimba hizo bila kukutana na mumewe....jamani jamani!!!!

Source : ITV
 
Niliisikia mara ya kwanza 2009 nilishangaa sana, akutanishwe na TB JOSHUA kila kitu kitabaki historia.
 
Ushasema ni matatizo,thus sio normal hata kidogo! Ni kiasi tu cha kumhurumia.

kuna madaktari bingwa wa wanawake wanaoheshimika a-town kama 3 hivi wamempitia wote kumcheck lakini wametoka kapa....hawaoni kitu mama yupo normal....kwa mujibu wa vipimo vyao
 
akafanyiwe opereshen!!!!!!

mi naona wangemnyofoa kizazi kabisa toka alipofikisha watoto 9....na ukiwaona hao watoto wake wote ni wanono.....na ni familia iliyo duni kidogo
 
nildhani labda ana utaalamu wa kufunga hiyo mimba isikuwe kama ndugu zangu wa Kagera,kumbe yeye ni matatizo maskini... Hizo mimba anapataje bila kukutana na mumewe au anakutana na mwanaume mwingine anaye julikana?
Mara nyingi huwa nasikia mimba za majini kama ya shekh hussein haizidi miezi mitatu unajifungua... Duh sasa hii vp.
Bibi kama unaamini kuwa kuna Mungu aliye muweza wa yote basi mtumaini yeye, naye atakusaidia.
Pole sana.
 
Preta hiyo ishu ipo juu ya uwezo wa binadamu hata ukitoa kizazi atapata mimba, ni ya kiroho maombi tu hapo.
 
Preta hiyo ishu ipo juu ya uwezo wa binadamu hata ukitoa kizazi atapata mimba, ni ya kiroho maombi tu hapo.

sasa wanachelewa nini si wachukue hatua hiyo haraka.......watoto kumi na saba bado upo tu unasubiri wa kumi na nane.........dah
 
Huyo mama alihojiwa siku moja, anasema kizazi walimtoa, ila sasa haieleweki inakuwaje!
 
huyu mama ana historia yake.....kizazi kilishatolewa mda...lakini mimba zinaingia...kuna siku walionyesha mpaka kwake na kwa kweli kuna timu imekamilika watoto ni wengi sana.......

wataalamu wafanye uchunguzii..maana watoto 17 sio mchezo eti
 
yale matukio ya mimba zile mfululizo yamemharibu kisaikolojia na ndo maana anaisi kama ana mimba lakini si kweli kwani madktari wamempima na kuona hana mimba yeyote ila yeye anaisi ana mimba....na kuhusu kuzaa na kuendelea kushika ujauzito hilo lilikuwa zamani na sasa halipo tena kilichobaki sasa ni hisia zake tu ndo zinamfanya awaze sana na c vinginevyo............
 
jamani hii hainiingii akilini.....kuna mwanamke mmoja anayeishi Arusha maeneo ya Maji ya Chai amekuwa akibeba mimba miaka mitatu badala ya miezi tisa,anasema alipopata mtoto wa 5 ndipo matatizo yalianza....baada ya kuzaa huyo mtoto mimba nyingine ilibaki ndani ya kizazi....ki ufupi alipata watoto 17 kwa mtindo huo, wanne walifariki wakabaki 13 na sasa ninapoandika hapa ana mimba nyingine ina miaka miwili na nusu....kilichoniacha hoi kabisa ni kuwa, anapata mimba hizo bila kukutana na mumewe....jamani jamani!!!!

Source : ITV
Ni maombi tu ndi suluhisho la tatizo lake, tatizo kama haamini katika maombi ndio shida!!!!!!!!!!!! hata hivyo wana JF tumuombee kila mtu kwa wakati wake Mungu atatusikia na kumhurumia yeye, Mungu atamsaidia tu
 
Back
Top Bottom