Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,898
JK baada ya kudhani kumleta mzungu wa Canada itakuwa msada kwake kurudisha hadhi yake miongoni mwa Watanzania sasa haya yameibuka .Hebu semeni JK alifikiria nini kumleta huyu mzungu ghafla hivi ?
Wabunge Canada wahoji ziara ya Waziri Mkuu wao nchini Tanzania
Na Mwandishi Wetu
ZIARA ya Waziri Mkuu wa Canada Stephen Harper nchini, imeibua mambo mapya, baada ya baadhi ya wabunge na viongozi wa serikali ya nchi yake, kupinga kukutana na uongozi wa Kampuni ya Madini ya Barrick katika kikao cha faragha.
Kabla ya kumaliza ziara yake, Harper alikuwa na kikao cha siri kilichoandaliwa na Ubalozi wa Canada nchini na kudumu kwa dakika 45, kuzungumza na makampuni ya Canada ikiwemo ya Barrick.
Paul Dewar, Mbunge wa Jimbo la Ottawa ya Kati (NDP), alisema Harper alipaswa kukutana na watu walioathirika na uamuzi wa kampuni hiyo kuwafukuza kazi baadhi ya wafanyakazi wake na kujua hatma yao.
"Kampuni ya Barrick imesababisha mtafaruku kwenye jamii ya Watanzania, Waziri Mkuu alitakiwa akutane moja kwa moja na watu walioathirika na maamuzi ya Barrick kuwafukuza wafanyakazi wake wasio na chombo cha kuwatetea badala ya kukutana na uongozi wa kampuni," alisema Dewar ambaye pia ni Waziri Kivuli wa Mambo ya Nje, katika mahojiano na Gazeti la Toronto Star juzi, na kuongeza;
"Alipaswa kuangalia mazingira halisi ya kampuni hii kushindwa kujali usalama wa wafanyakazi hao."
Vilevile, Joan Kuyek Mratibu wa Kitaifa wa Kikundi kinachofuatialia taratibu za uchimbaji madini kwenye migodi cha MiningWatch, alisema kitendo cha Kampuni ya Barrack kutojali maslahi ya wafanyakazi wake katika nchi za Chile na Tanzania, kinakiuka taratibu za kimataifa za uchimbaji madini.
Alisema nchini Chile, Kampuni hiyo imekuwa ikilalamikiwa kwa uharibifu wa mazingira na kutojali usalama wa wafanyakazi wake, mambo ambayo pia yamekuwa yakilalamikiwa Tanzania.
"Kama Waziri Mkuu Harper amekutana na wawakilishi kutoka Barrick pekee na hakukutana na wachimbaji wadogo, wala watu wanaoshughulikia athari za kijamii, kiuchumi na kimazingira kwenye maeneo ya migodi nchini Tanzania, wala wawakilishi wao, hii inashtua sana!" alisema Kuyek.