Ujangili na Biashara zisizoeleweka: Ni nani huyu - Mohsin Abdallah(Sheni)?

juspen

Member
Dec 20, 2012
24
10
UPDATES:

Novemba 2014, Gazeti la Economist limeandika haya https://www.economist.com/news/midd...-and-poachers-merit-further-investigation-big

IMG_2662.jpg


Aidha, vema kusoma Ujangili na Biashara zisizoeleweka: Ni nani huyu - Mohsin Abdallah(Sheni)?

Wanabodi ebu tusaidiane background au CV kama inawezekana, au picha basi ili kumfahamu huyu Kada Mohsin Abdallah ambae alitajwa ktk report ya Wanaintelejensia wa Kimataifa ktk report yao kuwa ni namba moja kwa kazi za Ujangili na inaonekana Serikali yetu kaishika( kaiweka ktk pocket) na ndio maana hatua hazijajukuliwa juu yake.

Lakini pia napenda kufahamu background ili angalau kunisaidia na jamii kwa jumla kwa sababu kuna usemi wa kiswahili unasema (Mtoto wa nyoka nae ni nyoka au kuna mwingine unasema Jasili aachi asili) sasa unaweza kukuta ni mtu mwenye matukio kama hayo toka akiwa mtoto ili tusiendelee kushangaa kwa nini, huyu anafanya hivi?itasaidia tutajua hakukujwa angali mbichi, tukilazimisha sasa hivi lazima tumvunje!

Cha mwisho hawa ni watu ambao tupo nao sana mtaani na ktk shughuli mbalimbalia za kijamii au biashara,unawezakuta mnapatiwa michango ya kujenga nyumba ya ibada au Shule na mkapokea alafu baada ya kumaliza ile nyumba ya Ibada au Shule pazuka migogoro mingi na vita vya waumini kwa waumini au watoto wanafeli hovyo au watoto washule wanaingia ktk ujambazi,uvutaji bangi au dawa na udokozi na vitendo viovu tukadhani hawafundishwi kumbe hata pesa tuliyopata kwa ajili ya kujenga na kununua vitabu ni laana tupu kutoka kwa Jangili fulani au Fisadi fulani kwa hiyo zile dhambi zinaturudi sisi au watoto wetu wasikuwa na hatia.

Kwa hiyo ni vizuri kumfahamu sura ili kama kuna kitu tunapata kwake tunakitakasa kwanza na ndipo tunaendele nacho.

Namaliza kwa kuomba Mwana JF yeyote anayemfahamu huyu mtu atuanikie hapa jamvini usiogope! "Dhambi kubwa kuliko zote ni Uoga" Godbless Lema

Nawasilisha!

=======

Mjue Kada wa CCM Mohsin Abdallah

Imeandikwa na Mwandishi Maalum, Dodoma

Jumanne, Agosti 07, 2012

*Tume ya Jaji Warioba ilianika madudu yake
*Ni bilionea anayehodhi vitalu vya uwindaji

Hivi karibuni, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee (Chadema) aliuibua bungeni mkataba ulioingiwa baina ya kampuni za Uranium Resources PLC, Western Metals Limited na Game Frontiers of Tanzania Limited uliotengenezwa na Kampuni ya Kitanzania ya Rex Attorneys, na kusainiwa Machi 23, 2007.Mkataba husika ambao vipengele vyake vinaainisha kwamba unatakiwa uwe wa siri, unaihusu kampuni ya uwindaji wa kitalii ya Game Frontiers of Tanzania Limited inayomilikiwa na Mohsin M. Abdallah na ndugu Nargis M. Abdallah." Mohsin Abdallah ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM na mmoja wa wafadhili wakubwa wa chama hicho. Pia ni Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Wamiliki wa Kampuni za Uwindaji wa Kitalii Tanzania (TAHOA). Mtu huyu ameshutumiwa kwa ukwepaji kodi na 'kuwanunua viongozi' wa kisiasa na wa vyombo vya dola.

Mwaka 1996 Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, aliunda Tume ya Kuchunguza Kero ya Rushwa nchini. Tume hiyo iliyokuwa na wajumbe kenda, iliongozwa na Waziri Mkuu mstaafu Jaji Joseph Sinde Warioba.

Katika ripoti hiyo, Mohsin, pamoja na washirika wake walituhumiwa kwa mambo mbalimbali. Gazeti la JAMHURI limeona ni vema likawakumbusha wasomaji ili waweze kumjue vema kada huyu wa CCM mwenyhe ukwasi wa kutisha. Ifuatayo ni sehemu ya ripoti hiyo ililiyomhusu Mohsin na wenzake - neno kwa neno: Hill Top Hotel and Tours Ltd inayomilikiwa na Mohsin Abdallah na Hitesh P. Arjun ilipewa Certificate of Approval Enterprise na Kituo cha Uwekezaji Rasilimali tarehe 3/1/1991.

Baadaye watu hao walianzisha kampuni ya Kigoma Hill Top Hotel iliyosajiliwa tarehe 2/4/1992 na ambayo ilirithi Certificate of Approval Enterprise iliyokuwa imetolewa kwa kampuni ya Kigoma Hill Top Hotel and Tours kuendeleza ujenzi wa Hoteli ya Kitalii ya Kigoma. Kampuni hii mpya inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Hitesh Arjun na Deusidedit Kisisiwe. Wamiliki hawa pia wanamiliki makampuni mengine ama kwa pamoja au mmoja kama ifuatavyo

(i) SHENIS COMMERCIAL LTD inayoshughulika na mauzo ya nguo, vitambaa na vipuri vya magari na mashine inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Mrs Nargis Mohsin Abdallah na Deusdedit Kisisiwe. Kampuni hii ilisajiliwa tarehe 27/7/1988.
(ii) TILE ANDA TUBE LTD iliyosajiliwa tarehe 7/12/1992 inashughulikia na biashara ya vifaa vya ujenzi, umeme, pombe na dawa na inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Deusdedit Kisisiwe na Tariq Mirza.
(iii) FIVE WAYS CLEARING AND FORWARDING AGENCY iliyosajiliwa tarehe 23/10/1992 kwa ajili ya kuondoa mizigo bandarini na usafirishaji wa abiria na mizigo kwa njia mbalimbali, biashara ya vipuri na vifaa vya ujenzi, uchimbaji na uuzaji wa madini nchi za nje inamilikiwa na Triphon Maji na Deusdedit Kisisiwe.
(iv) ROYAL FRONTIER (T) LTD iliyosajiliwa tarehe 7/3/1994 kwa ajili ya uwindaji wa kitalii na usafirishaji wa watalii, inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Deusdedit Kisisiwe na Rashid Omar.
(v) GAME FRONTIER (T) LTD nee MNM Hunting Safaris Ltd, inafanya shughuli zinazofanana na zile za Royal Frontier na inamilikiwa na Mohsin Abdallah, Mr. Abdikadir Mohamed na Mr. Ahmad Muhidin. Shenis Commercial Ltd ndiyo kampuni ya kwanza kisha ikafuatiliwa na Kigoma Hill Top. Baadaye makampuni mengine yaliibuka haraka haraka, jambo linaloashiria kwamba yalitokana na Kigoma Hill Top na yanafanya shughuli zake kwa kushirikiana. Vifaa vilivyoagizwa na Kigoma Hill Top na kusamehewa kodi ni vingi kuliko mahitaji ya hoteli.

Kwa mfano, kampuni iliagiza vigae vya sakafu 27,248, containers 3 za marumaru zenye ujazo wa mita za mraba 3264.8, magodoro 120 na taulo 4,00 wakati hoteli ina vitanda 60 tu. Aidha, iliruhusiwa kuagiza boti tatu na injini nne (outboard engines) na kufanya Hoteli hiyo kuwa na boti 7.

Idadi hii ya boti ambazo imeelezwa kwamba zitatumika kwa uvuvi wa kitalii ni nyingi sana ikilinganishwa na idadi ya vyumba vya hoteli hiyo na inawezekana zitatumiwa kwa shughuli nyingine. Vifaa vya ziada inaaminiwa viliuzwa na makampuni mengine yanayomilikiwa na wakurugenzi wa Kigoma Hill Top Hotel. Taarifa ya IPC inaonyesha kwamba ingawa kampuni ya Kigoma Hill Top Hotel ilipatiwa misamaha ya kodi, IPC haikuona na haikupendekeza aina ya vifaa vya ujenzi wa Kigoma Hill Top Hotel vinavyotakiwa kusamehewa kodi.

Wakurugenzi wa kampuni walikuwa wanawasiliana na Hazina moja kwa moja kuanzia mwaka 1991 hadi Julai 1995 walipoanza kupitisha maombi ya misamaha hiyo IPC. Hata hivyo, baadhi ya vifaa ambavyo vilisamehewa kodi na Hazina havikustahili kusamehewa kodi. Kwa mfano, kampuni ilisamehewa kodi magari Na. TZF 5059 Toyota S/Wagon, TZF 8455 Toyota L/Cruiser, TZF 8612 Land Cruiser S/Wagon na TZF 6001 ambalo ni gari ya kifahari aina ya magari ya Mercedes Benz Sportscar, na ndege moja.

Ijapokuwa magari na ndege hiyo vyote vilisamehewa kodi chini ya mradi wa Kigoma Hill Top yamekuwa yanatumika na kampuni zao nyingine hapa Dar es Salaam na Kigoma. Kwa mfano, gari TZF 8454 lililoandikishwa tarehe 16/6/1994 kama mali ya Kigoma Hill Top, chini ya Import Declaration, mwagizaji alikuwa Royal Frontiers na Import Entries zilionyesha Kigoma Hill Top. Kampuni hii ilikuwa iagize ndege mwaka 1995 na ikasamehewa kodi kwa barua Kumb. Na TYC/1/150/9/176/7. Uchunguzi umeonyesha kwamba hakuna ndege iliyosajiliwa hapa nchini kwa jina la kampuni hiyo, lakini kampuni ya Game Frontiers ina ndege yenye namba za usajili 5H-GFT (Cesna 206) iliyosajiliwa mwaka 1995.

Uchunguzi pia unaonyesha kwamba kampuni ya Kigoma Hill Top Hotel inatumia sana ndege hiyo kwa kuwapeleka watalii na wageni huko Kigoma Hill Top Hotel ingawa haina leseni ya biashara ya usafiri wa anga. Tume imezungumza na mmoja wa wamiliki wa kampuni ya Kigoma Hill Top, Deusdedit Kisisiwe, lakini maelezo aliyoyatoa kuhusu tuhuma hizo hayakuridhisha.

Tume inaamini kwamba:
(i) Bwana Mohsin Abdallah na wenzake, hasa Deusdedit Kisisiwe wamefungua kampuni nyingi za biashara na kuomba misamaha ya kodi kwa kampuni moja ya Kigoma Hill Top Hotel. Kampuni imeagiza vitu vingi vilivyosamehewa kodi na kuvitumia au kuviuza kupitia makampuni yao mengine ambayo hayakupata misamaha ya kodi.

(ii)Wafanyabiashara hawa wamekuwa wanawatumia viongozi wa Serikali katika kuficha maovu yake. Kwa mfano, Kampuni ya Fiveways Clearing and Forwarding Agency ilimpa hisa Bw. Tryphon Maji aliyekuwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dar es Salaam na hivyo alikuwa habughudhiwi na polisi anapofanya vitendo kinyume cha kanuni na taratibu.

Katika makampuni ya Royal Frontier (T) Ltd hisa zimetolewa kwa ndugu wa aliyekuwa Waziri wa Maliasili, Utalii na Mazingira Bw. Juma Hamad Omar na katika kampuni ya Game Frontiers (T) Ltd hisa zimetolewa kwa Ahmed Muhidin ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mkurugenzi wa Wanyamapori Bw. Muhidin Ndolanga. Hisa hizi zimetolewa kwa wakubwa hawa kama kivuli (cover) ili waweze kuyapatia makampuni haya vitalu vya uwindaji pamoja na kurahisisha shughuli za uwindaji.

(iii) Bw. Mohsin Abdallah na Kisisiwe wanapenda kuwatumia viongozi kama chambo katika biashara zao, ili waweze kuvuka kikwazo chochote kile kitakachokwamisha biashara zao.
 
Huyu ni mfanyabiashara mkubwa mjini Kigoma. Ana hotel ya kitalii inaitwa Kigoma Hill Top Hotel, na kampuni ya kusafirisha watalii kwenye mbuga za Gombe na Mahale.

Huyu zamani alikuwa na Garage ya kukarabati magari kule Ujiji, Sheni Auto Garage, ambayo aliifunga baada ya kuanza kujenga Hill Top Hotel. Ni rafiki mkubwa wa viongozi wakubwa wa Serikali tangu enzi za Mzee Ruksa.

Huyu ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Mkoa wa Kigoma, na mfadhili mkubwa sana wa CCM.

Watu wa Kigoma wanazungumza sana kuwa yeye ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya na pia ni mtumiaji wa bidhaa hiyo.
 
Huyu ni mfanyabiashara mkubwa mjini Kigoma. Ana hotel ya kitalii inaitwa Kigoma Hill Top Hotel, na kampuni ya kusafirisha watalii kwenye mbuga za Gombe na Mahale.

Huyu zamani alikuwa na Garage ya kukarabati magari kule Ujiji, Shein Auto Garage, ambayo aliifunga baada ya kuanza kujenga Hill Top Hotel. Ni rafiki mkubwa wa viongozi wakubwa wa Serikali tangu enzi za Mzee Ruksa.

Huyu ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Mkoa wa Kigoma, na mfadhili mkubwa sana wa CCM.

Watu wa Kigoma wanahisi kuwa yeye ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya na pia ni mtumiaji wa bidhaa hiyo.

mmmh! Kweli ukianza kusikiliza umbea na majungu utakufa kwa presha?
 
E bana e Mkuu Mchami, asante mno a thousand times!!!!!!!!
A BIG RED FLAG far beyond your ordinary imagination.


Huyu ni mfanyabiashara mkubwa mjini Kigoma. Ana hotel ya kitalii inaitwa Kigoma Hill Top Hotel, na kampuni ya kusafirisha watalii kwenye mbuga za Gombe na Mahale.

Huyu zamani alikuwa na Garage ya kukarabati magari kule Ujiji, Shein Auto Garage, ambayo aliifunga baada ya kuanza kujenga Hill Top Hotel. Ni rafiki mkubwa wa viongozi wakubwa wa Serikali tangu enzi za Mzee Ruksa.

Huyu ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM kutoka Mkoa wa Kigoma, na mfadhili mkubwa sana wa CCM.

Watu wa Kigoma wanahisi kuwa yeye ni mfanyabiashara wa madawa ya kulevya na pia ni mtumiaji wa bidhaa hiyo.
 
Risala fupi ya marehem CCM: Marehem CCM alizaliwa 05/02/1977.Enzi za uhai wake marehem alijishughulisha na kuua mazao ya biashara km pamba, tumbaku, kahawa, korosho na katan. Marehem pia atakumbukwa kwa kaz kubwa aliyoifanya kwa bidii ya kuua viwanda km Mwatex, Mutex, Kiltex, Ufi, Bora Tanelec, Mgololo, Tanganyika packers, viwanda vya maziwa.

Pia aliwaleta na kuwapa wagen mali za waTZ.Ameacha wachina kariakoo,waarabu loliondo,makaburu mererani na wazungu wa kila aina kwny migodi yote ya madini na gesi. Marehemu ameacha mke m1 aitwaye (CUF) na watoto wawili.

UDP na TLP. Shetani amuweke pabaya moton milele Amen.
 
Haya jibiringisheni then mkitaka mrukeruke, ila ukweli unabaki "muosha huosha"...kama ni jangili basi muda wake wa kujangiliwa utafika tu.
 
Aliyeshikana mkono na Mchuuzi wa rasilimali za Taifa anahusika. Ni mmiliki wa Zantas Air, ni mmiliki wa Hunting Companies kama tatu Hivi, ndiye aliyesub-lease illegally Hunting Block yake kwa Mantra Tanzania, kampuni iliyowekeza Mitambo ya kuvuna Uranium huko Namtumbo, kwenye hiyo illegal deal Serikali imekaa kimya na kumuachia huyo bwana apige $ 6m peke yake kwa niaba ya Watanzania. Zaidi ya hapo alikuwa Mwenyekiti wa Tanzania Hunters Association (TAHOA) for some years. Naomba nibakishe akiba ya maneno.

IMG_6363.JPG
 
Mwaka jana Halima Mdee aliwasilisha hii scandal inayomhusisha huyu jamaa, ina nadhan serikali iliamua kuitupilia mbali, tujage mwanawane...

The Opposition camp yesterday told the National Assembly about an alleged scam involving two uranium exploring companies and a hunting firm. They are said to have entered into a fraudulent contract apparently facilitating the subletting of the blocks contrary to the law and regulations.

This surfaced when the opposition tabled its "alternative budget estimates" Game Frontiers of Tanzania Limited, was alleged to have sub-leased Mbarang'andu village in Namtumbo benefiting some of USD6m payable in two phases. An additional 250,000 US dollars was set to be paid upon commencement of actual mining activities. Meanwhile, the local villagers are estimate to at best have had a mere s living in the surrounding villages 10,000 USD go into their meager financial capital circulation.

Shadow minister for Lands, Housing and Human Settlement Development, Halima Mdee named the exploration companies as, Uranium Resources PLC and Western Metals Limited. She also unveiled that the contract was done by a Tanzanian law firm, Rex Attorneys and signed on March, 23, 2007.

As a result of its presumed illegality, the confidential document is out for all to see and it names, Mohsin M. Abdallah and Nargis M. Abdallah as the owners of Game Frontiers of Tanzania Limited, the leasing party. "…another 55, 000 USD is to be paid annual, on every first of March to compensate the opportunity cost…" Mdee went on to unravel the scandal.

"I have gone through the Wildlife Conversation Act of 1974 and The Wildlife Conservation Act Number 5 of 2009. These acts allow a person with a hunting permit to only carry hunting activities and not otherwise…" she further explained.
She added that in accordance to the land laws of 1999 should a piece of land allocated for other purposes and then later be found to contain minerals then ownership returns to the government or the individual.
 
JK na mafisadi bwana hajambo sana
Hao ndio watu wanaoweza kumfichia mali zake, hivi kama huna kitu ukipewa bilion 5 tu c kila mtu atafahamu kwa jinsi utavyojawa na wenge la Terabyte za kutosha aisee?? Ma tycoon kama hao hawa hata wakipewa Trillion wamfichie wala huwezi kuwaona wana wenge. Masikini kipata fedha hana kifua, utajua tu. Nadhan ndo mana wahenga walisemaga maskini akipata kiboga hulia mbwata!!
 
mmmh! Kweli ukianza kusikiliza umbea na majungu utakufa kwa presha?

ok, kisa katajwa kada wa ccm, nyie watu wa ajabu sana. Mtu uyu mohsin abdala ni hatari kwa tembo hence future ya taifa letu anaiweka matatani,
lakini wendawazimu tokea ccm - lumumba ukiwemo wewe bado mnamtetea, nyie ni majuha pia mazumbukuku, haujali future ya watoto pia wajukuu wako unalojua ni kutetea wezi as long as wanatokea ccm. We fara sana
 
Aliyeshikana mkono na Mchuuzi wa rasilimali za Taifa anahusika. Ni mmiliki wa Zantas Air, ni mmiliki wa Hunting Companies kama tatu Hivi, ndiye aliyesub-lease illegally Hunting Block yake kwa Mantra Tanzania, kampuni iliyowekeza Mitambo ya kuvuna Uranium huko Namtumbo, kwenye hiyo illegal deal Serikali imekaa kimya na kumuachia huyo bwana apige $ 6m peke yake kwa niaba ya Watanzania. Zaidi ya hapo alikuwa Mwenyekiti wa Tanzania Hunters Association (TAHOA) for some years. Naomba nibakishe akiba ya maneno.

IMG_6363.JPG

YANI HAPA RAISI JK KWELI ANATUSALITI. ANASHIKANA MKONO NA UYU MTU AMBAYE NI HATARI KWA WATANZANIA. APA PRESIDAR HAJATUTENDEA HAKI WALAHi
 
Aliyeshikana mkono na Mchuuzi wa rasilimali za Taifa anahusika. Ni mmiliki wa Zantas Air, ni mmiliki wa Hunting Companies kama tatu Hivi, ndiye aliyesub-lease illegally Hunting Block yake kwa Mantra Tanzania, kampuni iliyowekeza Mitambo ya kuvuna Uranium huko Namtumbo, kwenye hiyo illegal deal Serikali imekaa kimya na kumuachia huyo bwana apige $ 6m peke yake kwa niaba ya Watanzania. Zaidi ya hapo alikuwa Mwenyekiti wa Tanzania Hunters Association (TAHOA) for some years. Naomba nibakishe akiba ya maneno.
IMG_6363.JPG
Mwaga vitu,
 
Back
Top Bottom