Ujamaa ulitushinda, Ubepari umetushinda; sasa twende na Uzalendo

inchaji

JF-Expert Member
Jul 5, 2019
1,988
2,000
Bila kujali itikadi za vyama vyetu tukubaliane sasa 'vichwa' wote waungane tutengeneze tu taifa la kizalendo lenye kulinda na kutetea maslahi ya nchi yetu na kuitii Katiba Mpya.

Tufute vyama halafu wale viongozi wa vyama wenye akili kama Zitto, Jussa, Mnyika, Mbowe, Lissu, Mdee na wengine wajumuike kuunda Serikali yenye kuleta utangamano, uzalendo na mahusiano mazuri kimataifa.

Hii nchi ni kubwa sana haiwezi kuongozwa kwa akili za CCM pekee.

Sasa hivi wanasiasa wengi walio ndani na nje ya CCM Rais Magufuli amewadhibiti juu ya maswala ya ubadhirifu na kukosa uwajibikaji. Wamekunja makucha tu wanasubiri muda wake upite wakunjue makucha waanze tabia zao za mchwa kuitafuna nchi.

Tujipange sasa kama nchi. Magufuli ametuonesha njia kwamba namna nzuri ya kuleta maendeleo ni kupiga vita ubishani wa kisiasa na badala yake tuungane kuijenga nchi.

Ameharibu baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na kuwa na mahusiano mabaya na mataifa ya magharibi na hilo linaweza kurekebishwa katika muundo wa Serikali ya Kizalendo.
 
Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,634
2,000
[QUOTE="inchaji, post: 38350451, member: 558080",]

Tufute vyama halafu wale viongozi wa vyama wenye akili kama Zitto, Jussa, Mnyika, Mbowe, Lissu, Mdee na wengine wajumuike kuunda Serikali yenye kuleta utangamano, uzalendo na mahusiano mazuri kimataifa.
.[/QUOTE]

Yani Hawa ndo watu wenye akili , Du hii noma sana Hadi mdee, Ni heri ungemtaja TAL aliyekimbia nchi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
3,937
2,000
Kama taifa ungekuwepo uzalendo kweli hayo yangeonekana zamani ,na so habari ya uchama na maslshi binasfi.wapo wenye weledi ila wanaonekana hatari kwa maslahi ya kundi la wachache.
 
Gellangi

JF-Expert Member
Apr 11, 2016
1,941
2,000
Hakuna uzalendo mahali ambapo ukandamizaji na ubabe unatawala.
Pia uzalendo siyo kitu ambacho unaweza kulazimishwa kukifanya.Uzalendo ni moyo,utayari wa kuitetea na kuitumikia jamii/nchi kwa ukweli bila kutarajia ama kusubiri shukrani au sifa binafsi.Uzalendo ni kutumika kikamilifu kwa niaba ya watu wote bila ubaguzi wa aina yoyote.
Huu Uzalendo wa CCM Mpya wa kusifu na kuogopa kukosoana(Uchochezi/Ubeberu) ni wa kipekee sana.Mnahubiri Uzalendo huku mikononi mkibeba mapanga na misahafu!
Tuliwahi kuwaambia Katiba Mpya ya Wananchi pekee ndiyo dawa ya kutibu majeraha mliyolisababishia Taifa letu mnadai siyo kipaumbele cha Rais.Napenda kuwakumbusha kuwa Katiba siyo chombo cha Rais wala serikali Bali ni Mali na Haki ya Wananchi wa Tanzania.
Wananchi walihitaji Katiba Mpya, wakagharamia mchakato wake,mkaipindisha kwa maslahi yenu halafu mnahubiri Uzalendo?Sidhani kama huo ndio Uzalendo tunaoufahamu sisi wabishi.
Tujitafakari,Mh.Magufuli anayafanya mambo ya kizalendo kwa utashi wake au Ilani ya chama chake,itakuwaje Siku akiondoka?Atakayemrithi Naye atende kwa utashi wake?Nchi hii siyo familia binafsi na inastahili tukaweka misingi yetu kwenye Katiba ambayo Rais yeyote toka chama chochote ataifuata na kuienenda vinginevyo anatupisha bila vurugu.
Nchi ni kubwa kuliko Rais yeyote,hata Mwl.Nyerere(RIP) hakuwa mkubwa kuliko Katiba.
Tuwe wazalendo bila ubinafsi,Watanzania wote wana Haki na ni watoto wa Mungu.
 
Ikitotanzila

JF-Expert Member
Sep 22, 2020
500
1,000
Hivi mnaposema rais jpm amedhibi watu kwa ulaji mna maana gani? Mbona awamu hii ndo ulaji umekithiri sema kwa kujuana Sana na mtandao wa jpm ndo wanatafuna nchi hii.

Angalia makonda au polepole walivyo matajiri wa kutupwa sasa hivi. Msidanganywe na fix za jpm ulaji umetamalaki sasa hivi na ukabila umeongezeka Mara dufu. Ajira siku hizi ni vimemo tu wakati kipindi Cha jk ajira kila mtu ana haki ya kupata Tena bila kuomba hususani ualimu na udaktari
 
Dp800

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
1,082
2,000
Mi nimeishia hapo ulipotaja viongozi wenye akili ukamuweka na Lissu
 
Jidu La Mabambasi

JF-Expert Member
Oct 20, 2014
9,367
2,000
Bila kujali itikadi za vyama vyetu tukubaliane sasa 'vichwa' wote waungane tutengeneze tu taifa la kizalendo lenye kulinda na kutetea maslahi ya nchi yetu na kuitii Katiba Mpya.

Tufute vyama halafu wale viongozi wa vyama wenye akili kama Zitto, Jussa, Mnyika, Mbowe, Lissu, Mdee na wengine wajumuike kuunda Serikali yenye kuleta utangamano, uzalendo na mahusiano mazuri kimataifa.

Hii nchi ni kubwa sana haiwezi kuongozwa kwa akili za CCM pekee.

Sasa hivi wanasiasa wengi walio ndani na nje ya CCM Rais Magufuli amewadhibiti juu ya maswala ya ubadhirifu na kukosa uwajibikaji. Wamekunja makucha tu wanasubiri muda wake upite wakunjue makucha waanze tabia zao za mchwa kuitafuna nchi.

Tujipange sasa kama nchi. Magufuli ametuonesha njia kwamba namna nzuri ya kuleta maendeleo ni kupiga vita ubishani wa kisiasa na badala yake tuungane kuijenga nchi.

Ameharibu baadhi ya maeneo ikiwa ni pamoja na kuwa na mahusiano mabaya na mataifa ya magharibi na hilo linaweza kurekebishwa katika muundo wa Serikali ya Kizalendo.
Uzalendo ndio mode gani ya production.
 
iMind

JF-Expert Member
Mar 27, 2011
2,376
2,000
Uzalendo ndo nini? Katika awamu zilizopita wananchi waliwatuhumu viongozi si wazalendo. Ndo maana hakukuwa na maendeleo. Katika awamu hii viongozi wamejivika Uzalendo uliotukuka na kuwatuhumu baadhi ya wananchi siyo wazalendo.

Sasa nani mzalendo na nani si mzalendo inaweza ikaleta mjadala mkubwa.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom