Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Hata hivyo, kwa kuwa inafahamika kwamba kuwatumia watu wengine kuchuma, sio kitu kinacholeta picha nzuri “As universal law’ hoja ya kuwasaidia wanaochumwa hutumika, na kutokana na uelewa mdogo wa wachumwaji, hukubali kutumiwa na mchumaji.
Hebu jaribu kufikiri, mtu anachukua mkopo benki ‘wenye riba’, anaingiza kwenye kampeni za siasa, anakuahidi kwamba lengo lake ni ashinde ili akusaidie, na wewe unamwamini. Pamoja na kumwamini, hauko tayari kumuunga mkono mpaka akuhonge, na bado unaamini kwamba pamoja na kukuhonga ataenda kukusaidia tena wewe. Yaani daktari, akuhonge ili ukubali akutibu! halafu ukipigwa kekundu unashangaa hahahah!
Kinachosababisha ujasiriamali wa ki - siasa ni kuwa na idadi kubwa zaidi ya wastani ya watu wanaoamini kwamba wao wako duniani kupokea kutoka kwa wengine “Takers” licha ya kufahamu kwamba jambo hilo ki uadilifu si bora. Kwa hiyo mwanasiasa naye kama sehemu ya jamii hiyo hiyo; anakuwa anaamini anatakiwa a ‘Take’ lakini pia anafahamu kuwa mtu mmoja mmoja kwenye jamii anaamini anatakiwa ku ‘Take’ vilevile.
Kwa hiyo anaitumia saikolojia hiyo mbovu ya jamii kuiahidi kwamba ita ‘Take’ kutoka kwake, na kwa sababu uelewa ni mdogo, basi jamii inakubali.
Matokeo yake jamii inapigwa 3 bila asubuhiiiii, badala ya ku ‘take’ inapoteza. Hapo ndipo unakuta watu wanalalamika toka tuchague mbunge wetu hatujamwona tena huu ni mwaka wa 4, anaonekana sinza na Dodoma tu. Hachangii hata siku moja. Amenunuliwa. N.k. Wanasahau walishapewa chao wakati wa kampeni. Hivi hata kama ni wewe ulikopa benki ukagawa pesa ili upate cheo flani (ubunge kwa mfano), unarudi jimboni?Na ukirudi utakuwa serious?
Ni nini cha kufanya? Kwanza tuelewe kuwa, kila mtu kwenye jamii anapoamini kuwa anatakiwa kuchuma kutoka kwa wengine, na kuna mtu yuko mahali anatakiwa ndio awe anatoa (wakati naye pia anaamini anatakiwa kupokea); hilo ni tatizo kubwa na ndio msingi wa yote haya.
Ili kutoka kwenye huo mzunguko, tunatakiwa tuanze kujijengea utaratibu wa kila mmoja wetu kujiambia "mimi ndiye ninayetakiwa kufanyia wengine, mimi ndiye ninayetakiwa kutoa, mimi ndiye ninayetakiwa kusaidia na nimekuja duniani kutoa sio kupokea ".Na hilo linatakiwa kuanza na wewe unayesoma hapa sasa. Kwa kadiri tutakavyokuwa na watu wengi zaidi wenye mtizamo huo; ndivyo tatizo litakavyopungua na kinyume chake ndivyo tatizo litakavyozidi kukuwa.
Tukiliweza hilo, tutapata viongozi wengi na sio watafuta vyeo wengi. Tutakuwa na watu wengi ambao wako tayari kutoa muda wao, rasilimali zao na akili zao kusaidia wengine kuliko kukaa mahali kusubiria kupokea.
Hawa ndio viongozi wanaoweza kuwa na tija kubwa. Ikumbukwe kiongozi si lazima awe na cheo lakini mtu anaweza kuwa na cheo na asiwe kiongozi. Ukiona mtu anatafuta sana cheo, ujue huyo ni ‘Taker’ na ‘Taker’ hawezi kuwa kiongozi bora hata siku moja.Viongozi bora huwa ni ‘Givers by nature’ na unaweza kuwatambua kwa wao kutumia walivyo navyo kusaidia wengine bila kutafuta fidia.