Ujasiri wa Kifisadi: Vijana na Wazee nani Zaidi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujasiri wa Kifisadi: Vijana na Wazee nani Zaidi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Companero, Nov 25, 2009.

 1. Companero

  Companero Platinum Member

  #1
  Nov 25, 2009
  Joined: Jul 12, 2008
  Messages: 5,475
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Nawaandikia ninyi vijana, alinena mwandishi maarufu, kwa kuwa mna nguvu na mmemshinda yule mwovu. Ufurahieni ujana wenu, akasisitiza mwandishi mwingine mahiri, kabla hazijaja siku zilizo mbaya, yaani siku za uzee, mtakaposema hamna furaha katika hizo. Maandiko haya yanaonesha ni jinsi gani vijana walivyo na nafasi kubwa katika maisha na jamii kwa ujumla. Pengine ndio maana Mheshimiwa Mkuu Muungwana ametamka kuwa katika Baraza lake lijalo la Mawaziri, kama atajaliwa tena na Jalia kutinga Ikulu, basi litakuwa na sura za vijana zaidi.

  Sasa swali la msingi la kujiuliza ni: Je, vijana hao watakaopewa mamlaka hayo wana nguvu? Na, je, wamemshinda yule mwovu, yaani, ufisadi? Ili kulijibu hili swali ni vyema kulinganisha vijana waliopo sasa madarakani na wazee ili kuonana dalili za kupata viongozi vijana wenye nguvu na ujasiri wa kupambana na ufisadi nafsini mwao na nchini kwao. Mada pacha ya 'Uchumi wa Kifisadi: Injini inayoendesha Nchi' inatoa mwanga wa jinsi ambavyo ufisadi haujali ujana, utoto wala uzee hapa nchini Tanzania. Sasa, je, vijana wataleta tofauti gani hapo 2011?
   
 2. B

  Boramaisha JF-Expert Member

  #2
  Nov 25, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 820
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Lengo lilikuwa kufurahisha vijana. Bado ile kauli mbiu ya "maisha bora kwa kila Mtanzania" imo kwenye kumbukumbu zetu na hatujayaona hayo maisha bora. Tusidanganyike kuhusu kauli ya uongozi kwa vijana. Kauli za reja reja kwa masuala ya msingi hazifai. Twaambiwa vijana watateuliwa kuwa viongozi je imefanywa tathmini kujua iwapo kuna vijana wa kutosha wanaoweza kulisukuma hilo gurudumu kwa manufaa ya Taifa. Vijana wa leo naona wanawaza kujiendeleza wao wenyewe binafsi - kupata fedha waweze kujenga makasiri kabla hawajazeeka na kununua magari watuongezee idadi ya magari barabarani. Vijana wepi na wangapi wanaowaza kuendeleza nchi yao?

  Saed Kubenea kamaliza kila kitu katika article yake kwenye Mwanahalisi la leo kuhusu kauli aliyoitoa Muungwana.
   
 3. Scientist

  Scientist JF-Expert Member

  #3
  Nov 25, 2009
  Joined: Feb 7, 2009
  Messages: 392
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Muungwana keshashtukiwa, kwa sasa aje na gia nyingine!
   
 4. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #4
  Nov 25, 2009
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,321
  Likes Received: 1,787
  Trophy Points: 280
  Hao vijana anaowaongelea atawatolea wapi? UVCCM! Maana kuna opportunist kibao, matunda ya ufisadi wanasubiri nafasi tu tuje kuwasikia. Kama hiyo ndio approach, bado sio dawa ya tatizo. Lazima kuwe na namna inayofaa kuwaandaa watu kuwa viongozi wa kesho. Kigezo kisiwe ni kimbelele cha mtu bali ni uwezo wake katika kuongoza
   
 5. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #5
  Nov 25, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Janja ile ile ya mwaka 47, eti JK ni kijana ........
   
Loading...