Uingereza yalalamika kuingiliwa uchaguzi na Urusi.!

idawa

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
25,284
38,305
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May ameishutumu vikali Urusi kwa kuingilia uchaguzi wa nchi na kuendesha uhalifu wa mitandao.

Akiongea mjini London May alisema kuwa serikali ya Vladimir Putin anajaribu kuhujumu nchi zilizo huru.

Bi May alisema kuwa Urusi ilikuwa ikiunda taarifa za uongo dhidi nchi za magharibi.

Lakini akaongeza kuwa kwa sababua Uingereza haitaki makabiliano na Urusi italazimika kulinda maslahi yake.

Matamshi yake ni kinyume na yale ya rais wa Marekani Donald Trump ambaye alisema wiki iliyopita kuwa anaamini kuwa Putin hakuingilia uchaguzi wa Marekania mwaka 2015

May alisema kuwa Putin ni lazima afuate mkondo mwingine kutoka kwa ule amechukua hivi karibuni ikiwemo kulimega eneo la Crimea , mzozo nchini Ukrain na mashambulizi ya mitandao kwa serikali za nchi na mabunge kote Ulaya.

Urusi inawez kuwa mshirika muhimu wa nchi za magharibi ikiwa tu itafuata sheria, alisema May.
 
Ameanza tena kuchonga mdomo kuna kipindi Kim Jong Un alitishia
kuishambulia Austaralia kwa nyuklia Uingereza kuona mtoto anatishiwa akatoka hadharani kujihami kuwa naye atatumia nyuklia kujihami na kulinda washirika wake
Russia akamwambia akae kimya visiwa vitazamishwa kawa makombora ya nyuklia akawa ameufyata leo hii tena kaamua kumshutumu mbabe asiyekuwa na mbwembwe
 
Russia ni powerful country but haeawezi Kuwa super power sababu hawana strategies za kumpindua USA kutoka powerful country of the world
 
Wazungu buana,kulialia tu lakini huenda kuna mabaya zaidi wao wanayofanya..ila wakwanza kutaka huruma za walimwengu.
 
Jamaa wanalalamika si mchezo,

sasa bila kutumia hizo mbinu,wangempanda kichwani putin.

Ieleweke Russia ndo nchi tajiri kupita zote kwa rasilimali,mataifa ya magharibi yamekuwa yakiitolea udenda russia na kufanya mbinu zote kuingilia chaguzi zake ili waweke mtu wao,
sasa Putin akawageuzia ubao hawaishi kulalamika,
Russia ilikuwa ni empire zamani mno kabla hata marekani haijakuwepo
 
Russia ni powerful country but haeawezi Kuwa super power sababu hawana strategies za kumpindua USA kutoka powerful country of the world
marekani inalindwa na zile bahari mbili,paciffic na antlantic,
ingekuwa nayo iko bara la europe haingekuwa superpower,
wakati wa vita vya pili vya dunia ,wenzake kina uk,france;italy,russia walirudi nyuma kwa viwanda kuharibiwa na vita,
ilichukua miaka kumi kuweza kurebuild,wakati wote huo marekani alikuwa anapiga kazi na ndipo hapo alipowaacha wenzake,
na ndo maana marekani hapendi kupigana vita katika ardhi yake,anataka apiganie europe,middle east ,asia etc ili kuepuka uharibifu
 
hii leo sio propaganda za magharibi?!! teh! teh! wabongo buana kwa kupenda kushabikia wanachopenda kusikia!!
 

Similar Discussions

3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom