Ujangili na Biashara zisizoeleweka: Ni nani huyu - Mohsin Abdallah(Sheni)?

Jana Nilikutana na mzee mmoja mstaafu wa maliasili katika mazungumzo yetu Alinipa uzoufu wake wa miaka mingi maliasili kama askari ,pia alinipa assignment na maswali mengi ambayo yaliniacha na ???? Alitumia maneno kama "serikali kujikoshaa" mfano issue za kontena ya meno ya tembo.Alitolea mfano mchina anaweza kuja akitokea asia kuwinda Ndovu bila mkono wa serikali?? kibaya zaidi kwa huyu mzee wetu mstaafu wanyama pori hakujipanga, mzee huyu hivi sasa anatafuta kibarua katika kampuni binafsi za ulinzi (security guard). pamoja naku zeeka sana anataman apangiwe lindo la silaha ashike bunduki ili mshaara wake uwe mkubwa kidogo kweny kampuni ya ulinzi wamekua wakikatalia kutokana na uzee wake.
 
Nasubiri kuona matundu yanavyotema misamaha ya kodi... nasubiri kuona vilio vya waliozoea kukinga mikono ili wapewe chochote na makada wenzao wenye sifa za ufilisi rasilimali za nchi. bado nasubiri kuona wanavyojikinga na mabua kana kwamba si wao waliowapongeza na kuwaficha wahujumu hao. Bado nasubiri kuona wanavyoapizana na kujilaani, bado nasubiri kuona wanavyolipasua kwa mikono yao jahazi ambalo wakitamba nalo!!! yani bado... bado... bado...
 
Ukiona Mkulu kagusa kila sehemu lakini kwenye ujangili hajagusa ujue kuna namna....wacha ninyamaze nisije kupimwa mkojo wa uchochezi
 
Nchi yoyote ile ambayo haina mfumo wa ufuatiliaji uhalali wa vipato vya watu wake, ni dhahiri kwamba watu waovu watatumia mwanya huo kuhujumu nchi kupindukia na hivyo kuwa na ukwasi wa kutisha ambao kwa namna moja au nyingine, kinamna, huutakasa na hivyo kuonekana ni utajiri halali!
Inawezekanaje kwa mfano mtumishi wa umma anakuwa na maghorofa au magari zaidi ya mahitaji yake lakini pia zaidi ya kipato chake na kunakuwa hakuna wa kuhoji? Inakuwaje, kwa mfano mfanya biashara mchanga kwa usiku mmoja anakuwa na ukwasi wa kupindukia bila hata ya kufuatilia mtiririko wa kipato chake kwa uwazi?
Aina hii ya ukosefu wa mfumo wa kutumia takwimu sahihi juu ya aina ya njia kuu za vipato vya wananchi, wigo wa ajira, aina ya raslimali zilizopo na namna zinavyotumiwa katika kuboresha maisha ya wananchi, mfumo wa uzalishaji na masoko, nk , hupelekea watu wengine kutajirika kwa njia haramu na wakati mwingine hata kuua wengine na kuwanyanga'nya mali zao! Nani atawauliza?
Ni wakati mwafaka kuweka utaratibu wa wazi wa vipato vya kila mwananchi na mtiririko wake badala ya kufanya hivyo kwa viongozi tu. Kwani inapokuwa kwa viongozi tu, huo unakuwa mwanya mwingine kwa viongozi hao hao kutumia jamaa au ndugu zao kuficha walichouibia umma / serikali au pesa haramu kutokana na rushwa!
Tijitafakari!
Massanda, unachaosema ni sahai na kinachohitajika kama nilivyosema ni utashi wa viongozi au kiongozi wetu, and inthis context, Raisi wetu Dr. Magufuli au kama ilivyokuwa wakati wa Mwalimu Nyerere na Kamanda wake Marehemu Sokoine. Tuliokuwapo nakuona utashi wao katika kupambana na wezi wa mali ya umma, tunajua hakuna kinachoshindikana kwa dola, kama ikitaka kuisaidia nchi. Lakini kama kila mtu, kila kiongozi, kila raia na kila mgeni anajitahidi kuiibia nchi na kuuibia umma na viongozi wanatizama tu, HAKEMEI, kwa sababu wao pia ni part and parcel of that LOOTING system, lazima kutakuwa na shida. Lakini kama kuna viongozi wanaokemea na kuzuia na kujitenga na hii LOOTING na wananchi wakielezwa na kuelwa somo na kuona kile kinachookolewa kinawarudia kwa njia moja au nyingine in the form of social services and amenities then vita inakuwa rahisi kwani ina nguvu ya UMMA nyuma yake. Katika hali hii, USHINDI ni DHAHIRI.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom