Ujambazi wa polisi liwe fundisho kwa Serikali ya Rais Samia

Shida sio wasomi tena hao wasomi wenyewe ndio wanaoisumbua serikali maana kwa elimu zao anaona anachelewa kupata maendeleo akifikiria elimu yake.
Mbona zamani kulikuwa na wa elimu ndogo hadi la saba b lakini weledi ulikuwepo? Tatizo hapo ni tamaa ya mali haraka haraka ebu wapewe mshahara wa kutosha uone kama kazi haijafanywa vizuri hata na rushwa yaweza pungua.
Ni bora wawe polisi wachache posho kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwani zamani walikuwa wanalipwa mshahara mkubwa ukilinganisha na sasa mkuu? :oops: :oops: :oops:
 
Kwa hiyo wewe unakubaliana na UJAMBAZI huu wa polisi au msimamo wako ni upi? Nini kifanyike?

Hapana sikubaliani na ujambazi ninachokisema ni kwamba huwezi kutegemea kazi nzuri kutoka kwa Polisi au profession yoyote ile kama pia hauimarishi na kuboreaha mazingira, leo hii ukisema Waziri hakuna gari, nyumba na Mshahara laki 5 unafikiri ni wangapi watataka kuwa Waziri ?

Hivyo ili kubadilisha hali ni lazima kuendane kuboresha mazingira pia, vinginevyo hakuna kitakachobadilika.
 
Bora ukutane na majambazi kuliko polisi. Jambazi atakupora tu, Iia polisi atakupora na kukuua kabisa; akikuonea huruma anakubambikiza unga na bunduki ukafie jela.
 
Bora ukutane na majambazi kuliko polisi. Jambazi atakupora tu, Ila polisi atakupora na kukuua kabisa, akikuonea huruma anakubambikiza unga na bunduki, ukafie jela

Sasa unaelewa hiyo maana yake ? Unaelewa jamii ambayo imefikia hapo ni jamii ya aina gani ? What’s next ?
 
Sasa unaelewa hiyo maana yake ? Unaelewa jamii ambayo imefikia hapo ni jamii ya aina gani ? What’s next ?
Ujambazi wa polisi hatuutaki na pia hatutaki injustice katika nchi hii inayopelekea maovu kama haya. Sasa wewe unadhani nini kifanyike ili tuwe na jeshi la polisi na jamii iliyostaarabika? Tunatokaje kwenye mkwamo huu?
 
Polisi inabidi wafanyiwe vetting kabla ya kuajiriwa na wakiwa kazini, wabambikia kesi na wala rushwa ushahidi ukusanywe wapigwe Court Marshalls na kuondelewa kazini.
 
Ujambazi wa polisi hatuutaki na pia hatutaki injustice katika nchi hii inayopelekea maovu kama haya. Sasa wewe unadhani nini kifanyike ili tuwe na jeshi la polisi na jamii iliyostaarabika? Tunatokaje kwenye mkwamo huu?

Wafanye kama walivyofanya kwa Wanajeshi, wawaboreshee mazingira ya kazi wakishafanya hilo ndio sasa wanaweza hata kuajiri watu ambao pia wanaweza kuwa waadilifu na waaminifu, vinginevyo huwezi kutegemea Polisi awe mwadilifu kama anafanya kazi kwenye mazingira duni kiasi hicho.

Ulishawahi kuona mtu kapata ajali mbaya barabarani watu wanapiga simu polisi na polisi kuja kuchukuwa maiti barabarani ? Uliona vifaa vya kazi vya polisi ?
 
Shida sio wasomi tena hao wasomi wenyewe ndio wanaoisumbua serikali maana kwa elimu zao anaona anachelewa kupata maendeleo akifikiria elimu yake.
Mbona zamani kulikuwa na wa elimu ndogo hadi la saba b lakini weledi ulikuwepo? Tatizo hapo ni tamaa ya mali haraka haraka ebu wapewe mshahara wa kutosha uone kama kazi haijafanywa vizuri hata na rushwa yaweza pungua.
Ni bora wawe polisi wachache posho kubwa

Sent using Jamii Forums mobile app
ukizungumzia swala la mshahara mimi napingana na wewe kama ni mshahara wapo viongozi wa serikali wa ngazi za juu sana wanalipwa mamilioni ya pesa lakini bado wanajipimia kwa urefu wa kamba yao! mfano mzuri we umeshuhudia kashfa ngapi za ufisadi ambazo zinahusisha mabilioni ya pesa na ukiangalia wahusika ni watu wanaolipwa pesa nyingi zaidi ya hao wanaojiita polisi. kwaiyo hata walipwe tsh ngapi bado wataendelea na tabia yao kifupi ile ni nature tu ya ile kazi maana karibu hao jamaa wote ndio wapo hivyo! solution pekee wanapokuwa course wafundishwe sana juu ya maadili tofauti na hapo tutaendelea kuona vioja vya hawa jamaa kila siku....!! kwakweli mtoa mada umeongea jambo la maana sana kwani hawa jamaa wamekuwa kero sana katika jamii yetu unakuta mtu una maisha ya chini sana tofauti na yeye anayepokea mshahara japo ni mdogo lakin bado anatamani kukuchanja wewe mwana nchi wa hali ya chini tena anachofanya ni kukutengenezea kesi...! kama kuna mtu yeyote mwenye mamlaka umu jukwaani ninaomba alipitie kwa makini sana bandiko la huyu bwana kisha akalifanyie kazi kwani ameongea kitu cha maana sana kuhusu hawa jamaa
 
Ndio maana nimeagiza Waziri wa Mambo ya ndani na IGP Ziro wajiudhuru nyadhifa zao ili kuonyesha uwajibikaji binafsi. Wasimtwishe Rais Samia lawama zote hizi na kupelekea chuki dhidi ya serikali kutoka kwa wananchi wanyonge wanauliwa na polisi kama kuku kila kukicha.
Rais kama rais pia anastahili lawama sababu yeye ndiye aliye mteua wazir mwenye dhaman kwaiyo anachotakiwa kufanya rais akiona mtu ha fit kwenye teuzi yake atumbue" sasa we kama rais unaona kabisa kwamba mtu hawajibiki bado tu una mchekea, unaona matendo ya uhalifu yanaongezeka bado tu umekaa
  • Waziri yupo
  • Igp yupo
  • Rpc yupo
Wote hao wapo lakin bado tu vitendo vya uhalifu vinazidi kuongezeka maana yake sasa raisi asipowawajibisha tafsir yake ni kwamba anavutiwa na ule uovu unaoendelea
 
Hata sababu wanazotoa baada ya kumuua polisi mwenzao ni za kitoto sana. Polisi mwelewa mwenye divisheni wani au twu hawezi kutoa sababu ya kiqumer kama hii waliyotoa hawa failures :oops: :oops: :oops:
Nakuhakikishia Kati ya Polisi 7 wa Mtwara, mmoja ni form 6 waliobaki Wana digrii. Sasa sijui elimu unaongelea ipi? Polisi imeoza.
 
Tatizo sio form four fulure, maana hao ndio wametoka kwenye familia duni hapana
Hapa kuna shida ya mfumo "dokoa nyama nimalize mboga yote" maana haiwezekani baba yangu namuona akiiba vitu analeta nyumbani ananiambia mwanangu "kuwa mkubwa nawe utafute vyako",
Siku nikikuwa mkubwa nafahamu kumbe baba alipita njia hizi ok akili itanikaa kichwani wapi nipite!
Maana waswahili husema "Akili za kurithi anaerithi huwa mara mbili ya aliyemrithisha ;,
So hapa kwa maoni yangu mfumo mfumo ndio unataleta shida kwenye Taasisi yetu hii pendwa inayotulinda wanachi wa Tanzania.
 
Hata uwe na div 1,2,3masters,PhD ukishakuwa na tamaa,njaa itakuchukua tu
Alafu polisi kokote duniani kuna good cops and bad cops(crooks)

Ova
 
Hata uwe na div 1,2,3masters,PhD ukishakuwa na tamaa,njaa itakuchukua tu
Alafu polisi kokote duniani kuna good cops and bad cops(crooks)

Ova
Njaa ni kitu kibaya sikatai lakini njaa ya msomi haiwezi kufanana na njaa ya kilaza. Serikali ya CCM ituondolee vilaza hawa waliojaa ndani ya jeshi la polisi ili kulijengea heshima jeshi hili linalozidi kuoza kila kukicha.
 
Afrika nchi nyingi polisi wako hivyo hivyo
Kitabia

Ova
Si kweli mkuu. Mbona kule Kenya, Rwanda na Burundi hakuna mapolisi wenye njaa kali kama hawa waliotapakaa hapa nchini tanzania. Hawa wa hapa wamezidi, sio kwa njaa hizi wanazopora mali za raia na kisha kuwaua. Ni uhuni na ujambazi wa hali ya juu.
 
Njaa ni kitu kibaya sikatai lakini njaa ya msomi haiwezikufanana na njaa ya kilaza. Serikali ya CCM ituondolee vilaza hawa waliojaa ndani ya jeshi la polisi ili kulijengea heshima jeshi hili linalozidi kuoza kila kukicha.
Labda polisi wawekewe mazingira bora,kuanzia mishahara,makazi,afya etc wawalipe vizuri
Ili kuwapunguzia kujingiza kwenye tamaa na kushirikiana na wahalifu

Ova
 
Si kweli mkuu. Mbona kule Kenya, Rwanda na Burundi hakuna mapolisi wenye njaa kali kama hawa waliotapakaa hapa nchini tanzania. Hawa wa hapa wamezidi, sio kwa njaa hizi wanazopora mali za raia na kisha kuwaua. Ni uhuni na ujambazi wa hali ya juu.
Mh nani kakuambia
Kenya polisi wao wana njaa,wako polisi macrooks mzee
Hata burundi,zambia,Malawi kote huko
Nchi kidg ambsyo polisi wao wako kikaz ni Namibia na Botswana
South Africa tu polisi wao wapo ma crooks pia

Ova
 
Back
Top Bottom