Ujasusi wa kiuchumi: Katika hili kenya imetupiga bao

The Genius

JF-Expert Member
May 29, 2018
820
2,070
Kenya imezindua bandari ya Lamu, kilometa 240 kaskazini mwa mji wa Mombasa. Ni bandari kubwa kuliko zote Afrika Mashariki inayotarajiwa kutoa ushindani mkubwa kwa bandari ya Dar Es Salaam na Durban.

Kijiografia, bandari ya Lamu inaweza kuhudumia nchi jirani za Kenya hasa Ethiopia na Sudan kusini. Lakini kimkakati inaweza kuhudumia Afrika na dunia nzima.

Inawezaje kuhudumia Afrika na dunia nzima?
Kwenye biashara ya usafiri wa majini kuna kitu kinaitwa 'Transhipement' - ambapo bandari kubwa zinapokea meli kubwa zinazobeba bidhaa nyingi na kuzigawanya kwenye meli ndogondogo zinazopeleka bidhaa kwenye bandari zingine ambazo haziruhusu meli kubwa. Kwa mfano, baadhi ya meli kubwa haziwezi kutia nanga bandari ya Dar es Salaam kwahiyo zitatia nanga bandari ya Lamu, halafu meli zingine ndogo zitapokea mzigo huko Lamu na kuzipeleka bandari za Dar es Salaam, Mombasa, Tanga nk.

Pia, meli ndogondogo zinaweza kukusanya bidhaa kutoka maeneo mengine na kuzipeleka kwenye bandari ya Lamu kisha kuzipakia kwenye meli kubwa zinazosafiri huko duniani. Hiyo ndio namna ya bandari ya Lamu itakavyohudumia dunia.

Ni ipi nafasi ya Tanzania katika hili?

Linapokuja suala la biashara kupitia usafiri wa majini Tanzania ina bahati kubwa kijiografia, pengine kuliko nchi zote za Afrika ukiondoa Misri. Tanzania ni lango la asili la Afrika kutokea nchi za Asia, hasa China na India ambazo zinafanya vizuri kwenye soko la dunia kwa sasa. Pia, China na India pekee ni nchi mbili zenye idadi ya watu karibu theluthi ya dunia nzima. Ukipata soko la kuuza chakula na malighafi za viwanda kwa nchi za China na India, unatajirika. Lakini bado hatujachangamkia soko hili. Faida nyingine ya kijiografia ya Tanzania ni namna ilivyopakana na mataifa mengi yanayounda jumuia ya Afrika Mashariki (EAC); Uganda, Rwanda na Burundi na yale yanayounda jumuia ya SADC, Zambia na Malawi ambayo yanategemea bandari ya Dar es Salaam. Zaidi ya hizo nchi za SADC na EAC kuna DRC ambayo inazalisha malighafi nyingi kwa ajili ya viwanda vya nje ya Afrika. Kuna nchi za Angola na Congo - Brazaville, ambazo pamoja na kuwa na bahari ya Atlantiki bado ni rahisi kwao kufanya biashara na mataifa ya Asia kupitia Tanzania.

Kwa faida hizi za upendeleo, bandari ya Dar es Salaam haipaswi kuwa kituo cha kukusanya bidhaa kupeleka Lamu. Tunahitaji bandari kubwa.

Taarifa zinaonesha bandari ya Dar es Salaam inazidiwa uwezo, na eneo lilopo halitoshi kwa upanuzi zaidi. Kunahitajika bandari kubwa na ya kisasa kuliko ya Dar es Salaam kabla ya mwaka 2030.

Kulikuwa na mawazo ya bandari ya Afrika Mashariki ambayo ingejengwa Mwambani bay, Tanga. Ukaja mpango wa bandari ya Bagamoyo, lakini hakuna kilichofanyika. Sasa Kenya wamezindua bandari kubwa Afrika Mashariki, sisi bado tuendelee kujibizana?

Serikali iangalie namna ya kutekeleza mipango ya ujenzi wa bandari, ile ya Mwambani Tanga au Bagamoyo, alimradi maslahi ya nchi yazingatiwe.

Nawasilisha.
FB_IMG_1622124765068.jpg
 
ukweli mchungu; economically kenya wameshatuacha kipande kirefu sana.

watanzania tusikasirike ndo hivyo tena
 
Kenya wana bandari ngapi, na wanatazamia kuhudumia nchi ngapi??

Sisi tuna bandari ngapi, na tunatakiwa kuhudumia nchi ngapi???

Tabia za kuchunguza jirani kafanya nini huko kwenye majumba yetu, ndio zimetufikisha hapa. Mtu anakula nyama macho yanakutoka kisa weww unakula mchicha, wakati kimahesabu ya kiafya umemwacha mbali.
 
Wasiwasi wako tu, Tanzania tutamove kivyetuvyetu sio kuangalizia alichofanya jirani, tunafanya tunachokiweza sio tunachokiona na kukisikia
 
credit Cyrilo
Hivi unapata hasara gani ukitoa credit kwa mwandishi halisi wa makala..

otherwise wewe mwenyewe uwe ndio Christopher Cyrilo hapo umetumia ID nyingine
 
Kenya imezindua bandari ya Lamu, kilometa 240 kaskazini mwa mji wa Mombasa. Ni bandari kubwa kuliko zote Afrika Mashariki inayotarajiwa kutoa ushindani mkubwa kwa bandari ya Dar Es Salaam na Durban.

Kijiografia, bandari ya Lamu inaweza kuhudumia nchi jirani za Kenya hasa Ethiopia na Sudan kusini. Lakini kimkakati inaweza kuhudumia Afrika na dunia nzima.

Inawezaje kuhudumia Afrika na dunia nzima?
Kwenye biashara ya usafiri wa majini kuna kitu kinaitwa 'Transhipement' - ambapo bandari kubwa zinapokea meli kubwa zinazobeba bidhaa nyingi na kuzigawanya kwenye meli ndogondogo zinazopeleka bidhaa kwenye bandari zingine ambazo haziruhusu meli kubwa. Kwa mfano, baadhi ya meli kubwa haziwezi kutia nanga bandari ya Dar es Salaam kwahiyo zitatia nanga bandari ya Lamu, halafu meli zingine ndogo zitapokea mzigo huko Lamu na kuzipeleka bandari za Dar es Salaam, Mombasa, Tanga nk.

Pia, meli ndogondogo zinaweza kukusanya bidhaa kutoka maeneo mengine na kuzipeleka kwenye bandari ya Lamu kisha kuzipakia kwenye meli kubwa zinazosafiri huko duniani. Hiyo ndio namna ya bandari ya Lamu itakavyohudumia dunia.

Ni ipi nafasi ya Tanzania katika hili?

Linapokuja suala la biashara kupitia usafiri wa majini Tanzania ina bahati kubwa kijiografia, pengine kuliko nchi zote za Afrika ukiondoa Misri. Tanzania ni lango la asili la Afrika kutokea nchi za Asia, hasa China na India ambazo zinafanya vizuri kwenye soko la dunia kwa sasa. Pia, China na India pekee ni nchi mbili zenye idadi ya watu karibu theluthi ya dunia nzima. Ukipata soko la kuuza chakula na malighafi za viwanda kwa nchi za China na India, unatajirika. Lakini bado hatujachangamkia soko hili. Faida nyingine ya kijiografia ya Tanzania ni namna ilivyopakana na mataifa mengi yanayounda jumuia ya Afrika Mashariki (EAC); Uganda, Rwanda na Burundi na yale yanayounda jumuia ya SADC, Zambia na Malawi ambayo yanategemea bandari ya Dar es Salaam. Zaidi ya hizo nchi za SADC na EAC kuna DRC ambayo inazalisha malighafi nyingi kwa ajili ya viwanda vya nje ya Afrika. Kuna nchi za Angola na Congo - Brazaville, ambazo pamoja na kuwa na bahari ya Atlantiki bado ni rahisi kwao kufanya biashara na mataifa ya Asia kupitia Tanzania.

Kwa faida hizi za upendeleo, bandari ya Dar es Salaam haipaswi kuwa kituo cha kukusanya bidhaa kupeleka Lamu. Tunahitaji bandari kubwa.

Taarifa zinaonesha bandari ya Dar es Salaam inazidiwa uwezo, na eneo lilopo halitoshi kwa upanuzi zaidi. Kunahitajika bandari kubwa na ya kisasa kuliko ya Dar es Salaam kabla ya mwaka 2030.

Kulikuwa na mawazo ya bandari ya Afrika Mashariki ambayo ingejengwa Mwambani bay, Tanga. Ukaja mpango wa bandari ya Bagamoyo, lakini hakuna kilichofanyika. Sasa Kenya wamezindua bandari kubwa Afrika Mashariki, sisi bado tuendelee kujibizana?

Serikali iangalie namna ya kutekeleza mipango ya ujenzi wa bandari, ile ya Mwambani Tanga au Bagamoyo, alimradi maslahi ya nchi yazingatiwe.

Nawasilisha.View attachment 1799513
Bandari ya Dar haifanyi kazi katika ufanisi wake inavyotakiwa, kuna upigaji sana
Kabla ya kufikiria kuipanua sijui kuifanyaje, uthibiti uwepo
Tatizo wasimamizi ndo wapigaji wenyewe.
Tulikuwa na jirani miaka ya 90 mwishoni alikuwa anafanyakazi bandarini alikuwa aktanba kuwa kila siku anarudi na mzigo wa maana, kati ya tshs 3m na tshs5m
 
Back
Top Bottom