singanojr
JF-Expert Member
- Sep 24, 2020
- 1,420
- 7,906
- Thread starter
- #21
SIMULZI YA KIJASUSI
UMOJA NAMBA TISINI NA SABA
KAULI YA MWISHO YA RAISI
MWANDISHI : ISSAI SINGANO
NAMBA : 0687151346
SEHEMU YA 12
Tulipoishia ni pale kijana damiani kutekwa na mtu asie fahamika
ENDELEA NAYO
Ilikuwa ni muda wa saa mbili asubuhi bwana kimbona akiagana na mke wake kwa ajili ya kuelekea ikulu , na hatimae alifanikiwa kupata nafasi ya kukutana na muheshimiwa , kutoka masaki mpaka ikulu hakukuwa na umbali mkubwa sana , dereva wake alitumia dakika ishirini kufika ikulu .
Alipita getini mara bada ya kukaguliwa na akaruhusiwa kisha akaongozwa na mwanadada mmoja mrembo alievalia suti nyeusi , ambae alikuwa ni sekretatary wa raisi .
“ karibu sana kimbona “ aliongea mheshimiwa henry huku wakikaa kwenye masofa .
“ mheshimiwa kwanza niseme nashukuru kwa kuitikia wito wangu wa kuonana na wewe “
“ ni kweli kabisa , hii ni mara ya pili tunaonana sasa , na nadhani tutazidi kuonana siku za usoni “
“ ni kweli muheshimiwa , nashukuru sana “
“enhe sasa twende kwenye swala lililokufanya uombe kuonana na mimi “
“mkuu kama siku ile kwenye kikao tulivyokubaliana juu ya mali za bwana Bruno , mpaka sasa imekuwa ngumu kupatikana kwa nyaraka zinazohusu mali zake , kwani bila nyaraka hizo hakuna uwezekano wa kuzitumia kwani zipo chini ya sheria mpaka sasa , mpaka pale mrithi halali atakapo tokea “
“ ndio nalielewa hilo kimbona “
“ sasa basi ni kwamba mpaka sasa juu ya upatikanaji wake umekwama hivyo nahitaji msaada wako “
“ msaada gani kwangu unaohitaji ??. “
“ kwa kifupi ni kwamba mpaka sasa nyaraka hizo tunaamini anazo danny “
“ unamaanisha danieli mtalemwa ?”.
“ ndio muheshimiwa , huyo ndio tunaamini anazo , kwani mtu wa kwanza tuliekuwa tukimshuku inaonekana kutojua juu ya nyaraka hizo “
“ kama anazo danieli mtalemwa itakuwa ngumu sana kuzipata , maana danieli kama amekabidhiwa na Bruno basi haitokuwa rahisi kumshawishi atupatie nyaraka hizo .“
“mheshimiwa sina mpango wa kukaa chini na danniel kumshawishi juu ya hili , nataka nizichukue kwa namna yoyote hata kama ni ya kimapigano “.
“ hahaha … kimbona , unafikiri hilo linawezekana , labda tupeleke jeshi , lakini hilo ni swala ambalo haliwezekani kabisa sheria haziruhusu “
“ naelewa muheshimiwa , kuna mtu anawezakuifanya kazi hio kwa umakini mkubwa na ikafanikiwa , hivyo nahitaji msaada wako “
“ mtu gani huyo unahitaji msaada kwangu ?”
“ carlos Cardoso “
“kimbona huyo mtu ndio nani , sina taarifa zake “
“ mheshimiwa huyo ni muuaji wa kimataifa , kwa taarifa nilizonazo ni kwamba carlos alikamatwa hapa nchini Tanzania katika moja ya kazi aliotumwa na U-97 ya kumuua Bruno , lakini kupitia TISS na jeshi walimkamata “
“ kimbona sina taarifa ya mtu huyo kushikiliwa hapa nchini “
“ inawezekana muheshimiwa huna hizo taarifa lakini mimi nina tarifa ya bwana huyo kushikiliwa hapa nchini na taarifa hizo lazima TISS wanazo ila ni top secret “
“ kama ni kweli unataka nikusaidije kuhusu hilo??. “
‘ nataka umtoe gerezani awe huru ili atufanyie kazi yetu kwani huyo ndio mtu pekee alieweza kumpiga danny mpaka akapoteza fahamu “.
“kimbona sina mamlaka ya kutoa wa fungwa wa aina hio gerezani “.
“mkuu humtoi gerezani kwa oda yako , ila kuna jambo nataka ulifanye nasisi tutamalizia kumuweka huru “
“ jambo gani ??“
“ kwanza kabisa inatakiwa tufahamu anashikilwa katika gereza lipi , baada ya hapo utoe agizo la mfungwa huyo kuhamishiwa gereza lingine na sisi tutamaliza kazi”. Mheshimiwa alifikiria kwa muda .
“ kimbona inabidi kwanza nijue taarifa kamili za huyu mtu , maana nimehudumu nchi hii kama makamu wa raisi lakini sina tarifa zake , nikishafanikisha hilo nitakupa jibu “ aliongea mheshimiwa kisha aliagana na kimbona .
Baada ya kimbona kuondoka , raisi hakutaka kabisa kulifumbia macho swala hilo , kwani kitendo cha kuwa mkuu wa nchi halafu jambo kama hilo halifahamu kwake ilimtia ukakasi kidogo .
Alitoa simu yake kisha aliongea na mkuu wa TISS bwana elly matinde .
“ nahitaji faili la carlos cardoso ofisini kwangu “ aliongea raisi . na kumfanya mkuu wa TISS anyamaze .
“ mkuu hilo swala ni classified na lipo chini ya umoja wa taifa mheshimiwa “. Henry alijikuta akianza kupandwa na hasira ila alijaribu kujizuia .
“ bwana matinde , mimi ndio mkuu wa nchi , hivyo nakupa masaa mawili nahitaji faili hilo hapa ofisini kwangu “ .alikata simu
“unanijibisha mimi , muda sio mwingi lazima nikutoe kwenye hio nafasi “ alijiongelesha mwenyewe , na alionekana alikereka sana. .
Masaa mawili baadae bwana matinde alifika ofisini hapo akiwa na faili husika , alisalimiana na mkuu wake .
Alichuku faili lile na kulisoma kwa umakini mkubwa kisha baada ya kumaliza alimwangalia matinde .
“nashukuru sana , unaweza kwenda nalo sasa “ aliongea henry na matinde aliaga na kaondoka .
Siku mbili mbele taarifa ya kubadilishwa kwa mkuu wa TISS na mkuu wa police IGP kizito kabwela zilitangazwa katika vyombo vya habari , kila mtu alishangazwa na uamuzi huo , huku kila mwananchi akiongea lake , lakini mamuzi yalikwisha fanyika na hakukuwa na wa kupinga, huku uapisho wa wakuu wapya ukifanyika siku ya pili yake .
Mkuu mpya wa TISS alikuwa ni bwana yusuph majid , huku mkuu wa polisi IGP akiwa ni aniseth kanyama wote waliapishwa ikulu .
Baada ya kuapishwa taarifa nyingine ya kuhamishwa kwa mkuu wa polisi kanda maalumu jiji la dar es salaam bwana hashimu juma alihamishiwa mkoni Arusha .
“nimekuita hapa ofisini , kuna mabadiliko kidogo yanatakiwa kufanyika katika magereza , wafungwa wafuaatao nataka wahamishiwe kutoka gereza la ukonga na kuwapeleka gereza la morogoro “ aliongea raisi akimpa maagizo bwana aniseth kanyama.”
“ ndio muheshimiwa nitafanya kama ulivyoagiza “
“hakikisha swala hilo linakuw siri “
“ sawa muheshimiwa “.
Baada ya agizo hilo raisi alitoa simu yake na kumpigia kimbona na kumwambia tayari wafungwa watapelekwa gereza la morogoro kesho kwa hio ahakikishe kazi inafanikiwa .
Baaada ya kimbona kupata simu hio kutoka kwa raisi alipanga timu yake na kuwapa ramani nzima ya magari yatakapo pitia na sehemu ya kufanya misheni yao .
“tukio litafanyikia mkese “ aliongea kimbona huku akiwaangalia vijana wake
“Kutoka dar mpaka mkese ni masaa mawili , mkifika hapa mkese mtapokea ujumbe wa gari alilopanda carlos , lakini mtasubiri mpaka mpate amri nyingine ya kuyasogelea magari , hakuna kufanya mauwaji ya aina yoyote , kazi ni moja tu kumchukua carlos Cardoso .” aliongea kimbona akiwa ofisini na vijana wake wa kazi .”
“ ndio muheshiiwa tumekuelewa “.
“ safi , kama mmenielewa mna swali lingine ?”
“ mkuu hatuna “
“ hahaha….. mnaona sasa msivyo makini , huyu carlos mnamjua ?”
“ hapana mkuu “
“ sasa hilo ndio swali , nataka muwe makini katika hili , picha yake hii hapa “ .
Vijana walitawanyika kwa ajili ya kusubiria siku ya kesho kwa ajili ya kuanza kazi , hatimae siku yenyewe iliwadia , kimbona alipokea muda wa wafungwa hao watakapotolewa gereza la ukonga .
“ watatolewa saa kumi na mbili kamili ukonga “” ilikuwa ni sauti kutokea kwenye simu na haikujulikanna alikuwa akiongea na nani .
Kiongozi aliekuwa akiongoza kundi la bwana kimbona alikuwa ni meja , ni bwana mmoja ambae alikuwa na mwili wa mazoezi , mwenye sura pana ambayo muda wote haikuwa na tabasamu , meja aliwapanga vikosi vyake ndani ya kijiji cha mkese kwa ajili ya kukamilisha misheni waliopewa na boss wao , hakutaka kabisa swala hilo lifeli na ndio maana alikuwa makini kabisa brabarani , saa moja na dakika kumi ndio muda waliokuwepo ndani ya eneo hilo wakiwa kwenye gari walilolipaki mita kadhaa kutoka kwenye makazi ya watu .
Ilipotimu muda wa saa moja na nusu alipokea ujumbe wa gari alilokuwa amepandishwa carlos Cardoso , aliwapa wenzie taarifa na kisha walijipanga kwa umakini mkubwa , kwanza kitu cha kwanza walichokifanya ni kusimamisha gari katikati ya barabara na kisha walijificha pembeni ya barabara .
Wakati wakiwa wamejificha meja , alipokea simu . namba ilikuwa mpya .
“ get ready “ ilisikika sauti ya mwanamke kwenye masikio yake .
Huku upande wa juu kabisa juu ya mti kulionekana kuna mtu aliekuwa amelalia tawi huku akiwa ameshikilia bunduki aina ya sniper riffle .
Saa mbili kamili magari matatu yalifika eneo la mikese mbele ilikuwa ni gari la polisi juma pia kulikuwa na gari la pollisi katikati lilikuwa na karandinga lililokuwa limebeba wafungwa , gari ilipita makazi ya watu na kusonga mbele na hapo ndipo polisi walipo ona gari iliokuwa imezuia barabara , kama ujuavyo polisi wa kitanzania kukereka , basi walishuka pasipo kuwa na umakini na kulisogelea gari lile aina ya noah .
Ndani ya kalandinga alionekana jamaa mmoja aliekuwa na midevu mingi , mwenye mwili uliokuwa umejazia , alikuwa ni bwana wa rangi nyeupe aina ya red Indians , jamaa mara baada ya kufika eneo lile , alijikuta akitabasamu , na ni kama mtu ambae alijua kinachoendelea , lakini kufumba na kufumbua bwana yule alionekana akidondoka chini palepale na kuwafanya wafungwa wengine wapige kelele na kushitua gari la polisi lililokuwepo nyuma.
Polisi wale walitoa bunduki zao aina ya SMG na kusogelea gari ile , lahaulah! Lilikuwa ni kosa kubwa , kwani polisi wale walidondoka mmoja baada ya mwingine , lakini cha kushangaza ni kwamba hakuna hata mmoja aliekuwa akivuja damu , polisi waliokuwa wametangulia mbele walikuwa wapo watatu na hawakujua nyuma wenziwe washaramba chuma , na kosa kubwa walilolifanya ni kutochukua tahadhari kwani ile wnalifikia gari walitokea watu watatu kwa nyuma yao na kuwazimisha pale pale .
“ mchukueni carlos , hakikisheni wafungwa wengine hawatoki “ ilikuwa ni sauti ya kimbona ikimpa maelekezo meja , aliwapa ishara wenzake na kuisogelea gari aliopandishwa carlos na kuchukua funguo kwa moja ya polisi .
“ wote geukieni nyuma , aliamrisha moja ya jamaa aliekuwa amejifunika uso na wafungwa wote waligeukia nyuma , wawili walibaki nje na mmoja aliingia ndani ya gari na kisha walimtoa carlos ambae muda huo alikuwa hajitambui , walimbeba mzobe mzobe na kutoka huku wale wawili wakifunga mlango .
“ ondokeni , watashituka baada ya dakika mbili “ ilisikika sauti ya mwanadada ikimpa maelekezo kwa njia ya simu .
Taarifa ilimfikia IGP mfungwa mmoja ametoroshwa na watu ambao hawajulikana ,huku polisi wakizimishwa na dawa ya usingizi wa muda mfupi kwa kutumia tranguilizer gun , IGP taarifa hio ilimchanganya kidogo , na hakutaka kubaki nayo mwenyewe , kwani alimjulisha raisi .
“ hakikish swala hilo linabaki siri , uchunguzi ufanyike siri kwa siri pasipo watu kujua , pili andika ripoti ya wafungwa hao kufikishwa salama katika gereza la morogoro “ yalikuwa maagizo kutoka kwa raisi na IGP alifanya kama alivyoambiwa .
Kimbona akiwa kwenye tabasamu zito mara baada ya kupokea simu kutoka kwa vijana wake , iliingia simu nyingine kutoka kwa raisi .
“habari mheshimiwa “
“ salama , sasa kimbona nimepata habari kwamba zoezi limefanikiwa , hongera sana , ila hakikisha baada ya nyaraka hizo kupatikana mtu wa kwanza kuzipata awe mimi “.
Kimbona alifikiria kwa muda na kisha alimkubalia mheshimiwa raisi .
Pembeni ya kiwanda cha katani cha kutengeneza magunia kilichopo morogoro , kulikuwa na jumba moja ambalo lilikuwa kama stoo , ndani ya jumba hilo ndio vijana wa kimbona ndio walimuingiza carlos huku wakiwa wamemfunga mikononi kwani walihofia bwana huyo akishituka anaweza akawapa kibano na akatoroka , baada ya kumuingiza walimuweka kwenye kiti na kumfunga tena na kisha meja alitoa simu na kumtaarifu boss wake kuwa wapo site huku wakimzindua na maji .
“muwekee simu sikioni “ aliongea kimbona na meja alifanya kama alivyo ambiwa .
“ carlos Cardoso “
“quem e` voce??( wewe ni nani ) aliongea kwa kireno .
“ My name is kimbona you probably don’t know me , I am the one rensponsible for getting you out of prison , I have a job I need you to do for me in exchange for your freedom ( naitwa kimbona kuna uwezekano hujawahi kunisikia popote , mimi ndio nimekutoa gerezani , kuna kazi nahitaji unifanyie , malipo ni kupata uhuru wako )
“falar estou ouvindo “ ( ongea na kusikiliza )
“Tomorrow we will meet to talk don’t try to escape because you will not be able to leave this country safely (kesho tutaonana , usijaribu kuwaletea vijana shida maana hutoweza kutoka nje ya hii nchi salama )“ aliongea kimbona kisha akakata simu .
Siku iliofuata asubuhi yake kimbona alifika ndani ya morogoro .
“There is documents I need and person who has them is Daniel(kuna nyaraka nazihitaji na mtu huyo anazo danieli )“ aliongea kimbona na kumfanya carlos ashituke .
“ danieli mtalemwa ?”
“yes , I think you know him well because you have met him , I released you from prison for that job (ndio , nafikiri unamfahamu vizuri maana ushawahi kukutana nae , sasa nimekutoa gerezani kwa ajili ya kazi hio “.)
“ I have condition “ akimaanisha kwamba ana sharti
“speak”
“ After your work I need you to assure my safety of leaving this country (baada ya kazi yako nataka unihakikishie usalama wa mimi kutoka nje ya nchi hii)”.
“ once the work is done you are free to go “ akiaamanisha kwamba pale kazi itakapokamilika ataweza kwenda .
“ not free to go , I want you to assure my safe exit “( akimaanisha kwamba sio kwenda tu , anataka amhakikishie kuwa atatoka kwenye nchi hii bila shida yoyote .
“ that is within my power , perhaps if there is onether “( akimaanisha kwamba hilo lipo ndani ya uwezo wake , labda kama kuna lingine “
“there is nothing more , important for everyone is to keep promise , if you go against it I will kill you “( hakuna la ziada muhimu ni kutimiza ahadi ukienda kinyume nitakutafuta popote pale na kukuua ).
“Well how many days will you complete the task , because at moment we don’t know where danny is”.(ni siku ngapi utakamilisha kazi kwasababu kwa sasa hatujui danny alipo ).
“I need week , I also need some informations about him to get me started , especially places where he recently appeared. ( akimaanisha kwamba anahitaji taarifa zinazomuhusu danny sehemu alizo onekna mara ya mwisho , pia kukamilisha hilo atachukua wiki moja ).
“The last time he appeared in Tanga Lushoto , when I sent my boys to kill Bruno, all you have to do is find damian rabani where he is, if you find him he will lead you to find him ( mara ya mwisho alionekana lushoto nilipotuma vijana wangu kumuua Bruno , unachotakiwa kufanya ni kumtafuta damiani na atakuongoza kumpata danny ).
“”and who is this damian and how close is he to this danny ?”(na huyu damiani ni nani na anah ukaribu gani na danieli ).
“thes are the questions I hoped for from you and my boys have given me this file , it contains all the information abaout him , car and other requirements about yur mission meja will give you , hope you will work out (hayo ni maswali ambayo nimetegemea kwamtu makini kama wewe hili ni faili nililotumiwa na kijana yangu kutoka kituo cha polisi lushoto lina taarifa zote zinazo muhusu damiani , mahitaji mengine kuhusu kazi yako utayapata kwa meja , natumaini kazi itafanikiwa kwa weredi )..
“ and last we will be communicating at every step you reach”( na jambo la mwisho tutakuwa tunawasiliana kwa kila hatua )
******
Ilikuwa ni siku kama tano tokea tukio la kutekwa kwa damiani litokee na siku mbili baada ya carlos kupewa kazi, upande mwingine ndani ya jiji la Tanga wilaya ya korogwe , kilomita chache kutoka mombo katikati kuna mji uliokuwa ukijulikana kwa jina la chekelei , ndani ya kijiji hiki mita kadhaa kutoka barabarani , kulikuwa na jumba kubwa lililokuwa limezungukwa na uzio mkubwa , ndani ya jumba hili liliingia gari moja aina ya brevis nyeupe , na kwenda kupark sehemu iliokuwa na gari lingine aina ya BMW , baada ya kupark alionekana mwanadada mmoja akitoka ndani ya gari hio ,alikuwa mweupe mrefu alievalia suruali ya jeans na sweta la mikomo mirefu huku nywele zake akiwa amezibana kwa nyuma .
Alizunguka upande wa pili nakufungua mlango na hapo alionekana kijana Damiani aliekuwa na mabendeji usoni akitoka nje ya gari hilo huku akichechemea , alisaidiwa na mwandada huyo kisha walifungua mlango na kuingia ndani .
"Danny tumefika " aliongea mwanadada yule akimuongelesha mwanaume aliekuwa amesimama akiwa anaangalia runinga .
Danny aligeuka na kuwaangalia na kumfanya damiani aanze kurudiaha kumbukumbu zake nyuma , kumbukumbu nazo zilimpeleka mpaka siku ya interview yake , mtu aliempa lift alimkumbuka vyema , lakini alishangaa mtu huyo kuwa pale mbele yake .
" Karibu damiani " aliongea daniel huku akiwaonyesha sehemu ya kukaa huku danny , alikuwana mwili ulioshiba mazoezi kwani siku hio alikuwa amevalia singlend tu na suruali ya jeans .
" asante " .
" Naona kwa mshangao huo utakuwa unanikumbuka vyema , maswali yako nitayajibu ,sasa hivi unatakiwa kupumzika kwanza " aliongea huku akimpa ishara yule mwanadada kwamba amfuate .
" suzzane nimepokea taarifa hapa carlos yuko huru , katolewa siku mbili zilizopita " .
" Unamaanisha carlos cardoso ?"
" Ndie huyo "
" imekuwaje akawa huru ?".
"Hilo silifahamu , lakini nina hisia raisi anahusika katika hili ".
" Kwanini unasema hivyo "
" kwasababu tukio la carlos kutoka limefanywa na watu ambao hawajulikani mpaka sasa , pili tukio limetokea mkese wakati alipo kuwa akihamishiwa gereza la morogoro , hapo unaweza kuona kuwa hakukuwa na sababu ya carlos kupelekwa morogoro , my feelings zinaniambia kuwa huu ulikuwa ni mpango wa kumtoa gerezani , kikubwa ni kwamba amri ya carlos kuhamishiwa morogoro inetoka kwa raisi , pili henry hakuwa akimjua carlos mpaka alipo pata taarifa hizo kutoka kwa mstaafu matinde "
" kwa muunganiko huo inaonekana kweli anahusika , lakini swali linakuja kwanini katolewa?? ".
"sababu lazima itakuwepo nafikiri unakumbuka moja ya kauli ya mwisho ya marehemu juu ya henry?? " .
" ndio nakumbuka ".
" Basi lazima tufahamu sababu kwanini katolewa , na njia ya kujua sababu ni kumkamata carlos tena na kuhakikisha anasema kike alicho agizwa , maana mpaka sasa kuna dalili zote za U-97 kurudi tena kwenye hii nchi na biashara ya madawa kuendelea , kazi ambayo tumeifanya kwa jasho kubwa kuitokomeza ."
" na vipi kuhusu damiani ?" ..
" Mpango uko kama ulivyopangwa , na utaratibu wa kumtoa nje ya hii nchi kwa ajili ya mafunzo uko pale pale kesho ataondoka rasmi kuelekea china.
Wakati ambao suzzane anaingia na damiani kwenye nyumba iliopo chekelei , gaidi wa kiamatafia carlos alikuwa hatua kwa hatua mpaka wakati gari ya suzzane ikiingia ndani hapo aligeuza gari na kuondoka
“vou voltar mais tarde “ ( nitarudi baadae usiku ) aliongea na kuondoka .