UJAMBAZI: Magari yote yenye tinted yapigwa marufuku na Polisi jijini Dar

Nchi ya wajinga inaongozwa na mjingam,kwanini hawa polisi wanajua hasa maana gari kuwekwa "tinted" kwenye vioo,ninavyofahamu mimi nchi nyingi zenye hali ya hewa ya joto kali yenye nchi zenye Jua kali ndio gari zinawekwa vioo "Tinted",maana ya kuweka tinted kwenye vioo vya gari ni kupunguza ukali wa jua kwenye vioo..

Polisi wafanye kazi zao kwa ueledi sio kutafuta suluhisho kwa njia ya rahisi kama hivi,kama ni majambazi basi watafute njia husika ya kuwakamata majambazi sio kuwaadhibu wakaazi wote wa daresalam kwa makosa ya kikundi kidogo cha majambazi
 
Habari ndugu zangu!
Tinted siyo kosa la jinai na haijawahi kuwa kosa!
Nchi inaongozwa na sheria!
Kwanini Tunyanyasike Kwa matamshi yasiyo zingatia sheria? Kama Kuna haja ya kutoa Tinted kwanini wasipeleke mswada bungeni?
Nchi haiendeshwi Kwa matamko tu kama vile unaongoza punda! Sisi ni watu, Tena tumeenda shule, Tunaomba tuongozwe Kwa sheria Tafadhari! Haiwezekani kisa kiongozi umeibiwa mchepuko, ama Kwa kushauriwa na mkeo halafu ghafla unatangaza kupiga marufuku!

Jeshi la polisi lizingatie sheria
Haiwezekani hata siku moja jeshi lenye taaluma na weledi waje na simple excuse ya kupiga marufuku Tinted eti kisa Kuna baadhi ya watu wanatumia kufanyia ngono! Hivi tangu lini Kuna sheria inayoelekeza ngono ifanyiwe wapi? Kuna watu wanafanyia porini je tutachoma misitu?
Kama hoja ni uharifu je; Bodaboda zinazotumika kiharifu zina Tinted?
Kwanini ghafla tinted zipigwe marufuku bila kuzingatia athari Kwa walaji na wauzaji? Inamaana nayo hayo magari ya serikali yaliyowekwa Tinted hutumika kiharifu?
Wanasheria mko wapi kupeleka hawa watu mahakamani? Kuna watu wana stock kubwa na imelipiwa kodi inakuaje mtu apige marufuku ghafla? Waandishi Wa habari itisheni mahojiano kuhusu jambo hilo.

Faida za Tinted
1. Kuzuia mwanga.
2. Kutunza kioo
3. Haivutii wezi/ vibaka kuvunja vioo kuchukua Chochote!
4. Kiusalama inazuia mtu kuonwa na kila mtu.
5. Matajiri na watu maarufu si vyema kuonekana na kila mtu wapitapo ili kuepusha kero mbalimbali.
6. Wagonjwa si vyema kuonekana
7. Umbea Kwa majilani kuangalia kila kitu unachobeba. N.k
WAMIRIKI WA MAGARI KUNA UMHIMU WA KUFANYA MAANDAMANO YA AMANI KUELEKEA MAKAO MAKUU YA POLISI KUPINGA ZUIO LA TINTED
Ganja @ work.
 
Kwanza sheria ipitishwe na waanze na magari ya serikalini wengine wafuate ili tujue wako serious

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu hii siyo sheria Ni mwendelezo wa matamko yasiyozingatia sheria. Umeshawahi kuona STL, STK zina sticker za bima which means gari la serikali likipata ajali to the point of unrepairable ni kutupa ambapo zingekuwa Na comprehensive insurance tungekuwa tunafidiwa magari mampya kama nchi. So na hili tamko ambalo nadhani ni amri sidhani litagusa magari ya serikali. Mi sijawahi kuona wala kusikia eti gari la serikali kukamatwa eti limevunje sheria za usalama barabarani. Ni hayo tu.

Mungu ibariki Tanzania yetu
 
Kaimu Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dsm amepiga marufuku uwepo wa magari yenye vioo vya tinted ktk jiji la Dar.

Amesema imebaidinika magari hayo hutumika kwa mambo ya ujambazi na uvunjifu mwingine wa maadili ikiwemo ngono, hivyo kuanzia Jumatatu itafanyika operesheni maalumu ya kukamata magari hayo.

Chanzo: ITV jiji letu!
Hivi anajua kuwa Bashite na wenzake ndiyo magari wanayotumia kwa shuguli zao binafsi hapa mjini?
 
Upuuzi sana huu inaonesha jinsi gani polisi wamekoma njia mbadala yakukusanya mapato ya rushwa toka road license ipigwe chini.

Mpinga alikuja na matamko yake kuwa spotlight zote zitolewe then badae akasema zisitolewe lakini zifunikwe bila kujali kuwa watu washalipishwa sana faini......

Tatizo polisii kumejaa darasa la saba na form four failure

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma tena page ya ITV kule facebook inaonyesha watu watoe tinted "ili kuondokana na adha ya ukaguzi". Sijaelewa, kwa hiyo kumbe sio kosa bali mtu utapata adha ya kukaguliwa mara kwa mara au? Mwenye written tangazo angesaidia kulibandika humu.
 
Majirani.

Maandamano labda ya Magari na sio ya kwenda kwa miguu.

Ushauri wangu kwako Tii sheria bila Shuruti/i].. sera kuu za utawala huu ni Chuki na chuki inazidi kukua na kuna kitu kimeongezeka nacho ni wivu vumilieni tu kutesa kwa zamu.

Mkuu hiyo siyo sheria ni tamko/amri ya mtu mmoja tu. Hakuna sheria iliyopo ya kuzuia/kukataza tinted. Lakini kwa kuwa mkulu mwenyewe alishasema anaweka katiba pembeni kwanza ili anyooshe nchi, sasa kila mwenye mamlaka ananyoosha tu hata ambacho hakijapinda.
 
Kaimu Kamanda wa polisi kanda maalum ya Dsm amepiga marufuku uwepo wa magari yenye vioo vya tinted ktk jiji la Dar.

Amesema imebaidinika magari hayo hutumika kwa mambo ya ujambazi na uvunjifu mwingine wa maadili ikiwemo ngono, hivyo kuanzia Jumatatu itafanyika operesheni maalumu ya kukamata magari hayo.

Chanzo: ITV jiji letu!
Hiii itahusu pia na gari za polisi zenye tinted?
 
Usiombe mida ya kuanzia saa mbili usiku uharibikiwe na gari pale ocean road/barack obama beach utajuta! Na hapo ni chini ya km kutoka ikulu!
HAHAHAAAA UTATAMANII ARDHI IPASUKE
MIMI NILISHAWAHI SIMAMA PALE DARAJANU
Kawe KUMWOKOA MAMA MMOJA YAKASIMAMA MAGARI KAMA MANNE GAFLA NAWAOMA WANAJESHI WANACHUNGULIA KWENYE FENSI TUKIO ZIMA NA BASTOLA SHINGONI WAKITUAMBIA TOKENI HAPO HARAKA SANA

CC..MRANGI
LOH
 
Back
Top Bottom