Bila kujali itikadi za vyama vyetu tukubaliane sasa 'vichwa' wote waungane tutengeneze tu taifa la kizalendo lenye kulinda na kutetea maslahi ya nchi yetu na kuitii Katiba Mpya.
Tufute vyama halafu wale viongozi wa vyama wenye akili kama Zitto, Jussa, Mnyika, Mbowe, Lissu, Mdee na wengine wajumuike kuunda Serikali yenye kuleta utangamano, uzalendo na mahusiano mazuri kimataifa.
Hii nchi ni kubwa sana haiwezi kuongozwa kwa akili za CCM pekee.
Sasa hivi wanasiasa wengi walio ndani na nje ya CCM Rais Magufuli amewadhibiti juu ya maswala ya ubadhirifu na kukosa uwajibikaji. Wamekunja makucha tu wanasubiri muda wake upite wakunjue makucha waanze tabia zao za mchwa kuitafuna nchi.
Tujipange sasa kama nchi. Magufuli ametuonesha njia kwamba namna nzuri ya kuleta maendeleo ni kupiga vita ubishani wa kisiasa na badala yake tuungane kuijenga nchi.
Ameharibu baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na kuwa na mahusiano mabaya na mataifa ya magharibi na hilo linaweza kurekebishwa katika muundo wa Serikali ya Kizalendo.