manuu
JF-Expert Member
- Apr 23, 2009
- 4,064
- 10,723
Leo kuna rafiki yangu aishie Arusha amenipigia simu na kunieleza usiku wa kuamkia leo amevamiwa na kundi la majambazi wapatao 15 na wamechukua vitu vingi nyumbani kwake ila cha kushukuru hawakujerui mtu yeyote.
Jamaa ananiambia ilikuwa kama kama saa 8 hivi usiku akasikia kama kishindo fulani aliposhtuka akawai bastola yake kidogo akasikia kwenye chumba alipolala wife ukunga,wife na watoto walikuwa wanalia sana na akasikia sauti ikimuuliza wife mume wako yupo wapi kwani yeye ndo tunamtaka tumuue.
Jamaa kusikia hivyo sababu alikuwa amelala chumba cha pili kumpisha mama sababu ni mzazi wa kama mwezi hivi akapnda darini akatulia,Huku chini wale majambazi wakaendelea kupita vyumbani kumtafuta jamaa walipomkosa mmoja akasema anabahati sana huyu,akatoa amri kwa wale wengine wachukue vitu wapakie kwenye gari walichukua vitu vingi sana. Baada ya mda jamaa akashuka kutoka darini anasema alikuwa anatetemeka mpaka bastola akawa hawezi kuishika kwa woga.
Duh,Jamaa anajiuliza hana kisa na mtu na si mtu wa kutoka nje ya ndoa, kwa nini sasa wale jamaa walikuwa wantaka roho yake?
Ila kweli gate na ukuta wenye electric fence hausadii kitu jambazi akitaka kukuingilia kwani jamaa amejizatiti kweli kwenye securitywise lakini majamaa wakazama ndani.
Unadhani nini tena mtu unaweza fanya kuongeza ulinzi nyumbani hasa wakati wa usiku?