Ujamaa wa Tanzania ni kwenye Katiba tu! - Zitto Kabwe

Ujamaa umewashinda akina Lenin na Mao utauweza wewe Zitto?

Usitake kuchekesha watu saa hizi.

Umebuuugi man.

Ungekuwaa mjamaa ungejiunga hapo awali na chama cha kibepari? au huo ujamaa umeujuwa...

Nimependa sana comment yako. Tunafanyiana maigizo ya kitoto kwenye siasa. Nayaona maigizo hayo kama mapenzi ya kitoto. Unakuta mtu kakaa na mpenzi wake miaka nenda rudi wakiachana unasika ooh, mwanake/mwanamegani hajui hata...siku zote hukuyaona haya hadi ulipoachika. Tufike sehemu watanania tuache kuchezewa akili na hawa wanasiasa.

Jana mwingine anatangaza kuchukua majimbo ya CUF. Eti mpinzani anaye pingana na wapinzani kwa nin asijiite timu B ya chama tawala. Siasa zetu zinatia kichefuchefu kwa hawa wanasiasa wanatuana sie km hatuna akili.
 
Last edited by a moderator:
NI vema viongozi hasa wa vyama vya siasa wakaweka wazi sera zao juu ya mfumo wanaoufuata ili hata wapigakura wajue na wachague kwa kuzingatia hilo pia. Ujamaa kwa sasa umebaki kwenye vitabu, sidhani hata CCM kama inaukubali mfumo huu ingawa hakuna kiongozi aliyejitokeza kuhoji.

Nadhani ni wakati muafaka vyama vya siasa vianze kujitofautisha kwa mfumo wa uchumi wanaouamini na watakao utumia kama wakipewa nafasi ya kuiongoza nchi.

Hilo la msingi ! Maana kwa sasa tofauti YA vyama vya siasa Iko kwenye MAJINA na MAVAZI TU ! Lkn ilipaswa tujue CCM wanaamini nini tofauti na CDM hivyo kwenye uchaguzi tungechagua SERA zaidi kuliko kushabikia tu kama mpira.
Kila mara utasikia CCM mafisadi lkn hakuna anaeonyesha SERA Itakayo komesha ufisadi huku tukijua kua yeyote atakae ingia Ikulu atawatumia watanzania ktk Utekelezaji wa kazi mbalimbali.
 
Kama una access please watch TBC-1 now!.

Zitto Kabwe na Simbachawene wako live on Tbc -1 wakizungumzia uchumi!.

Mazungumzo hayo yamejikita katika kujadili muswada wa sheria wa kuboresha mazingira ya kufanya biashara Tanzania.

Amesema tatizo kubwa la Tanzania kama nchi, hatuna mfumo wa ukweli wa eundeshaji wa uchumi wa taifa. Katiba inahubiri kuwa Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya siasa ya Ujamaa na Kujitegemea. ambayo mfumo wake wa uchumi ulipaswa kufuata misingi ya ijumaa.

Zitto amesema, kiukweli Tanzania haifuati misingi ya uchumi wa kijamaa bali tunafuata misingi ya kibebari tena ubebari mbaya kabisa!.

Kwa maneno haya ya Zitto yanamaanisha sisi Tanzania "We don't practice what we preach"!.

Kwa mtaji huu, jee tutafika?!.

Pasco.
Nikimtazama ZITTO namuona mwalimu JK Nyerere kwa mbali. Namaanisha ana fikra na mtazamoo safi juu ya nchi hii. Kwa upande wangu Zitto ni mwanasiasa anayehitajika saana katika nchi hii. CHA MUHIMU ZITTO ZUBERI KABWE USIFE MOYO, UTASEMWA SAAANA, LAKINI WEWE ENDELEA KUTENDA MEMA, MUOMBE MWENYEZI MUNGU ATAKUPA NGUVU ZAIDI. Ni mtazamo wangu
wapendwa msijenge chuki.
 
Ujamaa umewashinda akina Lenin na Mao utauweza wewe Zitto?

Usitake kuchekesha watu saa hizi.

Umebuuugi man.

Ungekuwaa mjamaa ungejiunga hapo awali na chama cha kibepari? au huo ujamaa umeujuwa...
FaizaFoxy.
 

Attachments

  • 1427125935025.jpg
    1427125935025.jpg
    10.8 KB · Views: 143
Last edited by a moderator:
Pasco kwa Maoni yako unaonaje hiki anachokihubiri ndugu yetu Zitto Kabwe? Ni kweli katika mfumo wetu tunauhitaji ujamaa ambao kwa moja ama nyingine ndio uliosababisha Baba wa Taifa Mwl Nyerere atukanwe na baadhi ya watu hapa Tanzania na kwa namna fulani ilikuwa ni kama moja ya Sign ya "kushindwa" kwa uongozi wa Nyerere.

Binafsi naona kama huu ni mwanzo wa kushindwa kwa huyu mwanasiasa Machachari. Yaani leo hii ukawaze kuwarudisha watu kwenye Maduka ya ushirika? Wapange foleni kununua Chumvi,Sukari,Sabuni na mahitaji mengine ya msingi. Iwe ni marufuku kuwa na chombo cha habari nje ya Chombo cha serikali... Hapana nasema tena hapana au labda niwe siijui misingi ya kijamaa ndio naweza kuukubali mfumo huo. Au labda mpaka nitakapo sikia huo mfumo wa ujamaa anaosimamia Zitto Kautohoa kutoka wapi na unasemaje? Vinginevyo Never ever.

Halafu mkuu Pasco hivi kwanini wanasiasa wetu maarufu wanashindwa kumtambua Nyerere kama Baba wa Taifa?? Nimeona hata Zitto kwenye Tamko lake alipoongoa na waandishi wa habari,pamoja na kudai wao ni wafuasi wa Unyerere, akilenga kusifu kile kilichosimamiwa na kuasisiwa na Baba wa Taifa lakini ameshindwa kumuita wala Kumtambua Nyerere kwa Utambulisho wake tunaoutambua sote kama taifa. Hivi hii imakaaje? Ni Wanasiasa wachache sana wanaomuita Nyerere kwa jina la Baba wa Taifa tena wengi ni kutoka Upinzani hususani Chadema, kwa masikio yangu nimewasikia, Mbowe,Dr Slaa,Mnyika,Mkapa wakijitapa na kutamka bila ukakasi "Baba wa taifa" Never sijawahi kuwasikia, Tundu Lissu,Zitto,Kikwete,Mwinyi etc wakitumia jina hilo. Wengi utasikia "Mzee wetu" "Mwasisi wetu" na mengine yanayo fanana na hayo..

Hivi ni nani aliyetoa amri ya Nyerere kuitwa Baba wa Taifa? Maana watu wabapata ukakasi kweli kulitamka hili neno (Jibu la msingi tafadhari kwa swali hilo)

BACK TANGANYIKA
 
Last edited by a moderator:
Mtafufua kila nyuzi lakini huyoo dogo yupo katika zama zake za mwisho kisiasa
 
Back
Top Bottom