Ujasusi - Umoja namba 97

SEHEMU YA 67
SUZZANE IN TRAP (SUZZANE MTEGONI )
Patrick siku hio hakuweza kabisa kwenda hata kazini , moyo wake ulikuwa na majeraha makubwa sana , kitendo cha uhusiano wake kuvunjika kisa mwanamme kwake ni jambo gumu sana kulivumilia , hakuwahi kuwazia siku moja anaweza kukataliwa na mwanamke , katika maisha yake yote hakuwahi kukataliwa na mwanamke , kila mwanamke aliekuwa akimtongoza hakupata shida kubwa , lakini mwanamke Merina ndio mwanamke wa kwanza kumkatalia , lakini pia ni mwanamke wa kwanza kwake kumpenda kwa moyo wake wote , mara baada ya kupewa taarifa za uhakika na Mage kwamba Damiani amerudi kwake lilikuwa ni pigo kubwa dalili za kumpoteza Merina zilikuwa wazi kabisa , na jambo hilo kwake lilikuwa ni gumu sana kulikubali , hakujua afanye nini kwa wakati huo , siku hio aliamua kujifungia zake ndani akinywa pombe pasipo kufanya maamuzi yoyote , hata pale baba yake alipomuhitaji kufika ikulu kwa ajili ya kumpa maelekezo ya kazi alitoa sababu ambazo zilimshangaza baba yake kabisa .
Siku hio mara baada ya kukaa ndani siku nzima , ndipo alipoamua kutoka muda wa jioni kwa ajili ya kuonana na rafiki yake Ahmedi ili ampe ushauri ni jambo gani alifanye ili kumpata mwanamke Merina , kwani mpaka wakati huo hakuwa tayari kabisa kumpoteza , alikuwa yupo tayari kulipigania penzi la Merina kwa namna yoyote ile , mahali walipo panga siku hio kuoana ilikuwa ni maeneo ya Sinza la chaz.
Muda wa saa moja juu ya alama Patrick alikuwa maeneo hayo akiwa na gari yake kali , huku akiwa amevalia kinadhifu kabisa , jambo ambalo liliwafanya warembo waliokuwa eneo hilo wamtamani mwanaume huyu , kwani wengi walikuwa wakimjua sana kwani kabla ya Patrick kukutana na Merina , maeneo hayo ya La chaz ndio zilikuwa pande zake za kula bata akiwa na marafiki zake , lakini ni muda mrefu kidogo hakuwahi kufika eneo hilo na yote hayo ni kwasababu ya mapenzi yake juu ya Merina.
Ahmedi alikuwa tayari yupo eneo hilo akiwa amezungukwa na warembo wakila bata , kama kawaida ya msomali huyu kupenda bata , mara baada ya kumuona rafiki yake kufika alimpungia mkono huku akimkaribisha kwa bashasha sana .
“ Karibu sana mzee wa bata , maeneo haya yamekumisi sana , angalia warembo wanavyokuangalia , ni muda sana hujafika maeneo haya” Aliongea Ahmedi huku akimwangalia Patrick kwa tabasamu .
Patrick naye hakuongea lolote aliketi huku akitabasamu , alionekana kuwa serious mno , baada ya madakika kadhaa muhudumu alifika na Patrick aliagiza ‘whiskey’ aina ya Jackdaniel .
“ Ewaaa! mambo ndio hayo sasa “ aliongea Ahmedi na kuwafanya warembo waliokuwa wamekaa karibu yake watabasamu .. lakini wakati wanaendelea aliingia mtu mwingine ambae Patrick alifurahi sana kumuona , huyu hakuwa mwingine alikuwa ni Sabi , mkurugenzi wa ikulu mawasiliano , na alikuwa maeneo hayo pia kwa ajili ya kuonana na marafiki zake hao .
“Sabi karibu sana rafiki yangu , kumbe na wewe ni mzee wa haya maeneo ?” aliongea Patrick huku akimsabahi Sabi .
“Hahaha .. pat ndio mimi ni mwenyeji sana , siku moja moja nakuja haya maeneo kupunguza stress za kazi na mengineyo , leo nakuona umejumuika hapa maana nasikia ulikamaatika na mapenzi mpaka maeneno haya huonekani ..”
“Point hio “ alikazia Ahmedi ambae muda huo pombe zilikuwa zishaanza kumuingia akilini kisawa sawa , na jambo hilo lilimkera kidogo Patrick kwani alitumaini kwamba atapata wasaa mzuri wakuongea nae ili ampe ushauri akiwa hajaelewa lakini ni tofauti na alivyokuwa ametegemea kwani mtu huyo alikuwa chakali pombe zimemkaa kichwani , lakini jambo la kushukuru ni kwamba Sabi alifika eneo hilo , ni kweli alikuwa amemsahau sana rafiki yake huyo kwa kitambo , lakini mara baada ya kumuona alikumbuka busara alizokuwa nazo Sabi tokea wakiwa wote masomoni na aliona litakuwa jambo jema sana kama atayaweka wazi yanayomsibu kwa marafiki zake hao .
“Ahmedi kabla sijaanza kupiga mtungi nadhani unakumbuka jambo tuliloongea mchana nililotaka kuongea na wewe , lakini imekuwa vyema sana na Sabi yupo hapa , so kabla sijaanza kulewa nataka tuongee kwanza .. hawa warembo unaonaje tukiwarudia baada ya maongezi yetu “
Aliongea Patrick na wakati huo mhudumu alimletea sabi na yeye heinken na Ahmedi aliwapa ishara wale warembo kwamba waondoke mpaka atakapo waita tena huku akiwataka waagize chochote wanachotaka atalipa .
“Enhe certified lover boy hebu tueleze” Aliongea Ahmedi kiutani lakini ni utani uliomuingia Patrick , lakini alijikaza Zaidi kwani alishajua akili za Ahmedi wakati huo ni nusu kwa nusu .
“ Merina rafiki yangu , ananitesa sana yule mwanamke”
“Mmhmh .. ! aisee na wewe pat siku hizi unateswa na mapenzi “ aliongea Sabi kwa mshangao kwani alikuwa akimjua sana rafiki yake huyo kwa muda mrefu alikuwa ni mpigaji .. na alikuwa akikumbuka kauli zake kwamba mapenzi hayatakuja kumtesa , lakini sasa kusikia jamaa analalamika mwanamke anamtesa kwanza alishangaa sana lakini pia alijiuliza ni mwanamke gani huyo mwenye uwezo wa kumtesa Patrick , kwani pesa anazo , mvuto anao , lakini pia kazi anaiweza kwake lilimshangaza .
“Sabi nakwambia kijana wangu kakamatika , na haina budi tumsaidie kijana wetu mapenzi yanamuua huyu … kwa muonekano wake anaonekana amepigwa na kitu cha tani kichwani hana uelekeo” Aliongea Ahmedi .
“ Hebu tueleze mzee .. hatutakosa cha kukusaidia” Aliongea Sabi na Patrick alivuta pumzi na kuweka wazi yale yanayomsumbua mwanzo mwisho .. kwa ufupi baada ya Patrick kumtaja mrembo Merina swala hilo lilijibu baadhi ya maswali yake Sabi , lakini swala la pili ni jina la Damiani , alijiuliza ni Damiani anayemjua au ni Damiani mwingine .
Lakini kadri alivyoisikiliza stori hio fupi ya mapenzi yakusisimua alikuja kupata jibu kamili kwamba mtu ambae anazungumziwa hapo ni Damiani yule anaemjua … ambae ameambiwa siku ya jana yake kwamba ashaingia nchini .
“Daah! … kwanza pole sana rafiki yangu Patrick ni Dhahiri kabisa unampenda sana huyu mwanamke .. lakini pia niseme wazi kabisa nidhahiri huyu mwanamke kapenda sehemu nyingine .. swali hapa linabaki upande wa huyo mtu mwingine yaani Damiani ..je anampenda Merina … lakini kabla sijakushauri Zaidi nadhani , mpaka sasa unajibi lako mwenyewe kichwani na unahitaji validation kutoka kwetu “ Aliongea Sabi .
“ Ni kweli kabisa nina maamuzi ambayo mpaka sasa nimeamua …. Unajua nimepigania penzi la Merina tokea muda mrefu sana na niseme kabisa mimi ndio mtu ninaestahili kabisa kuwa na Merina , kwasababu kwanza nampenda lakini pili naamini huyo Damiani hampendi Merina kama ninavyo mpenda mimi hivyo maamuzi yangu ni kwamba sitokaa nione Damiani anakuwa na mapenzi na Merina kwa vyovyote vile “
“ Lakini bwana Ahmedi … unajua kwamba unayoongea hapo ni maswala ambayo yako nje ya uwezo wako .. na maanisha swala la Merina kukupenda ,, ni swala ambalo huna jinsi nidhahiri kwamba sio mtu sahahi kwako … kwani kama ni mtu sahihi kwako hisia zako na zake zingeendana .. kwa hio unachofanya ni kujitafutia matatizo Zaidi kwasababu yeye hakupendi na ukimlazimisha utaishia kuumia …”
“ Ewaaa ..umeingea point Sabi ..mimi huyu mwana nilikuwa namwambia kila siku jambo hilo hilo kwamba acha kulilia penzi penzi ambalo hulistahili “
“Utasemaje si listahili .. unamaanisha nini … nimefanya mambo mengi kwa ajilli ya Merina ,,, inakuwaje sistahili penzi lake”
“Alicho ongea Ahmedi ni kitu sahihi kabisa … Merina hakupendi kwasababu sio mtu sahihi kwako”
“Sabi na Ahmedi .. nimeishi kwa kujifunza vitu vingi sana kutoka kwa wanawake ,, they are just obsessed over someone … and they come to realize who they real want when it`s too late ,, and that I won`t allow it .. I love her because she is right woman for me if she is not the one I couldn’t love her at first sight and this far…(nawajua sana wanawake wanakuwa wanamtaka sana mtu bila kujua kile wanachokitaka ..na wanakuja kujua mtu sahihi wanaemtaka pale ikiwa muda ushakwisha na hilo ni jambo ambalo siwezi kuliruhusu )
“So what are you going to do .. she doesn’t love you ? (kwa hio unaenda kufanya nini .. hakupendi lakini )
“There is only one way .. It`s damian disappearance .. once he is gone .. I can make Merina fall for me .. am very sure with my judgement ..i will fight for what I want ( kuna njia moja tu na njia hio ni kumpoteza Damiani ,, akisha potea nitaweza kumfanya Merina anipende .. niko sahihi na maamuzi yangu .. ninakwenda kupambania kile ninachokipenda ).
“ You are feisty Pat .. but what is so special about this woman anyway ( unaonekana umeamua Patrick .. ni jambo gani spesho nalo huyo mwanamke )
“ I just don’t know Sabi .., yeah she is so beautiful and successful but for me the urge to have this woman for my life is something that I cant control over . (mimi sijui chochote sabi ,, ndio ni mzuri mrembo ana mafanikio lakini ilehali ya kumuhitaji kwa maisha yangu huyu mwanamke ni kitu ambacho kukikontrol nashindwa ).
“Pat wewe ni rafiki yangu sana .. and we have come this far because we have so many in commn .., right now I can`t just ignore what you feel .. and after all what you said is true we real don’t know about woman .. and in short we cant understand them .. who knows may be it is true that merina is just obsessed to be with Damiani… you have all the right to fight for her .. fight for what you love bro “ (Pat wewe ni rafiki yangu sana na tumefika tulipo sasa kwasababu tuna mengi yanayofanana na sasa hivi siwezi kuzidharau hisia zako .. na hata hivyo ulio yasema ni sahihi hatujui chochote kuhusu wanawake … kiufupi hawaeleweki .. unajuaje labda ni kweli merina anamtaka tu Damiani lakini sio mtu sahihi kwake kwa hio pigania kile unachokipenda ) aliongea Ahmedi ,, jambo ambalo kwa Patrick hakuletegemea kabisa ,, alijikuta akitabasamu mno .
Upande wa Sabi yeye hakuongea chochote .. aliona Patrick ni kweli amedhamiria .. lakini pia swala hili aliona ni swala la kufanyia kazi , aliona kuna ulazima wa kuongea na Damiani ili ajue na yeye upande wake kama anampenda Merina , kwani aliona kama Patrick ataweka nguvu kumpoteza Damiani kazi yao kubwa ilioko mbele yao ya kulikomboa taifa ingekuwa ngumu zaidi .. hivyo swala la kwanza aliona ni kumtafuta Damiani wakutane waongeee .
******
Masaa ,machache nyumba baada ya Suzzane kutoka nyumbani kwa Merina moja kwa moja aliekea kwenye kampuni ya Zakayo iliokuwa maeneo ya Mlimani city ndani ya jengo la PSSF , baada ya kufika eneo hili moja kwa moja alipaki gari yake na kwenda mpaka floor husika na baada ya kuingia hapo alinyoosha mpaka kwenye ofisi ya Zakayo , lakini kabla ya hapo alizuiwa na secretary wa Zakayo na hapo ndipo alipo omba kuonana na Zakayo lakini jibu alilopata ni kwamba Zakayo alikuwa ametoka , ila atarudi muda sio mrefu .
Kwakuwa jambo lililomleta mahali hapo ilikuwa na ulazima kwake , aliona nivyema akimsubiri , kwani kwenye kichwa chake alikuwa akijua fika kabisa kwamba Zakayo alikuwa akijua mahali ambapo Damiani yupo.
Na ni kweli ndani ya lisaa limoja Zakayo aliingia ndani ya eneo hilo na alipo muona Suzzane alijikuta akitabasamu na kisha alimpita na kunyoosha kwenye ofisi yake , lakini ile anaketi kwenye kiti chake na Suzzane na yeye aliingia hapo ndani akiwa na sura ya kikazi .
“ Karibu sana mrembo “ Aliongea Zakayo huku akiwa hana wasi wasi kabisa , akiwa ameweka tabasamu lake ka siku zote tabasamu ambalo mara nyingi lilikuwa ni kama siraha kwake katika biashara lakini katika mambo yake ya ujana hasa pale anapotaka kumnasa mwanamke yoyote yule .
“ Asante sana agent”
“ Niambie Suzzane nadhani kuna jambo muhimu lililokuleta hapa maana sio kawaida yako kuonekana maeneno haya , kwa kazi yako ilivyokuwa na majukumu mengi “
“Moja ya hayo majukumu ni hili lililonileta hapa Zakayo , naamini uwepo wangu mpaka sasa unajua ni kipi nimekijia , nataka kujua Damiani mahali alipo kwa sasa “ Aliongea Suzzane na kumfanya zakayo akae vizuri kwenye kiti huku akimwangalia usoni ..
“ Mimi nitajuaje Damiani alipo kama ninyi wanausalama mliokuwa mkifatiliakwa miaka mingi hamjui ?”
“ Come on Zakayo sina muda wa kupoteza .. nahtaji kujua Damiani alipo , na swala hili sio la kwangu binafsi ni swala linalojumuisha usalama wa taifa , kwa hio mimi kujua Damiani alipo ni muhimu sana , naomba tusiongee sana Zakayo , wewe ni mwanausalama nafikiri unajua ninachozungumza “
“Unauhakika gani kama najua mahali Damiani alipo “
“Zakayo najua yote unayoyafanya , mimi na wewe tunafanana kwenye jambo moja ,, wote ni wanausalama wenye mafunzo ya hali ya juu , lakini tofauti yako na yangu ni kwamba mimi nalifanyia kazi taifa , wewe unawafanyia kazi watu binafsi kwa ajili ya kujipatia fedha “
“ Hahahaha….. Suzzane hivi unajisikia unacho ongea kweli … good for you . ehe na vipi kuhusu kifo cha Danny yote hayo ni maswala ya kitaifa ?”
“Zakayo naomba tusifike mbali Zaidi , naomba uniambie ni wapi ninampata Damiani , najua umepewa kazi na Kimbona ya kumkamata Damiani lakini naomba nikwambie kitu .. mambo unayoyafanya Zakayo yanahatarisha usalama wa taifa lakini pia na usalama wa Damiani ,,, Damiani ni mtanzania na moja ya jukumu letu sisi kama watanzania ni kuhakikisha kwamba watanzania wanakuwa salama”
“ Okeya let say najua damiani alipo .. je nina sababu gani ya kukuambia wewe .. wewe ni mwana usalama tena ndani ya TISS una resources nyingi za kumfatilia mtu ,, kwanini ushndwe kujua alipo”
Wakati Zakayo akiongea simu ya Suzzane ilitoa mliio kuashiria kuna ujumbe mfupi ulioingia kwenye simu yake .. aliuangalia na kisha alitabasamu .
“ Kama hujui Zakayo damiani alipo naomba nikuulize swali … jana Damiani alipanda gari ya Merna ,, lakini asubuhi hii alieleta gari la Merina nyumbani kwake ni mfanya kaz wako . tena kwa maelezo yake kasema ndio umemuagiza .. unalijibu vipi hilo “
Zakayo alitabasamu kisha aliamka kwenye kiti alichokikalia nan a kuangalia nje .. n kama mtu ambae alikuwa anawaza jambo .
“Damiani tayari yupo kwenye mikono ya kimbona .. nishamkabdhi jana kwani ndio kazi Kimbona alionipa ,, nadhani jambo hili hata mheshimiwa atalifurahia kwani Kimbona na mheshimiwa ni washirika “
Aliongea Zakayo na kumfanya Suzzane amwangalie zakayo kwa macho ya mshangao .
“Lakini naweza nikakusadia kitu Suzzane ..vijana wa Kimbona muda wa saa nne wataenda kumchukua Damiani eneo nililomhifadhi .. , huo ndio msaada wangu kwako “ Aliongea Zakayo na kumfanya Suzzane apumue kama mtu alie na afadhali .
“Nashukuru kwa taarifa hio “.
“ Huna haja ya kunishukuru Suzzane … kama ulivyosema unafanyia kazi taifa na mimi nimekupa msaada kama mwanausalama mwenzio..” Aliongea zakayo na kutabasamu kinafiki na Suzzane na yeye alitambua kabisa kwamba zakayo hapo anamfanyia unafikia ,, na ndio maana na yeye alitabasamu kinafiki na kisha akatoka .
Wakati suzzane anatoka alitoa simu yake na kuwapigia vjana wake aliokuwa anafanya nao kazi , aliwapa maelekezo ya kuwafatilia vijana wa kimbona kila hatua wanayofanya .. huku Suzzane kichwani kwake akiwaza muda watakao enda kumchukua Damiani awafanyie shambulio la kushitukiza na kisha amchukue Damiani .
Zakayo yeye baada ya Suzzane kutoka ,, alijikuta akitabasamu .
“Mpango wangu unaenda kama nilivyopanga .. usiku huu nitapata majibu ya maswali yangu yote” Aliongea na kisha aliketi kwenye kiti chake .
ITAENDELEA
TUTAENDELEA WAKUU KESHO PANAPOMAJALIWA NITAJITAHIDI KUWEKA VIPANDE MPAKA VITATU , SIMULIZI HII NATAKA MPAKA KUFIKIA TAREHE 30 MWEZI HUU NISHAIFIKISHA TAMATI NITAMBULISHE KIGONGO KIPYA ZAIDI YA HII .
SIMULIZI ZANGU ZINAENDELEA KWA MPANGILIO HUU .
-MY DREAM MY FAVOURITE (The hollic shadow in missions)-Available complete

-UMOJA NAMBA TISINI NA SABA (Waraka wa raisi kabla ya kifo)- available complete
-2HOURS OF MEMORIES (Rise of darkness)-Realizing tarh30january

-UMOJA NAMBA TISINI NA SABA (Book of all names:U-97 the origin )- Ongoing

-UMOJA NAMBA TISINI NA SABA (Dreams of codes:2hours after effect)-Ongoing

Kwa taarifa tu hivi vitabu vitakuacha mdomo wazi kila mwisho wake bei yake 8000 except simulizi hii inayoendelea inapatikana mpaka mwisho kwa 3000 tu kwa anayetaka kusoma yote haraka haraka mpaka mwisho.
Tuma ujumbe watsapp no:0687151346 unajibiwa instantly.
 
Mkuu vipande vya Leo kama ulivyoahidi episode ya 68 &69 inatujia saa ngapi?
 
SEHEMU YA 68

TUVUMILIANE WAKUU NIMEEHINDWA KUEDIT MAJINA NA MWANZO WA SENTENSI KWA HERUFI KUBWA OTHERWISE STORI IPO CLEAN
LOSERS(WAPOTEZAJ )
SIKU MOJA NYUMA
Hii ni siku ambayo Damiani alitoka kwa Merina baada ya kumwomba gari .. aliendesha gari lake kwa umakini mkubwa huku akiangalia kama kuna mtu yoyote aliekuwa akimfatilia nyuma .. lakini kadri alivyokuwa akisonga mbele hakuona hatari yoyote ile ya kufatiliwa .
Dakika kumi na tano mbele alikuwa akipita maeneo ya Lugalo akielekea nyumbani kwake ,, alitembea kilomita kadhaa na kisha alikunja kushoto upande wa Mbezi beach high school akidhamiria kuelekea kwake , baada ya kama dakika kumi na tano alikuwa anakaribia geti la nyumba yake lakini mbele ya geti lake kuna gari ilikuwa imepaki maneo hayo , ilikuwa ni gari aina ya hilux nyeupe na mtu mwenye gari hilo alikuwa mbele ya gari lake akimpungia mkono , Damiani hakusita kusimamisha gari na baada ya kusimama yule mtu alimsogelea upande wa derava , na kwakua Damiani alidhania ni mtu wa kawaida bwana yule ,hakuwa makini kwani ile anashusha kioo alipigwa pigo la kushitukiza na pale pale akazima … aliefanya hivi hakuwa mwingine bali alikuwa ni Zakayo special agent huyu .. baada ya kufanya tukio lile , pale pale alimshusha na kumuingiza kwenye gari yake alirudi kwenye gari ile ya Merina alichomoa ufunguo na kisha akaifunga na kuiendela gari yake kisha akaondoka
Ndani ya masaa matatu tu ,, Zakayo alionekana akirudi maeneo yale yale ya Damiani anapoishi au Stephano lamberk na kisha aliingia kwenye gari ile ya Merina na kisha aliiondosha maeneo yale .
******
Ilikuwa yapata saa tatu na nusu ,, ndio muda ambao vijana wa Kimbona walikuwa wakipita maeneo ya Kongowe wakielekea Kisemvule maeneo ambayo ndio waliekezwa na Zakayo kuwa ndio suehemu Damiani alipokuwa akipatikana ,aliwapa maelekezo wakifika barabarani kuna namba wapige na atatokea mzee mmoja ambae atawapeleka , moja kwa moja hadi kwenye nyumba ambayo ndio damiani atakuwepo , na kweli ndani ya dakika kumi na tano kilomita kadhaa baada ya kupita Vikindu walipiga namba ile na kweli walimuona mzee ambae alikuwa amesimama barabarani , walisimamisha gari na yule mzee aliwapa maeekezo eneo husika .. sehemu hio kulikuwa na baadhi ya viwanda ,, walichukua upande wa kulia wakiwa na yule mzee wakiwa wamempandisha garini, baada ya kunyoosha kama mita miatano kutoka barabarani mzee yule aliwapa ishara ya kwamba ndio wamefika ,, ilikuwa ni mbele ya jengo moja lililokuwa likionekana kama ghala flani hivi , mzee yule aliwapa ufunguo na kisha Derick aliwapa ishara vijana washuke wakafungue , ndani ya dakka kadhaa tu walikuwa ndani ya jengo hilo ambalo ndani yake lilikuwa na uchafu japo sio sana ,, ilionekana ni kama sehemu ya kutunzia Pumba , basi baada ya kuingia hapo ndani wakiongozwa na derick , walipita kushotoo kwa mbele kulikuwa na chumba kilichokuwa na vioo vikubwa kwa juu ,, waliingia humo ndani kukiwa na mwanga na kisha walifungua mlango wa chumba kimoja kilichokuwa ndani jengo hilo ambalo lilikuwa ndani hapo , hio sehemu ilionekana ni kama ofisi iliokuwa na chumba cha mapumziko , walipo fungua humo ndani ndipo walipo mkuta damani akiwa amefungwa vizuri kwenye kitanda .
Mtu wa kwanza kutabasamu alikuwa ni derick , maana hio ilikuwa ni mara ya pili kumuona damian , lakini awamu hii alikiri kwamba damiani wa miaka ile na wasasa walikuwa wamebadilika sana , damiani wasasa alikuwa amejengeka kmazoezi lakini alikuwa akionesha kujiamiani Zaidi .damiani kitendo cha kumuona derick ndani hapo alijikuta kumbukumbu ya mama yake ikirudi kwa kasi ya ajabu sana na hasira nazo hazikumuacha salama , alijikuta akifurukurta kwenye kitanda kile cha chuma , alichofungwa na mnyororo .
“ hahahahaha.. kijana naona sasa umebadilika , umeingia kwenye kumi na nane zangu kwa mara nyingina miaka ile ulipona chupuchupu lakini awamu hii tarajia kifo chako “ aliongea derick huku akimpiga piga damiani mashavuni .”
“ huna lolote la kunifanya wewe fala , na nakuambia nitakuja kukuua kikatili sana kulipiza kifo cha mama yangu “
“ hahaha.. naona siku hizi hata sauti imebadilika ,, imekuwa ya kiume “ aliongea na vijana wake nao walicheka .
Huku upande wa nje ambako derick aliwaacha vijana wawili walinde eneo hilo kuangalia usalama kulikuwa ni kizaa zaa , kwani mwanadada suzzane aliekuwa amevalia mask alifika eneo hilo , na ilionekana alikuwa akiwafatilia vyema vijana wa kimbona , kwani ile anafika tu aliwapiga mapigo ya kusitukiza na nikitendo cha sekunde moja tu kila mtu alikuwa chini.
Wakati hayo yanaendeea , upande wa mita kadhaaa juu kabisa upande wa kushoto wa barabara , alionekana zakayo akiwa amekaa akiangalia upande wa chini kabisa wa jengo ambalo vijana wa kimbona walikuwa wapo kwa ajili ya kumchukua damiani .
Hata alivyomuona mtu akiingia hapo na kuwapiga mapigoo ya kushtukiza vijana wawili wa kimbona ambao walikuwa wamekaa kizembe nje wakilinda eneo hilo zakayo aliishia kutabasamu , kulikua na giza lakini kupitia darubini yake ilikuwa ikiweza kuangalia mpaka kwenye kgiza alifanikiwa kuona kila kitu na kumfanya atabasamu .
“ bado timu moja kufika , leo nakwenda kushuhudia mtanange , wa hali ya juu” aliongea zakayo huku akijiweka sawa kabisa .
Suzzane baada ya kutoa kichapo kwa vijana hao wawili ,, aliingia ndani nya jengo hilo kwa tahadhari ya hali ya juu kabisa huku mkononi akiwa ameshikilia vyema bastora yake alioifunga kiwambo cha kuzuia risasi alitembea kiubavu ubavu pasipo kupiga kelele , kwa mbele yake aliwaona vijana wawili wa kimbona waliokuwa mbele ya mlango wakuingialia wakiwa wanavuta sigara na nidhahili kabisa walikuwa wakiwasubiria wenzao waliokuwa ndani , kwa mwendo kama wa paka anaenyemelea panya alipita kwa nyuma yao na kujibanza kwenye pembe na pasipo hata ya kupiga kelele aliwasogelea wakiwa hawaelewi kile kinachoendelea , na baada tu ya kuwafikia kwa sipidi ya ajabu mno aliwapiga mapigo matakatifu ya shingo na hapo hapo kila mmoja alailegelegea , lakini aliweza kumuwahi huyu wa kwanza kwani wa pili alitaua kama zigo na alijikuta akijigonga kwenye bati lililokuwa mbele yake .
“ hebu angalia hao wapuuzi huko nje “ aliongea derick , huku pia akimwamrisha kijana aliekuwa upande wake wa kulia amfungue damiani ili waondoke nae , lakini ile anamaliza kufungua derick alijikuta akiguswa na kitu cha baridi kichwani , na ubaya ni kwamba katika vijana wote wa kimbona derick peke yake ndie aliekuwa akimiliki bastola na meja , lakini meja kwa wakati huo alikuwa ngomeni .
“ toa siraha yako nipatie “ ilikuwa ni sauti ya kibabe , lakini sauti hio ilisikika vyema kaatika masikio ya damiani , na damiani kwa spidi alijjikuta akimkadhia macho suzzane na suzzane ni kama alikuwa ametambua damiani alicho kigundua kwani na yeye alimwangalia , baada ya derick kutoa bastola yake , suzzane alimpiga pigo la shingo na pale pale akanyongonyea na kudondoka chini , akamfata na yule aliekuwa akimfungua damiani na yeye hakumsubirisha kwani alimpiga pigo na kuzima .
“ suzzane !” aliongea damiani
Na suzzane alitoa maski aina ya kitambaa kilichokuwa kikimziba uso na hapo ndipo alipo onekana mbele ya macho ya damiani .
“ za masiku damiani “ aliongea suzzane huku akimwangalia damiani aliekuwa amefungwa mikononi na mnyororo .
“naona umekuja kuniua kama ulivyomsaliti mshirika wako na kumuua “
“ unazungumza kuhusu nini damiani ?”
“ unajua ninachokizungumza suzzane , ulimuuwa bro danny “.
“ kumbe unajua nilimuua bro danny ,, basi nadhani mpaka sasa unajua ni jinsi gani nipo siriasi na kazi yangu damiani , umenikimbia sana na nimekutafuta sana , lakini hatimae nimekupata , nadhani sitotumia nguvu Zaidi kupata kile ninacho hitaji kutoka kwako “
“ unahitaji nini kutoka kwangu “
“ unajua ninacho hitaji damiani , lakini utaniambia baada ya sisi kutoka hapa , naomba usilete usumbufu maana haitakuwa jambo jema juu yako “.
Damiani hakuwa na ujanja kwa wakati huo , alimjua vyema suzzane kama komandoo , hivyo aliona kama angeleta utani asingetoka salama , lakini pia japo alijua suzzane asingemuua kizembe kutoka na kwamba bado alikuwa akimuhitaji , lakini kutokana na kwamba alikuwa amefungwa mikononin na mnyororo aliona jaroibio la kutoka hapo kwenye miikono nya mwanadada huyo isingefanikiwa .
Damiani alitangulia mbele huku nyuma akiwa ni suzzane, baada ya kutoka , hawakujisumbua hata kufunga geti, suzzane almwamrisha damiani atembee kusonga mbele huku wakipita gari waliokuja nao vijana wa kimbona .
Hili eneo la kisemvule ni sehemu ambayo ilikuwa haijajengeka sana , na majengo yaliokuwepo maeneo haya mengi yalikuwa yameachana umbali mrefu kidogo , hata miundombinu ya haya maeneo haikuwa mizuri sana ukiiacha barabara , kwani kulikuwa na mpaka maeneo mengine ambayo hayakuwa na umeme kabisa , hivyo hata hili eneo ambalo wakina suzzane walikuwa wakipita hakukua na nyumba nyingi lakini njia pia ilikuwa imefunikwa na baadhi ya vichaka .
Mita kadhaa mbele kabla ya suzzane kufika upande wa barabarani , upande wa kushoto ndipo kulitokea jambo la kushitukiza ambalo hata suzzane mwenyewe hakulitegemea
“ yeess hapo sasa “ ilikuwa ni sauti ya zakayo upande wa juu , kwani alishuhudia timu ya watu wawili mmoja mwanaume na mmoja mdada .
Zakayo alimshuhudia yule bwana mmoja wa makano akirusha kitu kama chuma , na kwakuwa suzzane hakutegemea tukio hilo chuma kile kilimpigga kwenye mikono na siraha yake ilienda pembeni , tukiio lile lilimfanya damiani na yeye ashituke na hapo ndipo damiani alipo mshuhudia mtu ambae hakumtarajia eneo hilo .
“ Janeth “ alitamka damiani na pale pale janeth alimsogela damiani na kumpa tabasamu kisha akamfungulia mikono yake , huku upande mwingne mtu aliefika nae eneo hilo na kurusha chuma hakuwa mwingine bali alikuwa ni Abasi .
Ilikuwa ni kizaa zaa ndugu msomaji kwani baada ya damiani kufunguliwa hapo ngumi zilianza watu watatu kwa mtu mmoja .
Suzzane kushuhudia jinsi damiani anavyopiga alijua muda huo kwamha alikuwa akipambana na watu hatari , lakini pia suzzane aligundua kuwa watu anaopambana nao alikuwa ni watu aliokuwa akiwajua kwani haikuwa mara yake ya kwanza kupambana nao.
“ hapa ndipo niipokuwa nikipataka , mpango wangu wa kuwakutanisha wote umefanikiwa kwa asilimia mia moja “ aliongea zakayo huku akiangalia ngumi zinavyopigwa hapo .
“ suzzane alikuwa ni moto tena ule moto , kwani kila pigo alilokuwa akirushwa alikuwa akilipangua vyma sana , na mpaka wakati huo abasi alikuwa ashapokea mapigo mawili ambayo yalikuwa yamempunguza nguvu kabisa , na wakati huo mtu aliekuwa akionesha kuumudu mchezo huo wa kimapigano alikuwa ni damiani , suzzane aligundua kuwa damiani alikuwa amebadilika sana , hakuwa yule damiani mpuuzi mpuuzi na mwoga mwoga huyu alikuwa ni damiani mwingine na hata aina yake ya kimapigano aliona kabisa alikuwa akipambana na mzoefu , lakini japo damiani alikuwa akipigana vizuri yeye alikuwa komandoo , hakuona kama kuna namna yoyote ya watu hao kumchoropoka kwani yeye alikuwa na mbinu nyingi sana .
Lakini pia kwa wapinzani wake , walikuwa waijiua walikuwa wakipambana na mtu wa aina gani hivyo walikuwa na tahadhari za kutosha , kwani baada ya kama dakika tano za pangua , huku suzzane akionekana kumiliki mchezo huo ndio hapo hapo janeth alikuwa na bastora mikononi mwake na kumwamrisha suzzane atulie la sivyo atachanguliwa ubongo , na suzzane hakutaka kuleta ubishi , alinyoosha mikono juu kusalimu amri .
“ hahaha ..safii ,, suzzane leo umekamatika “ aiongea zakayo akionesha kutabasamu mno na tukio lile .
Baada ya suzzane kunyoosha mikono juu damiani alifata ule mnyororo aliokuwa amefungwa nao kisha alimfunga nao suzzane .
“tunaondoka nae au ?” aliongea janeth
“ hapana huyu tukiondoka nae ni hatari kwetu “ aliongea damiani na kisha alichukua bastora ya suzzane iliokuwa upande wa pili wa kichaka na baada ya kuichukua aliikoki kama mzoefu na kisha alimsogelea suzzane .
“ tunaweza kumuhoji, kwanini tusiondoke nae “ aliuliza Abasi na kumfanya damiani atabasamu .
“ unafikiri ataongea ,, ni kujisumbua tu .”
“ kwahio tunamuacha hapa “
“ ndio .. ila nataka nimpe zawadi yake ya kuniwinda na kunikosesha Amani “ aliongea damiani na kisha alimpiga suzzane risasi ya paja , jambo ambalo liliwatoa macho wakina janeth , suzzane aliekuwa amesimama alijikuta akitoa mguno wa maumivu na kisha alidondoka chini .
“ nitakutafuta suzzane sijamalizana na wewe “ aliongea damani na kisha waliondoka .
“ umekosea sana damiani kuniacha nikiwa hai ,, nakuapia hii siku utaikumbuka “ aliongea suzzane kwa hasira huku akijiburuza chini hapo kwa maumivu huku damu zikimtoka , na dakika kadhaa alisikia sauti ya gari ikitokomea kwenye masikio yake .
“ https://jamii.app/JFUserGuide!!!! “ alitoa tusi huku akijinyanyua kuelekea upande wa barabarani , , na bahati nzuri gari lake halikuwa mbali , aliingia kwenye gari na kisha kwa kutumia simu yake iphone yenye program ya SIRI.
“ hellow SIRI call Sabi “
Upande wa zakayo mara baada ya kuona jambo lake limeenda kama alivyotaka , alitoka mahali alipo kuwa amesimama na kisha aliingia kwenye gari lake na kuondoka ,akilifukuzia gari walilopanda damiani.
“ yule si janeth yule “ lilikuwa ni swali ambalo lilikuwa likizunguka kwenye kichwa chake , kila alipojaribu kufikiria ni kama mtu aliekuwa akikosa jibu .
Upande wa wakina damiani walikuwa wakipita mbagala rangi tatu na muda huo hakukuwa na magari mengi hivyo safari yao ilikuwa fupi mno ,
“ janeth nadhani una mengi ya kunieleza “ aliongea damiani .
“wewe pia una mengi ya kunieleza damiani “ aliongea janeth na kumfanya damiani atabasamu , lakini pia na Abasi aliekuwa akiendesha gari atabasamu .
Muda ulikuwa umeenda sana wakati damiani wanafika nyumbani kwake makongo juu , kichwani mwa damiani alikuwa akiliwazia gari la Merina , hakujua kama gari hio ilikuwa salama au lah , alikuwa akikumbuka tukio zima lililomtokea siku ya jana yake , na alikumbuka pia gari ile aliiacha ikiwa nje , lakini hakutaka kuwaza sana , kwani aliamiani hata kama gari hilo litaibiwa , angekuwa na uwezo wa kulipata , lakini pia aliona hata kama aisngelipaata angekuwa na uwezo wa kununu lingine na kumpa mimbwende huyo .
Baada ya wao kufika kila mtu alikuwa amechoka mno , na kati ya wote waliokuwa wameochoka damiani alikuwa ndio amaechoka Zaidi na isitoshe njaa ilikuwa ikimuuma sana , kwani ni muda kidogo alikuwa hyajapata chakula , kwani sehemu ile alieokuwa amefungiwa , japo mzee yule zakayo aliemuacha kumuangalia damiani alimletea chakula , lakini kwa damiani hakukigusa kabisa
Janeth baada ya damiani kwenda kuoga aliingia jikon na kuangaa chakula ,kwani wote walikuwa hawajala , na isitoshe janeth siku yote nzima alikuwa na mawazo juu ya damiani.
Baada ya lisaa walikuwa mezani watu watatu wakijipatia chakula .
“mlijuaje niko pale ?”
“ lilikuwa ni swali la damiani kwenda kwa janeth “
“ tulipata intel kutoka kwa mtu sehemu uliokuwepo “
“ kutoka kwa nani ?”
“ anonymous “ akimaanisha mtu ambae hajulikani
“ ilikuwaje mpaka mkapata hio intel , janeth wewe ni nani ?”
“ damiani wewe ni nani ?”
“ naona mnarushiana maswali ,, mnaonaje tukila kwanza then tukapumzika na kesho mkapeana majibu “. Aliuongea abasi na alichokiongea kilionekana kuwa na maana kwa wote wawili ,kwani kila mtu alikula na baada ya kula kila mtu alieleka upande wa chumba chake huku abasi akilala chumba cha wageni kwani ilikuwa ni mara yake ya kwanza kufika ndani ya nyumba hio .
*****
Ilikuwa ni asubuhi nyingine asubuhi iliotawalia na jua , wanasema waswahli siku njema au mbaya huonekana asubuhi na usemi huo ulikuwa ukitimilika katika asubuhi ya bwana kimbona , kwani ripoti aliokuwa akiitarajia kutoka kwa vijana wake ,, ilimfanya siku yake hio ya asubuhi kuharibika mno .
Hakuamini tukio kama hilo lingetokea , kwani siku hio alikuwa akiamini kabisa kwamba alikuwa anaenda kukutana na mtu aliekuwa akimfatilia kwa muda mrefu sana , Damiani rabani , mtu ambae alikuwa akiwakosesha usingizi usiku na mchana , hakujua kijana huyu alikuwa na bahati ya namna gani , kwani alionekana kuvuka kila kiunzi walichokuwa wakimuewekea , jambo hilo lilizidi kuwa gumu sana kwao .
Baada ya kupokea simu hio kutoka kwa vijana wake kwamba damiani alikuja kuokolewa na mtu ambae hawakuwa wakimjua lakini alikuwa na haiba ya kike , alitoa simu yake na mtu wa kwanza alietaka kumpigia wakati huo alikuwa ni zakayo .
Dakika kadhaa simu ilikuwa imepkelewa .
“ zakayo umefanya nini , mbona ni kama uliwauza vijana wangu”
“ unazungumzia nini kimbona “
“ inamaana mpaka sasa hauna taarifa kwamba damiani kaja kuokolewa ?”
“ sina taarifa hioo “ aliongea zakayo huku akijifanya kama mtu ambae ni kweli alikuwa ndio kwanza anapokea taarifa hizo kumhe alikuwa akijua kila kitu na alikuwa akiweka maigizo tu .
“ vijana jana walienda site kumchukua damiani , lakini katika process alitokea mtu aliejifunika uso mwenye haiba ya kike na kuwapiga vijana wangu na kuondoka na damiani , unauhakika haujawauza vijana wangu kweli ,, maana swala hilo tunalijua mimi na wewe tu , inawezakanaje mtu mwingine kufika eneo la tukio “.
“ mkuu nadhani umeenda mbali sana , mimi nimekufanyia kazi yako kwa weredi kabisa , inawezakana vipi mimi nikuuze , labda nikuulize ni watu wangapi wanamtafuta damiani “ aliuliza zakayo na hapo kimbona ni kama akili ilikaa sawa .
“ ni wengi “
“ kama ni hivyo , unahaukakika kwamba ni wewe tu unaojua uwepo wa damiani nchini “
“ tupo watu wawli tunaomtafuta damiani kwa udi na uvumba na kama ulivyosema ni kweli haujatoa taarifa hii kwa yoyote basi itakuwa ni mheshimiwa raisi , na kama vjana walivyosema mtu aliekuja kumchukua damiani ni mwanamke basi atakuwa ni suzzane “
“ umeona sasa mheshimiwa ,, inakuwaje unanituhumu kabla ya kulifikiria swala kama hilo “
“ lakini hata kama bwana zakayo ,, unafikiri kama kweli ni suzzane kajuaje kama tuko eneo lile “
“ hio inawekana , huenda alikuwa akiwafatilia vijana wako , au huenda pia kwenye kundi la vijana wako kuna mtu wake , yote yanawezekana ,, lakini pia huwezi ukamdharau suzzane kiasi hicho yule ni komandoo ana mafunzo ya kipelelezi “
“ ni kweli bwana zakayo naomba unisamehe katika hilo , lakini nadhani utanisaidia katika kumtafuta tena damiani “
“ mkuu kama ulivyosema kwamba mheshimiwa raisi ndio alikuwa akimuhitaji damiani na kama suzzane ndio, kwangu itakuwa ngumu kulifanyia hilo kazi , na tukio limetokea jana , huenda mpaka sasa damiani atakuwa amekwisha onana na raisi au walichokuwa akikihitaji kutoka kwake washakipata “.
“fuuuuuuck “ aliongea kwanguvu kimbona mara baada ya kukata simu , aliamini ni jambo baya sana kama mheshimiwa atakuwa tayari ashapata nyaraka alizoacha bruno .
Hakutaka kuzubaa aliamua kumpigia na sam na kumueleza kila kitu .
“ kimbona niseme vijana wako walikuwa wazembe sana katika hili , lakini hatuwezi tukahitimisha moja kwa moja kama mheshimiwa ashampata damiani”
“ unataka kushauri nini .. maana mpaka sasa kichwa changu kimekwama “.
“ kama mheshimiwa keshampata damiani litakuwa jambo jema pia , sio mbaya kwetu japo mpango wetu mimi na wewe utakuwa umekwama , lakini ndani ya U-97 ni jambo jema , hivyo inatupasa kujua kwanza kama ni kweli mheshimiwa ashampata damiani , na kama ashampata inabidi taarifa zote zitakazopatikana kutoka kwa damiani zijulikane ndani ya umoja .”
“ kwa hio tunalifahamu vipi hilo kama kashampata , akiamua kutudanganya “
“ kuna namna kimbona , hilo niachie mimi “ aliongea sam na kisha simu ilikatika
Huku upande wa ikulu raisi alikuwa kwenye mshituko na hio ni mara baada ya suzzane kutoa taarifa kwamba alimkosa damiani na kujeruhiwa , lakini licha ya mshituko huo pia ilikuwa ni afadhaali kwake pia kwamba kimbona na wenzie walikuwa wamemkosa kijana damiani , lakini jambo pia lililomshangaza Zaidi ni juu ya uhusikaji wa janeth ,, mwanadada ambae alikuwa akimjua kama proffesa.
ITAENDELEA
SEHEMU YA 69
THE FEAR OF TECHNOLOGY (OGOPA SANA TEKNOLOJIA )
Upande wa damiani baada ya kuamka siku hio hakupanga kwenda kazini na janeth vile vile , abasi peke yake ndie alietoka siku hio asubuhi asubuhi na kuondoka ndani ya nyumba hio akiwaacha damiani na janeth wakiwa wamelala
Masaa kadhaa mbele mtu wa kwanza kuamka alikuwa ni damiani , alijikongoja mpaka bafuni na kisha alijiswafi,, wakati akiendelea kuoga kuna jambo alijikuta akilikumbuka , ni flashi aliopewa na mke wa raisi huku maelekezo yake akiambiwa kwamba inatoka kwa bruno , jambo hilo ni kama lilimjia akilini muda huo kwani alijikuta akioga haraka haraka , na pasipo hata ya kujifunga taulo alitoka na kwenda chumbani kwake kuikagua suruali aliokuwa ameivaa jana , na ile baada ya kuingiza mikono kwenye mifuko sehemu ambayo alikuwa akikumbuka vyema kwamba ndio sehemu aliokuwa ameihifadhi , hakuiona , alijipekuwa kila kona ya mifuko lakini hakuipata kabisa , lakini wakati akiwa anahangaika mara mlango ulifunguliwa na janeth aliingia bila ya hodi na kumkuta damiani akiwa na anahangaika na suruali yake .
Janeth alijikuta akimkodolea damiani macho kwani damiani alikuwa uchi wa mnyama , , janeth macho yake yalikuwa kwenye kiungo cha damiani kilichokuwa kimelala , damiani na yeye japo ya kumuona janeth alikuwa ni kama mtu aliekuwa amepigwa na ganzi , kwani mpaka alipokumbuka kwamba hakuwa amevaa kitu zililikuwa zimepita sekunde kadhaa , janeth wala hakuwa na aibu kabisa ,nadhani ni kwasababu ya kukaa sana nchi za nje , kwani aliingia , na Damiani alivuta taulo na kujifunika .
“mbona unaonekana kama una mawazo “ aliongea janeth huku akaitabasamu akimsogelea damiani
“ kuna kitu nimepoteza “ aliongea damiani huku akiinama sehemu aliokuwa ameweka ile suruali yake .
“ ni muhimu sana ?”
“ sana ,, ni muhimu mno “ aliongea damiani kama mtu aliekuwa anawasiwsi , na jambo hilo janeth aliliona kwenye macho ya damiani .
“ utakipata , unaweza kuniambia ni kitu gani labda?”
“ ni flash dsk ,, ni muihimu kwangu ,, kuna mawili inawezakana niliindoosha wakati nashambuliana na suzzane , au mtu wa jana alieniteka hapo nje ndie aliechukuwa na hata simu yangu pia siioni “ aliongea damiani .
“mpaka hapo basi unapakuanzia ,, huna haja ya kuwa na wasiwasi namna hio “
Damiani alijikuta akivuta pumzi na kuzishusha na kisha alimwangalia janeth .
“ kuna kamera za getini , nadhani zilinasa tukio la mimi kutekwa “ aliongea damiani na kisha hakutaka kupoteza muda , kwani alimpita janeth na kuongoza upande ambao kuna chumba cha kuongozea kamera .
Baada ya kuingia ndani hapo huku akiwa na taulo lake kifua wazi , aliingia na janeth , aliangalia matukio ya jana yake na hapo ndipo aliposhuhudia kila kitu , na ni kama mtu aliemteka alitaka aonekana na kamera , kwani aliiangalia kamera vizuri na sura yake kuonekana .
“ zakayo “ alitamka janeth
“ unamjua “
“ ndio “
“ ni mwanamitindo , lakini pia ni mmiliki wa kampuni ya mavazi ya Z- stylish wear “
“ naijua hio kampuni nishawahi kufika hapo “
“ ndio , lakini inakuwaje zakayo akakuteka na anaonekana kuwa ni mtu hatari maana ukiangaia hata tukio la kukuzimisha lilikuwa ni kama mtu mtaalamu sana”
Na hapo hapo kumbukumbu za janeth zilianza kurudi , siku ambayo zakayo alifika kwenye kampuni yao ya NLT na kutaja jina la damiani , kitu ambacho hakukitegema kwa mtu kama zakayo kujua jina la damiani .
“ nadhani sasa ndio naelewa ubini sahihii wa zakayo “ aliongea janeth
“ unamaanisha nini ?”
“ ashawahi kuja ndani ya ofisi yangu na kutaja jina lako , mpaka sasa nishajua zakayo anaweza akawa ni mwanausalama , lakini nina namna ya kulitambua hilo “ aliongea janeth na kisha alitoka na kufata mkoba wake .
Alitoa tablet ambayo haikujulikana ni brand gani ya rangi nyeupe , iliokuwa na herufi moja tu ya neno ‘D’.
“ naomba unitumie hio hiyo video “
Aliongea janeth na muda mfupi tu tayari video ilikuwa kwenye ile tablet na baada ya dakika kadhaa za kugusa gusa na kupangusa ,, hatimae tablet ile ilianza kuscan picha ya zakayo ,, na ilichukuwa dakika moja tu ,, tayari alikuwa na majibu ya maswali yake .
“mwanaume anajua kuplay undercover huyu “ aliongea janeth na kumfanya damiani achukue ile tablet na kuanza kusoma taarifa .
“ ni Special undercover agent .. inaonekana yupo level sawa na ya suzzane na danny”.
“ unaamnaisha danieli mtalemwa kama ni huyo hawawezi wakawa sawa?”
“ unamjua danieli mtalemwa? “
“ ndio ni jasusi class A na ni komandoo “
“ unaokeana kujua mambo mengi Janeth ,, wewe ni nani? “.
“ kabla ya kukujibu hilo swali nataka nikuambie jana kukuuliza wewe ni nani ilikuwa geresha tu ,, kiufupi Damiani nakujua wewe kila kitu “
“unanijua vipi mimi ?”. aliuliza Damiani huku akimkazia macho Janeth kama mtu huku akiwa na hamu ya kutaka kusikia ni kwa namna gani janeth anamjua damiani .
“ nimepata taarifa zako kupitia faili la wazalendo “
“ inamaana na wewe upo kwenye orodha ya wazalendo raisi bendera aliowachagua ?”
“ jibu ni ndio lakini kuna Zaidi ya hilo “
“ lipi hilo ?”
“ mimi ni mtoto wa marehemu raisi bendera “ aliongea janeth na kumfanya damiani ashituke
“ unasema kweli ,, mbona katika orodha ya watoto wa bendera haujulikani ?”
“ siwezi kujulikana .. ndio lakini mimi ndio mtoto wa kwanza wa raisi bendera .. mama yangu ni mke wa raisi wa sasa “
“ unamaanisha madam wema ndio mama yako ?”
“ ndio”
Damiani alijikuta akishangaa sana , japo ni kweli umri wa janeth ulionekana kuwa mkubwa kidogo lakini hakutegemea janeth kuwa mtoto wa raisi bendera
“ ulikuwa wapi muda wote “
“ ni stori ndefu sana damiani lakini ufupi nikwamba raisi henry hajui uwepo wangu duniani kama mtoto wa bendera , kwani mama alificha mahusiano yake na baba”.
“ kwanini wafiche mahusiano yao , unataka kuniambia kwamba madam wema alikuwa akimsaliti raisi henry ?”
“ hapana , mama alikutana na raisi bendera kabla na ndio mwanaume wa kwanza kwa mama yangu , mama na baba walipotezana wakati wanamaliza kidato cha nne songea baada ya hapo mama ndio alibeba ujauzito wangu bila ya baba kujua ….” Janeth alianza kumuhadhithia mkasa mzima wa mama yake na raisi bendera .
“katika stori yako umesema unae mdogo wako ?”
“ huyo mdogo wako baba yake ni nani ?”
“ bruno lamberk “ damiani alijikuta akizidi kushangaa Zaidi , na kwanzia hapo alianza kukumbuka maneno ya bruno aliomuambia kuwa amtafute mtoto wake , huku akimpa kidani ambacho alisema kuwa ndio utakuwa utambulisho wa namna ya kumpata mtoto wake .
“ aisee .. ni stori ya kusisimua mno , kwahio mpaka sasa raisi henry hajui kama mama yako ana watoto wawili “
“ mheshimiwa raisi hajui uwepo wangu , ila anajua uwepo wa mdogo wangu pekee huyo aliepotea”.
“pole sana janeth ..”
“ pole ya nini ?”
“ umeweza kuishi pasipo malezi ya mama na baba si jambo dogo “
“ ni kweli lakini baba alikuwa akinitembelea mara kwa mara na hata mama pia , wote walikuwa wakinipenda sana na nasema mpaka sasa mama ananipenda sana kwani kwake ananiona kama moja ya kumbukumbu kubwa raisi bendera alioiacha hapa duniani “.
“ ni kweli kabisa ,, lazima iwe hivyo , lakini hujaniambia kuhusu swala la mzalendo wewe unahusika vipi “.
“ niliingizwa kwenye mpango wa uzalendo mara tu baada ya kumaliza masters na hii ilikuwa ni shinikizo kutoka kwa baba “
“ shinikizo kutoka kwa baba yako ?”
“ ndio , naweza kusema baba aliona kifo chake mapema sana , nakumbuka mara ya mwisho wakati ananitembelea nikiwa china aliniambia neno moja tu kwamba watu anaowaamini ndani ya uongozi wake ni wachache sana au hakuna kabisa .
“ inakuwaje akakitabilia kifo chake ,, unataka kuniambia kuna watu ambao walikuwa wakitaka mheshimiwa afe “.
“ ndio , hilo nina uhakika nalo asilimia mia moja na nipo hapa nchini kwa ajili ya kulifatilia hilo , lakini pia kumalizia kile baba alichokianzisha “
“ ni kipi baba yako alichokianzisha “.
“U-97”.
“huu umoja ndio kwanza nimeusikia na sijaujua undani wake kwa ujumla , unaweza ukaneleza unahusu nini , maana hii ni mara ya pili kama sio ya tatu kuusikia “.
“hata mimi sina mengi niyajuayo kuhusu umoja huu kwani mengi ni siri , ila kwa machache nnayoyajua nitakueleza siku nyingine , nadhani kwasasa ni muda wakufatilia kile ulichopoteza , na mtu wa kuanza naye ni zakayo “
“ kweli kabisa inabidi nianze na huyu zakayo “
*****
Upande mwingine jasusi wetu mpenda hela alikuwa kwenye gari yake ya kifahari akiwa anapita maeneo ya mikocheni na ndani ya masaa machache alikuwa akikatiza mtaa ambao ubalozi wa Kenya ulikuwa ukipatikana , dhumuni kubwa kwenye kichwa chake siku hio ni kwenda kujipatia hela , kwani ukiachna na kazi ambazo alikuwa amepewa na kimbona pamoja na kundi la mstaafu Matinde lakini bwana njoroge , balozi huyu kwa kenya pia alikuwa amempa kazi ya kumfatilia bwana stephano lamberk .
Aliingiza gari yake vyema na kwenda kuegesha katika eneo maalumu na baada ya hapo alitoka na moja kwa moja alipita mapokezi na kuonana na sekretari na kumueleza kuwa yupo eneo hilokwa ajili ya kuonana na balozi .
Secretary yule kwakua alikuwa na taarifa muhimu zinazomuhusu bwana zakayo aliruhusiwa moja kwa moja kuingia ofisi ya balozi.
“ karibu sana zakayo “
“ nashhukuru sana balozi “
“ nimefurahi sana jana ulivyonipigia simu kwamba kazi ulikuwa umeikamilisha , hebu pasipo kuchelewa leta matokeo ya kazi “
“ mheshimiwa nadhani wakati unanipa kazi hatukuongea malipo ya kazi yangu , nadhani swala hilo likianza itapendeza Zaidi “
“ hahaha .. nakuelewa bwana zakayo najua kazi yako inahitaj malipo na mimi kwa busara zangu nmekuandalia vibunda “
“ jumla ni ngapi ?”
“ milioni kumi “.
“sihitaji cash lakiini muheshimwa “
“ ni wewe tu zakayo mengi hapa ubalozini yanawezekana “
“hakuna shaka “.
“ leta kazi kwanza nione matokeo ndio nikamilishe muamala wako “
“ hakuna haja ya wewe kutoniamini muheshimiwa , mimi kazi zangu ni za viwango hivyo endelea tu na uthibitisho wa muamala “
Balozi alimjua vyema zakayo kwa kupenda pesa , hivyo hakutaka kuongea sana , kwani pia alikuwa akimuamini jasusi huyo katika maswala mazima ya kazi za kipelelezi.
“ enhe niambie sasa ,, nadhani upande wangu umekamilika umebaki wa kwako “
“stephano lamberk na damiani ni kitu kimoja “
“ ahahaha.. bwana zakayo labda sijakuelewa vizuri , inawezekana vipi wakawa kitu kimoja “.
Zakayo hakutaka kuongea sana alianza kutoa picha za stephano lamberk na kuziweka mezani na kisha alitoa picha za damiani na kuziweka mezani .
“ huyu ndio damiani kijana uliemsaidia miaka kadhaa nyuma “
“Ndio nakmkumbuka vyema huyu kijana “.
“ sasa huyu kijana yupo hapa nchini , na picha unazoziona ni za jana “ aliongea zakayo .
“ mpaka hapo nimekuelewa lakini pia sijakuelewa kwenye jambo moja , umesema Stephano lamberk na Damiani ni kitu kimoja , inawezekana vipi? “
“huyu ni Stephano lamberk , huyu ni Damiani , ukianagalia urefu unene na saizi ya sura kila kitu kinafanana , hilo ni la kwanza , la pili mahali anapoishi Stephano lamberk ndio mahali anapo ishi kijana Damiani , uhakika zaidi ni kwamba siku ya jana nzima niliweza kumshikilia kijana Damiani , na nikajaribu kumfatilia bwana Bruno lamberk na kwa taarifa nilizokusanya ni kwamba jana Stephanoo lamberk hakuonekana mahali popote pale hata nyumbani kwake “ aliongea Zakayo .
“ kama unayoyazungumza ni kweli , je inawezakana vipi huyu Damiani kuwa na sura mbili yaani ya stephano lamerk na ya kwake usiniambie ni kama Osam bin Laden”
“ hilo sijui mpaka hapo.. ila asilimia mia moja nina uhakika wa kwamba Stephano lamberk ndio huyu Damiani , haya yote yanaweza yakawezeshwa na maswala ya teknolojia muheshimiwa nadhani muda si mrefu kila kitu kitakuwa wazi “
“ kama ni hivyo basi ninapaswa kusubiri , lakini pia nitamtembelea mimi mwenyewe Stephano lamberk ili kujua kama ni kweli Damiani “
“hakuna shaka “ aliongea Zakayo na kisha aliaga na kuondoka huku dhumuni la kujipatia pesa lililompeleka hapo ubalozini lilikuwa limefanikiwa kwa asilimia mia moja .
MOTO UNAOKUJA SI WA KITOTO STAY TUNED
UNAWEZA ENDELEA KUSOMA KWA 3000 TU LIPIA NAMBA HIZI 0687151346 JINA ISSAI SINGANO THEN NI TEXT WATSAPP

NB : Unapata yote hadi mwisho

SEE YOU KWA VIPANDE VINAVYOENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom