Ujambazi wa polisi liwe fundisho kwa Serikali ya Rais Samia

Si kweli mkuu. Mbona kule Kenya, Rwanda na Burundi hakuna mapolisi wenye njaa kali kama hawa waliotapakaa hapa nchini tanzania. Hawa wa hapa wamezidi, sio kwa njaa hizi wanazopora mali za raia na kisha kuwaua. Ni uhuni na ujambazi wa hali ya juu.
Mwambie Mbowe akupe nauli uvuke hata mpaka.Polisi wa Tanzania ni watakatifu kabisa kulinganisha na Kenya.
 
Baada ya vitendo vya kijambazi vinavyofanywa na polisi kushamiri katika siku za karibuni, sasa imefika wakati serikali ijithathmini namna ya kuwachuja polisi wanaofaa kuajiriwa. Madhara ya kung’ang’ania form four failures (Divison 4 & 0) ndiyo yametufikisha hapa tulipo. Sasa serikali ianze mara moja kuajiri wahitimu waliofaulu vizuri (Divisheni 1 & 2) ili kulinda heshima ya jeshi la polisi. Polisi wenye ufaulu mdogo wana kiwango kidogo cha kufikiri na pia wana upeo mdogo wa kudadavua mambo.

Na pia imeonyesha hawa polisi ambao ni form four failures, wana tamaa ya pesa na inawezekana wanatokea familia masikini jambo linalopelekea kuwa na mitindio ya ubongo ama kwa kukosa lishe nzuri au kulelewa malezi ya ajabuajabu. Mtu aliyelelewa vema akili zake hukuwa vema na huwaza vema. Polisi wa sasa hivi ni zaidi ya vichaa. Ukitazma matukio wanayofanya na sababu wanazotoa unaona kabisa kwamba wana hililafu fulani vichwani mwao. Polisi mwenye akili zilizotimia hawezi kuondoa uhai wa raia kwa sababu tu ya fedha.

Michezo hii ya polisi ilianza wakati ule wa akina Zombe walipompora mamilioni ya fedha mfanyabishara wa madini kutoka Morogoro na kisha kumuua. Laana ilianzia hapa. Kabla machozi hayajakauka, wamekuja tena kumuua mfanyabishara mwingine wa madini kutoka Mtwara. Inauma sana. Ina maana polisi hawataki watu wachimbe au wajihusishe na biashara ya madini katika nchi hii? Polisi wamekuwa kama fisi wenye njaa wanaomfuata mtu nyuma wakitamani mkono mmoja udondoke wafanye kitoweo. Lakini polisi wetu hawa wameenda mbali zaidi. Wanalazimisha kumuua mtu ili wachukue mikono wale kisha kukimbilia vichakani kujificha.

Pamoja na ujambazi wote huu unaofanywa na polisi, tangu kuuliwa kwa Daudi Mwasngosi hadi mfanyabishara wa madini wa Mtwara, siajwahi kusikia Waziri au kiongozi yeyote wa polisi au serikali akiwajibika kwa kujizuru. Tukumbuke miaka ya nyuma Rais Ally Hassan Mwinyi aliwahi kujiuzuru uwaziri baada ya polisi kuhusika kwenye uhalifu kama huu unaofanyika siku hizi. Natoa wito kwa Waziri wa Mambo ya ndani na IGP Sirro kujiuzuru nyadhifa zao mara moja ili kuonyesha uwajibikaji wao kwa haya matukio ya kijambazi yanayofaywa na polisi mchana kweupe.​
UJAMBAZI wa Polisi upo na Utaendelea kuwepo kwani KATIBA iliyopo unawapa Mwanya wa kufanya UJAMBAZI
Hakuna Chombo kinachowachunguza
Polisi wanategemewa na Chama tawala kuwavusha
Mfano ya Matukio ya kijambazi Chini ya Utawala huu ni pamoja
1.Lissu Kupigwa Risasi
2 Akwilina Kupigwa Risasi
3.Wasiojulikana
4 Azory kutekwa na kupotea
5.Ben saanane KUTEKWA na kuuawa
6.Roma kutekwa
7.Mo kutekwa
8.Suala la HAMZA
9.Mchimba Madini Mtwara
Matukio yote hayo yamefanyika AWAMU ya 5
Hakuna Waziri ALIYEJIUZULU
Wala IGP wapo WANAKULA MAISHA


Sent from my SM-J600F using JamiiForums mobile app
 
Unakuta ni Polisi Jambazi huyo anajatibu kitetea Majambazi wenzake kama anjaa si aache kazi akaolewe
Si ndo hapo hata mm namshangaa :oops: :oops: Yeye anaona mahali pana njaa lakini bado amepangangania. Amerogwa?
 
Mwambie Mbowe akupe nauli uvuke hata mpaka.Polisi wa Tanzania ni watakatifu kabisa kulinganisha na Kenya.
Hivi mkiwaua raia na kuwapora fedha zao mnanufaika sana eeh? Jehanamu inawahusu kwa dhuluma hii.
 
Hii ndiyo aina ya polisi tulio nao hapa nchini
 
Back
Top Bottom