Ujasiri wa Rais Magufuli juu ya janga la korona katika ulimwengu wa roho

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,530
3,433
Awali ya yote napenda kutoa salamu za dhati kabisa kutoka katika kina cha nia yangu kwenu nyote nikiwa na uhakika salamu hii itapokelewa na kila mtu atakayesoma andiko hili na kuruhusu kuelewa zaidi ya uelewa ulivyo.

Natamani sana andiko langu niliweke katika lugha ambayo itamfanya kila mmoja kuelewa kwa urahisi kabisa kwa kuyaweka mambo ya ulimwengu wa roho katika hali ya wazi tofauti na yanavyochukuliwa na baadhi ya watu.

Ni vyema kabisa tukajua kuwa sisi sote ni viumbe wa kiroho tunaoishi katika mwili. Mwili ni kibebeo chetu na siyo sisi. Itakuwa vyema na wewe ukalitambua hili mapema kabisa ili unapoendelea kusoma andiko hili usitume shaka juu ya nitakayoyaandika.

Baada ya kutambua kuwa sisi ni viumbe wa kiroho tunaoishi katika mwili tunapaswa kufahamu pia sifa ya kuu ya ulimwengu wa roho na roho.

Zipo sifa nyingi mno za ulimwengu wa roho ila kwa kurahisisha uelewa wetu juu ya andiko hili ni kwamba ulimwengu wa roho ni ulimwengu wa milele, hauna mwanzo wala mwisho na pia hautawaliwi na mipaka ya mahali na wakati. Ulimwengu huu unaweza kuwa kila mahali na kila wakati.

Roho hayo ina sifa kama za ulimwengu wa kiroho ulivyo yaani haifungwi na gereza la mahali na muda kama ulimwengu wa mwili ulivyo ambao mwili wa kifuzikali huwa katika gereza la mahali na muda na hivyo kuwa katika mipaka mingi ya kuelewa na utendaji.

Kwanini natamani kuzungumzia ujasiri wa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania katika ulimwengu wa roho juu ya janga la Korona?..Hapa ndipo lilipo kiini cha andiko hili na ninatamani kila mmoja kuelewa ulimwengu huu unavyotenda kazi ndani yetu.

Ikumbukwe kuwa ulimwengu wa vitu hauna nguvu na hatuwezi kumba ila ulimwengu wa roho ndiyo wenye nguvu na ndiyo unaoumba vitu vinavyoonekana na kuakisiwa na milango ya fahamu ya mwili.

Katika ulimwengu wa roho ndipo vilipo vyanzo vya kila kitu chenye umbile lolote lile linaloonekana katika ulimwengu wa vitu tunaouhusi kupitia milango ya fahamu.

Kwa mantiki hiyo kila kitu hufanyika katika ulimwengu wa roho kabla ya kuchukua umbile halisi na kuwa kitu kinachodhihirika katika ulimwengu wa vitu. Ieleweke kuwa hata magonjwa makubwa yanayoikumba Dunia ikiwemo Korona ina asili katika ulimwengu wa roho. Mambo mengi kabla ya kujidhihirisha huwa yanakuwa katika hali ya kukosa umbile "form less" na yanakuwa katika ulimwengu wa roho.

Jambo lolote ambalo hatulitambui au hatulioni kupitia macho ya kimwili haimaanishi halipo. Ulimwengu wa roho una utoselezo wa kila kitu na una sifa ya umilele. Ulimwengu huu wa milele una kila kitu hivyo ni jukumu letu kuangalia na kuumba maumbile ya vitu hivyo.

Ugonjwa huu wa Korona umepewa umbile na kudhihirika Duniani haimaanishi haukuwepo hapo awali, kama nimeliweka vizuri ni kwamba ulikuwepo ila ulikuwa hauna umbile la kuudhihirisha Duniani.

Ili kuweza kuharibu umbile la ugonjwa huu wa Korona Duniani kinachohitajika ni nguvu za kiroho kuweza kuona chanzo na kutambua namna ya kuharibu umbile bila woga wala wasiwasi.

Mheshimiwa Rais anapotuhamasisha kuendelea kumtanguliza Mungu huku tukijiwekea hadhari na kuendelea na majukumu ni dhahiri kauli hii haibahatishi ila inayoambatana na nguvu ya kutuunganisha na akili ya kiumbaji.

Amekuwa akisema ugonjwa huu ni vita ya kiuchumi mara kadhaa huenda tunaweza tukachelewa sana kuelewa kama tunaishia kuangalia kwa kutumia macho ya nyama na kusahau kuangalia kiroho.

Anaposema hii ni vita tuelewe hii ni vita habahatishi ni suala la sisi kurudi katika ulimwengu wa roho na kuangalia kwa sababu ulimwengu wa roho haukosei na haubahatishi.

Watanzania tunahitaji nguvu za roho ili kuelewa na kufanya sawasawa na tulivyoelewa na siyo tofauti na hapo.Chanjo ya Korona siyo muhimu kama chanjo ya roho zetu. Tukumbuke chanzo cha Korona siyo umbile la kimwili lililodhihirika Duniani na kusambaa kila mahali ila ni umbile la kiroho lilochukua umbile la ugonjwa katika ulimwengu wa kimwili.

Kujiweka vizuri kiroho ni vizuri kuliko kujiweka vizuri kimwili ndiyo maana ila mara anatusisitiza kuwa karibu na Mungu na kuwa karibu na Mungu ni kuwa karibu na ulimwengu wa kiroho. Kwa maana nyingine anatutaka tupambane na chanzo cha tatizo kwa kumtanguliza Mungu badala ya kupambana na matokeo ya tatizo kwa kuutanguliza mwili kupokea chanjo.
 
Ukiwa mwenyewe kwa manufaa yako ruksa kufuata chochote kile unachopenda / Amini (After All ni Maisha yako).

Ikiwa umepewa dhamana ya maisha ya wengi, pia wengine wasio na Imani kama wewe.., basi ni busara wewe kwenda na Imani yako (kila mtu na Imani yake) ila ni lazima zaidi kufuata ushauri/ matakwa ya wataalamu (ambao kazi yao usiku na mchana ni kushughulikia hilo jambo).

Inawezekana kabisa wewe ukaamini ukinywa sumu utapona, lakini kuwaambia wengine pia wanywe sumu..., huko ni kutokuwa responsible...., (Cha maana ni kuwaambia kaa mbali na sumu).
 
Mh mleta mada,nina jambo langu.unaweza kuwa sahihi lakini shida kuwaaminisha walimwengu kuhusu ulimwengu wa roho tatizo ndio linaanzia hapo.

Embu tafsiri kwanza ulimwengu wa roho ni ulimwengu wa namna gani?, hata hao wanadini sio mar moja au mbili wamesikika wakisema "nilipokuwa kwenye ulimwengu wa roho" pasipo kufafanua huo ni ulimwengu wa aina gani
 
Mh mleta mada,nina jambo langu.unaweza kuwa sahihi lakini shida kuwaaminisha walimwengu kuhusu ulimwengu wa roho tatizo ndio linaanzia hapo.Embu tafsiri kwanza ulimwengu wa roho ni ulimwengu wa namna gani?, hata hao wanadini sio mar moja au mbili wamesikika wakisema "nilipokuwa kwenye ulimwengu wa roho" pasipo kufafanua huo ni ulimwengu wa aina gani
Ulimwengu wa roho ni umilele usiotawaliwa na mipaka ya muda na mahali ambao ni chanzo cha kila kitu katika ulimwengu wa vitu.
 
Ushahidi halisi kuwa ulimwengu wa roho upo ni kwamba sisi wanadamu tuna roho na roho ndiyo kila kitu kwetu miili yetu ni kibebeo cha roho.
 
Ukiwa mwenyewe kwa manufaa yako ruksa kufuata chochote kile unachopenda / Amini (After All ni Maisha yako)...
.
Mkuu inahitaji kuelewa zaidi ya uelewa unapokomea ili kutambua ulimwengu wa roho...lugha ya Kiswahili imetumia neno tafakari ila Kiingereza wanatumia neno "imagination"...huenda unaweza ukaelewa kiasi.
 
Mkuu inahitaji kuelewa zaidi ya uelewa unapokomea ili kutambua ulimwengu wa roho...lugha ya Kiswahili imetumia neno tafakari ila Kiingereza wanatumia neno "imagination"...huenda unaweza ukaelewa kiasi.
Mkuu jambo unalokosea ni kwamba sio kila mtu anatambua ulimwengu wa roho, kwahiyo kwenye kadamnasi ya watu wenye imani tofauti na utambuzi tofauti sio mbaya kila mtu kuwa na utambuzi wake individually, lakini linapokuja suala ya collectiveness inabidi twende na collective practical tested ways and means (hususan kama wewe ni kiongozi wa hao majority), especially kama hio miongozo haipingani na imani yako (hata kama inapingana binafsi ni bora kukumbuka kwamba position yako sio ya kiimani / kiroho)
 
UPUUZI MTUPU! Uongo wake kuhusu kutokuwepo corona nchini na kuzisagia barakoa ni chanzo kikubwa cha ongezeko la maambukizi na vifo vya kutisha.
 
Amekuwa akisema ugonjwa huu ni vita ya kiuchumi mara kadhaa huenda tunaweza tukachelewa sana kuelewa kama tunaishia kuangalia kwa kutumia macho ya nyama na kusahau kuangalia kiroho.
Mkuu naomba kwa lugha rahisi kabisa elezea ni kwa namna gani ugonjwa wa Corona ni vita ya kiuchumi kwa Tanzania wakati huo ugonjwa upo Duniani kote?
 
UPUUZI MTUPU! Uongo wake kuhusu kutokuwepo corona nchini na kuzisagia barakoa ni chanzo kikubwa cha ongezeko la maambukizi na vifo vya kutisha.
Mkuu hujaelewa jambo hapo Korona ni vita ya kiroho na siyo ya kimwili....tunaanzia kwenye formless kuja kwenye form.
Na pili Rais hajasagia barakoa ila ametutaka kuwa na tahadhari kubwa kwani siyo kila barakoa ni salama.
Mbona ameshauri kutumia za hapa Nchini (MSD) na za kujishonea?..
Kama angekuwa na nia ya kusagia kama ulivyodai unafikiri ameshauri juu ya hizo nyingine?
 
Mkuu jambo unalokosea ni kwamba sio kila mtu anatambua ulimwengu wa roho..., kwahiyo kwenye kadamnasi ya watu wenye imani tofauti na utambuzi tofauti sio mbaya kila mtu kuwa na utambuzi wake individually..., lakini linapokuja suala ya collectiveness inabidi twende na collective practical tested ways and means (hususan kama wewe ni kiongozi wa hao majority)..., especially kama hio miongozo haipingani na imani yako (hata kama inapingana binafsi ni bora kukumbuka kwamba position yako sio ya kiimani / kiroho)
Ndiyo maana nimetoka tujitambue kuwa sisi sote na wewe ikiwemo ni viumbe wa kiroho tunaoishi katika mwili.
Lengo ni kutaka kuliweka suala la kiroho nje ya mipaka tuliyoizoea
 
Back
Top Bottom