DOKEZO Nyaya zinazoshikilia nguzo zinaibwa zinatumika kufungia Linta!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

mgt software

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
13,767
7,115
JF wana

Nimefanya uchunguzi wa kitafiti kujua nini hasa malalamiko ya kila wakati ya watu kuiba miundombinu nikakuta kwamba kasi ya kupanda kwa nondo ndio sababu kuu watu kuiba nyaya za TANESCO na kuzitumia kushikiria paa nyingine kuziweka kwenye linta.

Ujenzi huu hatari umeanza hivi karibuni . Wezi hukata nyaya zinazosimami nguzo. Hizi nyaya utandikwa juu kama mbadala wa nondo, nyingine uzitumia kusukia paa. Si rahisi kugundua nyumba iliyowekewa haya manyaya kwani wako fasta kuhakikisha kila hatua wanapiga rip. Siri nyingi napewa na wajenzi.

Pia watu wasio waaminifu huuziwa na wafanyakazi wa TANESCO. Kwa sasa wezi wamebadilikia sengenge zenye uzito na unene wa kadiri nazo zinatumika kama nondo.
 
Sasa hivi hadi taa zinazotumia solar vibaka wanaiba batteries na hizo solar panels. Nchi imekuwa ya ajabu sana sijui tuna laana gani? Na muda si mrefu watamalizia na hizo nguzo kwenda kuuza scrapers.

Hatuna laana yeyote na acha kutunenea vibaya nchi yetu!

Kazi ni moja tu piga shaba majambazi yote na vibaka na panya road alafu zika kama halaiki kwenye shimo moja!

Walahi hutasikia malalamiko haya, yaani ni kuwapoteza kabisa hamna haja ya hospitali au mahakamani wasiendelee tena kula pesa ya serikali walahi
 
JF wana

Nimefanya uchunguzi wa kitafit kujua nini hasa malalamiko ya kila wakati ya watu kuiba miundo mbinu nikakuta kwamba kasi ya kupanda...
Ndugu Mteja

Tunashukuru sana kwa ushirikiano wako mzuri, tunaanza uchunguzi maramoja Kupitia idara yatu ya usalama (Security) tutafurahia zaidi kama utaweza kutusaidia mtu au eneo wanaofanya hivyo ili tuanzie hapo.
 
Halafu wakikamatwa wakipigwa risasi Abdul nondo anakuja kuwatetea

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
Mkuu
Dola inahakikisha vijana wanakosa hata fursa ya kujiajiri halafu dola hiyo hiyo inawaua watuhumiwa wa wizi....

Hivi umekaa na kutafakari kwa nini uhalifu unaongezeka?

Please sit down and think deeply wewe hauna ajira, unataka kufanya ujasiriamali kwa mtaji kiduchu unakutana na mazingira ya kutoweza hata kuanzisha biashara.... kilimo ndo hicho cha kuangalizia mvua....

Vijana wanakosa ufahamu mzuri kimaisha kwa sababu hata elimu yenyewe ya msingi imekosa misingi ya kuwajenga wajitegemee.

Ni laana kubwa sana kuwafanya vijana kama maadui wa jamii. Tunapaswa kuwajenga kwa sababu ndiyo nguvu yetu ya uzeeni.

Sishabikii wala sikubaliani na wizi lakini wanapokamatwa sheria ichukue mkondo wake au la tuwaambie Wabunge wetu wapitishe sheria kuwa mtu akituhumiwa kwa wizi apigwe risasi afe
 
JF wana

Nimefanya uchunguzi wa kitafit kujua nini hasa malalamiko ya kila wakati ya watu kuiba miundo mbinu nikakuta kwamba kasi ya kupanda kwa nondo ndio sababu kuu watu kuiba nyaya za tanesco na kuzitumia kushikiria paa nyingine kuziweka kwenye linta...
Usalama wa nchi umejengwa kwenye misingi ya kuchunguza wanachowaza wananchi na siyo kufanya analysis za damages za kijamii kwenye maamuzi ya watawala.

CCM imefika mahala inawakumbatia wapiga deal kuliko wajenga nchi. Wafanyakazi wanakatwa kodi kubwa ambapo mwenye akili atagundua kwamba wafanyabiashara wakubwa wanapata haueni kubwa kwenye kodi. Angalia matajiri wakubwa hawapo kwenye orodha ya walipajikodi wakubwa.

Mazingira ya uhalifu yanajengwa na matendo hasi ya dola dhidi ya wananchi ambapo watu hutafuta namna nyepesi (kihalifu) kujikimu.

Tunafikia mahala moundombinu inakuwa hatarini kuhujumiwa na kuharibiwa kabisa lakini akili na uwezo wa dola ni namna ya kuwalinda watawala na siyo kuilinda nchi itakiwavyo.

Inauma sana kwa haya matokeo tunayoyaishi
 
Ndugu Mteja

Tunashukuru sana kwa ushirikiano wako mzuri, tunaanza uchunguzi maramoja Kupitia idara yatu ya usalama (Security) tutafurahia zaidi kama utaweza kutusaidia mtu au eneo wanaofanya hivyo ili tuanzie hapo,
Msiishie Kupost tu Hii ni hatari Huko tuendako
 
Ndugu Mteja

Tunashukuru sana kwa ushirikiano wako mzuri, tunaanza uchunguzi maramoja Kupitia idara yatu ya usalama (Security) tutafurahia zaidi kama utaweza kutusaidia mtu au eneo wanaofanya hivyo ili tuanzie hapo,
ohoooo ndugu mteja tena
haya ndugu mteja kawachome waliokupa siri
 
Watu hawataki kusema tuu ya kuwa Utawala wa Samia na CCM kwa ujumla umefeli kabisa kabisa, na taifa linadidimia kwa kila nyanja.

Sent from my SM-A125F using JamiiForums mobile app
Wizi wa nyaya za umeme upo tangu utawala wa Mkapa, wizi wa mafuta ya transformers ukashamili kwenye utawala wa Kikwete.
Kwenye kuharibu miundombinu tukubaliane tu kuwa sisi Watanzania ni wajinga.
 
Back
Top Bottom