Ujanja ujanja wako JK unapata aibu, ona sasa haya mambo

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
JK baada ya kudhani kumleta mzungu wa Canada itakuwa msada kwake kurudisha hadhi yake miongoni mwa Watanzania sasa haya yameibuka .Hebu semeni JK alifikiria nini kumleta huyu mzungu ghafla hivi ?

Wabunge Canada wahoji ziara ya Waziri Mkuu wao nchini Tanzania

Na Mwandishi Wetu

ZIARA ya Waziri Mkuu wa Canada Stephen Harper nchini, imeibua mambo mapya, baada ya baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali ya nchi yake, kupinga kukutana na uongozi wa Kampuni ya Madini ya Barrick katika kikao cha faragha.

Kabla ya kumaliza ziara yake, Harper alikuwa na kikao cha siri kilichoandaliwa na Ubalozi wa Canada nchini na kudumu kwa dakika 45, kuzungumza na makampuni ya Canada ikiwemo ya Barrick.

Paul Dewar, Mbunge wa Jimbo la Ottawa ya Kati (NDP), alisema Harper alipaswa kukutana na watu walioathirika na uamuzi wa kampuni hiyo kuwafukuza kazi baadhi ya wafanyakazi wake na kujua hatma yao.

"Kampuni ya Barrick imesababisha mtafaruku kwenye jamii ya Watanzania, Waziri Mkuu alitakiwa akutane moja kwa moja na watu walioathirika na maamuzi ya Barrick kuwafukuza wafanyakazi wake wasio na chombo cha kuwatetea badala ya kukutana na uongozi wa kampuni," alisema Dewar ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje, katika mahojiano na Gazeti la Toronto Star juzi, na kuongeza;

"Alipaswa kuangalia mazingira halisi ya kampuni hii kushindwa kujali usalama wa wafanyakazi hao."

Vilevile, Joan Kuyek Mratibu wa Kitaifa wa Kikundi kinachofuatialia taratibu za uchimbaji madini kwenye migodi cha MiningWatch, alisema kitendo cha Kampuni ya Barrack kutojali maslahi ya wafanyakazi wake katika nchi za Chile na Tanzania, kinakiuka taratibu za kimataifa za uchimbaji madini.

Alisema nchini Chile, Kampuni hiyo imekuwa ikilalamikiwa kwa uharibifu wa mazingira na kutojali usalama wa wafanyakazi wake, mambo ambayo pia yamekuwa yakilalamikiwa Tanzania.

"Kama Waziri Mkuu Harper amekutana na wawakilishi kutoka Barrick pekee na hakukutana na wachimbaji wadogo, wala watu wanaoshughulikia athari za kijamii, kiuchumi na kimazingira kwenye maeneo ya migodi nchini Tanzania, wala wawakilishi wao, hii inashtua sana!" alisema Kuyek.
 
Shinikizo lipelekwe huko huko kwa Canadians maana sisi tukisema wanasema hatuna hoja.
 
hivi hawa viongozi wetu sijui wanafanya kazi kwa maslahi ya nani? angalia rada,aliyefanya uchunguzi na kupiga kelele ni mwingereza na katupatia full report tuweze kushtaki hao wahalifu lakini kilichotokea ni comedy tuu,tunaibiwa madini wanaotutetea ni hao hao canadians lakini vilaza JK na Karamagi na wabunge mbumbumbu bila kumsahau kada mpinzani wanasisitiza mikataba ni safi...dawa ni kuwanyima kula tuu la sivyo hii itaendelea kuwa order of the day!
 
Mimi nakwambia kuna mtu atafukuzwa kazi karibuni huko ikulu.

Washauri wa Kikwete wote wameoza, hakuna mtu wa kumshauri vyema.
Mimi naanza kupiga kampeni, FMES apewe nafasi kuwa mshauri mkuu wa raisi maana naona wengine hawa wote wachemfu.
 
hii hali inatisha
inabidi sasa tufike mahala hizi hoja zetu humu ziwe compiled halafu zichapishwe ktk kijarida mara nne kwa mwaka ili kuwafikia watanzania wengi zaidi.
hali ya kuwa kilaza huku una dhamana inatisha. mbona mawaziri wa nyerere hawakusoma wengi ila walikuwa na misimamo??
 
Hizo ni politics za ndani za Canada na wala hata siku moja haziwezi kutusaidia sisi.

Anayejua watu wa West, wa kwanza kujifanya wanatetea wanyonge lakini hakuna hatua wanazochukua zaidi ya kuzomeana bungeni.

Mcanada anajali maslahi ya nchi yake, mambo ya Watanzania ni ya JK na sisi watu wake.

Haya mengine ni usanii tu ndani ya mabunge ya West.
 
Hizo ni politics za ndani za Canada na wala hata siku moja haziwezi kutusaidia sisi.

Anayejua watu wa West, wa kwanza kujifanya wanatetea wanyonge lakini hakuna hatua wanazochukua zaidi ya kuzomeana bungeni.

Mcanada anajali maslahi ya nchi yake, mambo ya Watanzania ni ya JK na sisi watu wake.

Haya mengine ni usanii tu ndani ya mabunge ya West.

...bora hao unaowaita wasanii lakini wanasema ukweli na wanasema waziwazi tumepewa bad deal,vipi na wale ambao mtu akipiga chafya kuwa hii ni bad deal basi na bungeni anafukuzwa au kufukuzwa kazi,tusitake misaada mikubwa sana hata huo wa kelele unasaidia
 
Mtanzania nini kifanyike kaka?
Nchi za magharibi zinajali maslahi yao, lakini zinaweka mbele sana kufanya kazi under ethics amblella. Nadhani Canadian people needs to know the brutality of their corporation.

Hii ni kumuumbua JK amabaye amesema kwamba hatuna matatizo na Barrick lakini tunataka win win situation.
 
Back
Top Bottom