Ujamaa wa Tanzania ulishindwa, ubepari wa Tanzania hauelewiki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ujamaa wa Tanzania ulishindwa, ubepari wa Tanzania hauelewiki

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mkwawa, Jan 4, 2012.

 1. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #1
  Jan 4, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Nchi ya Tanzania imepitia mifumo kadhaa ya kiuchumi. Mfumo wa kwanza wa african socialism ulioasisiwa na Mwl Nyerere ulishindwa miaka ya mwanzoni mwa 80 kwa kuzalisha umasikini, kutokuwajibika, wezi na wahujumu wa mali ya umma. Pamoja na kwamba mfumo huu na sheria ziliweka wazi viongozi kutukumiliki mali au kutokuwa na biashara bado waliendelea kuwa navyo kwa njia za panya.

  Miaka ya 80 Nyerere akishuhudia umasikini, njaa, ukosefu wa bidhaa madukani, kushindwa kwa vijiji vya ujamaa na ukosefu mkubwa wa taaalamu na upoteaji mkubwa wa utu wa binadamu mwaka 1985 akaachia madaraka kwa hiari jambo na kitendo cha kishujaa kwa viongozi wa kiafrika na Tanzania ya leo.

  Kwa sasa tuna mfumo wa ubepari mseto usiofuta sheria za kibepari wala usio na sheria za kudhibiti au kuumulika umezalisha wezi na viongozi wafanyabiashara kwa kutumia kodi na mali za umma bila kujali wala huruma. mfumo huu mseto ndio umewafanya viongozi wa kisiasa na serikali kujilimbikizia mali bila biashara na bila ya sheria yeyote kuhoji. Mfumo huu umemsahau mwananchi wa kawaida na mali za nchi zimekuwa zikiuzwa bila faida kwa nchi na kwa muuzaji. mfumo huu umekaribisha walafi, walaghai, wahuni, wahujumu na wasaliti kwa sababu tu hatujautengenezea sheria za kuudhibiti.

  Mifumo yote miwili inaonekana inatushinda kwa sababu kama nchi hatukujiandaa kwa mfumo wa kwanza wala hatujajiandaa kwa mfumu wa pili. Katiba tuliyonayo haina nafasi kwa mifumo yote miwili. Nyerere alibeba mfumo kichwani kwake , na sasa mfumo huu wa ubepari mseto hauna sheria za jinsi ya kuuendeshal. sheria za kiuchumi haziko wazi wala za uwekezaji haziko wazi.

  Ili Ubepari huu mseto uweze kufanyakazi ndani ya nchi ya Tanzania ni lazima kuangalia sheria zetu mama. katiba ijayo ni lazima ijadili kwa undani mfumo wa uchumi na jinsi ya kujenga Tanzania yenye neema. Ni kazi ya wananchi, wachumi, wanasheria, wanataaluma wote kujadili kwa kina swala la uchumi kwenye katiba yetu mpya.

  Chief Mkwawa wa kalenga.
   
 2. bona

  bona JF-Expert Member

  #2
  Jan 4, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 3,796
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Labda nikurudishe nyuma kidogo, unaposema ujamaa wa nyerere ulishindwa nadhan unakosea kwani ulishindwa kwa kutumia vigezo vya kimagaribi vinavyopima uchumi kwa gdp ect unatakiwa ufaham kwanza hivi vigezo ni kiini macho tu kwa maisha ya mtanzania mmoja mmoja hatukuwa maskini kwani nakumbuka bibi yangu kule kijijini alikua ana akiba ya chakula mwaka mzima, mboga na matunda shambani ya kuchuma tu hakuitaji kuuza mahindi yake kunilipia ada mpaka chuo kikuu kwani nilisoma bure na hospital nilikua nikitibiwa bure kumuita mtu kama huyu maskini eti kwa sababu hana dola moja kwa siku ni ujinga coz she never needed it anyway!

  La pili unatakiwa ufaham ni nchi zilizochagua uchumi wa kijamaa tu ndio zimepiga maendeleo kwa kujitegemea kama cuba, china, urusi, na sasa venezuela etc nchi za kibepari zote zinaishia kua failed state, vita na njaa isyo ya kawaida, zilizoendelea ni zile zilizopata mwanya wa kuzinyonya nchi nyingine wakat kwa wakat wetu hatuna wa kumnyonya ili tuendelee kwani ubepari unataka uproduce in excess ili upate masoko hadi nchi za nje kama china kwa sasa!

  Kwa hiyo ujamaa unaonekana kama ni njia ngumu ila tutarud tu kama wenzetu kina Zimbabwe, Venezuela na Bolivia ambao waliishi kwenye ubepari miaka mingi mpaka yalipowafika shingoni si zimbabwe ilikua inachukuliwa kama mfano kwa africa kwa hatua za maendeleo ila waligeuka wananchi!
   
 3. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #3
  Jan 4, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Mkuu bona
  Mimi nashawishika ujamaa wa Nyerere ulishindwa kwa vigezo vya Tanzania wala sio vya magharibi. Mwanzoni mwa miaka ya 80 hali ya uchumi ilikuwa mbaya sana, kumbuka uhujumu uchumi ambao marehemu sokoine alikuwa akipambana nao. Kumbuka foleni za bidhaa za kawaida madukani kama sukari, mafuta, nk.

  Mwanzoni mwa miaka ya sabini nchi ilikuwa nzuri ilikuwa inauchumi mzuri. tulipoanza na siasa za ujamaa bila matayarisho tulishindwa. Vijiji vya ujamaa vilikuwa ni kizazaa kikubwa na vilishindwa vibaya sana. Viwanda vilivyo anzishwa ama achwa na wakoloni vilikufa miaka ya mwanzoni au katikakati mwa 80.

  Sera zote na maazimio ya siasa za ujamaa za Tanzania zilikufa. Elimu ilianza kuporomoka na kipatocha mtanzania kushuku huku shilingi ikishuka thamani. uwezo wa nchi ulipungua ndio sababu miaka zaidi ya ishirini hatuna vyanzo vipya madhubuti vya nishati.

  Sera za ujamaa zimezalisha mafisadi unaowaona leo bila sheria kuwashikisha adabu. List inaendelea. Bibi yako kuwa na chakula kijijini ule ulikuwa ujima alikuwa analima na mahitaji ya wakati ule hayakuwa makubwa. Nishati ilikuwa koroboi, na wengi walikuwa hawasomi. Watanzania wengi hawakuwa na mwamko wa kupeleka watoto shule kama leo. Nchi haikuandaliwa kuweza kupambana na ongezeko la watu na mahitaji yao.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 4. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2013
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  Ujamaa na kujitegemea(ukomunisti) haukupigiwa kura ya wananchi wala kupata baraka ya bunge . Ni ushabiki wa mtanzania mmoja tuu kutaka nchi isafiri katika njia za kikomunisti na kulifanya taifa zima lifuate njia hizo kinguvu. ni vizuri katika katiba mpya ujamaa na kujitegemea(ukomunisti) ufutwe mara moja na kulaani sera zake zote za kifashisti.
  madhara tuliyoyapata wananchi wa tanzania kwa kufuata siasa hii ya ujamaa na kujitegemea ni mabaya sana kupita hata nchi iliyoingia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe.
  1-kuchukia matajiri na kunyang'anya mali zao kuliua sana soko la ajira kwa wananchi.
  2- Kutokujenga shule nyingi za sekondari na vyuo vikuu kwa makusudi mazima, ili taifa lije kujitegemea kwa watalaamu wake wenyewe nako kulichangia sana kurudisha nyuma ustawi wa jamaii.
  3-kuwaimbia kwaya ya kuwasifia viongozi wa chama kila siku hata kama walikuwa wanafanya mabaya kwa wananchi kulichangia sana kuleta sumu ya kutowajibika kwa watendaji wakuu serikalini. maana hapo cheo kilikuwa ni ujiko na wala sio dhamana tena.

  4- kutojenga daraja la working class katika jamii na kuwatumbukiza watu wengio kuwa wakulima wa ujima kulilifanya taifa lipoteze mapato mengi ya P.A.Y.E

  5--kuwakata watu wasio na kazi mitaani DSM na kuweka rumade na kuwafunga miezi mitatu mitatu kwa kuwaita wazurulaji ulikuwa ukiukaji wa haki za binadamu.


  Hivyo itakuwa ni vizuri sana kama hii za ujamaa na kujitegemea ikafutwa mara moja katika katiba mpya.
   
 5. b

  babou Member

  #5
  Aug 22, 2013
  Joined: Jul 29, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  epuka kuandika juu ya mambo usiyoyajua. rudi shule ukasome vizuri. ujamaa na kujitegemea ni moja kati ya falsafa bora na zenye mashiko sana duniani.
   
 6. k

  kisorya Member

  #6
  Aug 22, 2013
  Joined: Apr 27, 2012
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Jaribu kutumikisha ubongo kidogo kabla ya kuleta uharisho wako humu, nani kakudanganya kwamba Ujamaa na kujitegemea(Socialism and Self relience) ni ukomunist? Rudi shule haraka sana ukajifunze.
   
 7. Askari Kanzu

  Askari Kanzu JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2013
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,526
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Naona hapo unachanganya mambo. Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ilianza rasmi 1967 kufuatia Azimio la Arusha. Sasa ukisema "Mwanzoni mwa miaka ya sabini nchi ilikuwa nzuri..." inakuwa vigumu kukuelewa una maana gani. Kumbuka pia uchumi uliporomoka kufuatia vita vya Kagera (1978-79).
   
Loading...