Uingereza yaitaka Tanzania kupinga kitendo cha Urusi kutumia kemikali za sumu

Baba Sangara

JF-Expert Member
Dec 16, 2007
293
154
Dar es Salaam. Serikali ya Uingereza imeitaka Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuiunga mkono katika kupinga kitendo cha Urusi kutumia sumu aina ya Novichok katika jaribio la kumuua Sergei Skripal na binti yake, Yulia.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita huko Salisbury, Uingereza na kwa sasa Skripal na Yulia wana hali mbaya hospitali.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, Machi 16, Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke amesema nchi yake haitavumilia majaribio yoyote ya mauaji ya watu wasio na hatia ndani ya ardhi yake.

Cooke amesisitiza kwamba ni wazi Urusi ilihusika kwenye jaribu hilo na walipewa nafasi ya kujieleza kwanini waliamua kutumia sumu hiyo ndani ya Uingereza licha ya kwamba matumizi ya kemikali kama silaha ni kinyume cha sheria za kimataifa, hata hivyo, mpaka sasa hawajatoa maelezo kuhusu suala hilo.

“Baadaye leo nitaonana na waziri wa mambo ya nje ili kumweleza kuhusu jambo hili na kuomba ushirikiano wa Tanzania. Ninaamini Tanzania iko pamoja nasi katika hili,” amesema balozi huyo katika mkutano wake na vyombo vya habari.

Mpaka sasa Uingereza inaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Austalia na Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (Nato). Pia, imeripoti suala hilo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Tukio hilo linatishia uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Urusi.

Mpaka sasa Uingereza imechukua hatua mbalimbali ikiwamo kuwatimua maofisa 23 wa intelijensia wa Urusi nchini humo. Pia, Uingereza imefuta ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov.

Vilevile, Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ametangaza kwamba hakuna waziri yeyote au mtu yeyote kutoka familia ya kifalme atakayehudhuria kombe la dunia linalotarajiwa kufanyika Juni mwaka huu huko Urusi.

Chanzo: Mwananchi

Warusi ni wapuuzi sana. Dunia ya leo assassinations zimepitwa na wakati no matter mhusika alifanya kosa gani. Anyway, tabia za madikteta ndivyo zilivyo tangu kale kuanzia na yuke wa NK, Putin, na wengineo hadi Afrika huku. Wao wanachowaza ni kuuwa kuuwa kuuwa na kujeruhi tu.
 
Msaliti hasamehewi

Urusi na China wame maintain nguvu sababu hio ku-eliminate parasites ,EU na USA dream yao ni kudhoofisha any superior country ambayo haitokani na wao ,njia pekee ya Urusi na China ni ku-eliminate betrayals ili waendelee na nguvu na kushindana na westerns kwa dunia ya sasa.Njia hizo unazoziita za kijinga kwa dunia ya sasa ndio imeifanya urusi kurise na kuwa na nguvu na ushawishi kwenye foreign affairs na North Korea kuheshimiwa na saizi anaongea kwenye meza ya mazungumzo na wakubwa ,China kuwa na ushawishi na nguvu duniani.

Western wabaki na utamaduni wao na uwerevu wao.

Ukiona nchi za EU wanakufundisha kitu au wanakuhubiria mifumo fahamu wanataka kuchukua kitu kwenye eneo hilo.Urusi haihitaji kuhubiriwa na kufundishwa na EU tuna mifumo yetu

-Vladimir Putin
 
Vilevile, Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ametangaza kwamba hakuna waziri yeyote au mtu yeyote kutoka familia ya kifalme atakayehudhuria kombe la dunia linalotarajiwa kufanyika Juni mwaka huu huko Urusi.

HII NDO MAIN POINT.
Do Russian cares
Wao wanachotaka world cup ifanyike kwao tu kwani wasipohuzuria kutakwamisha mashindano yasifanyike
 
Enheee hapa ndiyo tutaona undumilikuwili wa viongozi wetu, wasipounga mkono Itakula kwetu, wakiunga mkono maana yake tunaipoteza urusi ambayo haina mchango wowote kwenye uchumi wetu, hahahaha patamu sana hapo
 
Dar es Salaam. Serikali ya Uingereza imeitaka Tanzania na Jumuiya ya Kimataifa kuiunga mkono katika kupinga kitendo cha Urusi kutumia sumu aina ya Novichok katika jaribio la kumuua Sergei Skripal na binti yake, Yulia.

Tukio hilo lilitokea mwishoni mwa wiki iliyopita huko Salisbury, Uingereza na kwa sasa Skripal na Yulia wana hali mbaya hospitali.

Akizungumza na vyombo vya habari jijini Dar es Salaam leo, Machi 16, Balozi wa Uingereza nchini, Sarah Cooke amesema nchi yake haitavumilia majaribio yoyote ya mauaji ya watu wasio na hatia ndani ya ardhi yake.

Cooke amesisitiza kwamba ni wazi Urusi ilihusika kwenye jaribu hilo na walipewa nafasi ya kujieleza kwanini waliamua kutumia sumu hiyo ndani ya Uingereza licha ya kwamba matumizi ya kemikali kama silaha ni kinyume cha sheria za kimataifa, hata hivyo, mpaka sasa hawajatoa maelezo kuhusu suala hilo.

“Baadaye leo nitaonana na waziri wa mambo ya nje ili kumweleza kuhusu jambo hili na kuomba ushirikiano wa Tanzania. Ninaamini Tanzania iko pamoja nasi katika hili,” amesema balozi huyo katika mkutano wake na vyombo vya habari.

Mpaka sasa Uingereza inaungwa mkono na Marekani, Ufaransa, Ujerumani, Austalia na Umoja wa Kujihami wa Nchi za Magharibi (Nato). Pia, imeripoti suala hilo kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Tukio hilo linatishia uhusiano wa kidiplomasia kati ya Uingereza na Urusi.

Mpaka sasa Uingereza imechukua hatua mbalimbali ikiwamo kuwatimua maofisa 23 wa intelijensia wa Urusi nchini humo. Pia, Uingereza imefuta ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Urusi, Sergey Lavrov.

Vilevile, Waziri Mkuu wa Uingereza, Theresa May ametangaza kwamba hakuna waziri yeyote au mtu yeyote kutoka familia ya kifalme atakayehudhuria kombe la dunia linalotarajiwa kufanyika Juni mwaka huu huko Urusi.

Chanzo: Mwananchi

Sijawaelewa waingereza iweje ss watulazimishwe kuwaunga mkono kuilaani Urusi?Hii inamainisha watanzania ndo tumemwambia urusi atumie silaha za sumu au?wadau ebu tuelimishane huenda mm sifahamu haya mambo ya demokrasia za kimataifa.
 
Warusi ni wapuuzi sana. Dunia ya leo assassinations zimepitwa na wakati no matter mhusika alifanya kosa gani. Anyway, tabia za madikteta ndivyo zilivyo tangu kale kuanzia na yuke wa NK, Putin, na wengineo hadi Afrika huku. Wao wanachowaza ni kuuwa kuuwa kuuwa na kujeruhi tu.

Hujui unachoandika wewe Zuzu! Hao Waingereza ni waoga sana! Na wewe acha upuuzi zungumzia mambo unayoyajua! Wao hawana ulinzi wa kutosha? I am asking you kwa nini wakimbilie NATO Ufaransa na Marekani? Russia imewaomba watoe hiyo sample of course hawana sample kwa sababu Novichok it’s a derivative it’s not a single compound ni lazima uchanganye chemical zaidi ya mbili and it’s very lethal than sarin and VX. Baada ya kutumika kwa watu it’s very difficult to manage and death is imminent, the only difference is that it kills you slowly! Huwa antidote yake it’s time based! The big question is that wanatakiwa au wampeleke yule double agent Urusi akatibiwe ! Ndio maana wanasema hawataki kujibu kwamba ni ya kwao au la? That chemical weapon was developed in the 1980’s sasa unamhukumu mtu bila ushahidi hata mahakama ya kangaroo ya Tanzania inaweza kuona huo udhaifu wa Western Countries ! Wewe una waita wapuuzi are you mad? Wameweza kichakachua uchaguzi wa Marekani one down the road Democrats and Mr. Muller wanajiharishia and no ushahidi wa cyber !na hata France and you keep on baby sitting? Mwanaume wa vita yule. You ask the Germans they got a bloody hiding !Ukimwona simba kalowa usimuute paka we! Because you have no ability to get information from the other side unaunga mkono kama zuzu! Huyo Russian ex-spy Sergei Skripal, 66, was a snitch alikuwa double agent and he deserve death but they postponed his death so that a spy swap could take place sasa baada ya kutumia toilet paper si unatupa chooni! He is a traitor and time for payment ilikwisha fika! May be huyo binti yake (Yulia Skripal, 33, )alipewa zawadi ya vodka from Moscow anointed with one part and the other portion might have just been a piece of chocolate who knows what was the mixture. CIA and M16 who got information from him they have to crack their heads to solve the riddle! That is “Novichok” what about the invincible missile? Unachunguza wewe unahukumu wewe what a shame that portrayal of the highest degree of incompetence. Of course everybody’s life is important and equal to mine lakini let us reason carefully wale British wangefanya uchunguzi wao conclusively even using a third party and come to a credible conclusion ! Unawapa a superpower that can shake the US an ultimatum of 12 hours and expect compliance do you think Russia is a banana Republic or shithole like Tanzania! Shika adabu yako na ijishike pambafu!
 
Hii ni njama ya M15 dhidi ya Putin sababu ya kumchafulia kampeni za uchaguzi mkuu jumapili na matayarisho ya kombe la dunia litakalofanyika Moscow mwaka huu
 
Back
Top Bottom