Uingereza kuikopesha Ethiopia vitu vya makumbusho ilivyochukua miaka 150 iliyopita

Kunguru Mjanja

JF-Expert Member
Aug 22, 2012
2,036
3,927
Jumba la makumbusho la Victoria na Albert lililoko nchini Uingereza limetoa pendekezo la kurudisha kwa mkopo mali za Ethiopia zilizonyakuliwa na wanajeshi wa Uingereza miaka 150 iliyopita, ikiwa ni pamoja na taji la dhahabu, vazi la harusi la kifalme na kikombe cha divai cha dhahabu.

Pendekezo hilo lilitolewa baada ya vitu kadhaa kufikishwa kwenye maonyesho hadi mwezi Juni 2019 katika jumba hilo la maonyesho mjini London ili kuadhimisha vita vilivyotokea Maqdala mwaka 1868.

Wanahistoria wanasema ndovu 15 na nyumbu 200 walihitajika kubeba mali yote iliyoibiwa kutoka eneo la Maqdala, mfalme mkuu Tewodros II kutoka makao makuu yake kaskazini mwa nchi hiyo.

Mkurugenzi mkuu wa V&A Tristram Hunt amesema kwamba bidhaa hizo zitasalia kuwa mali ya jumba hilo la maonyesho lakini zitarudishwa nyumbani kwa ''mkopo wa muda mrefu''.

Jumba la V&A limesema vitu 20 ambavyo vinatarajiwa kupelekwa kwenye maonyesho vitawaruhusu watazamaji wapya kufahamu uzuri kwa bidhaa zao kwa mifano na utaalam mkubwa kwa ushonaji wa nguo na utengenezaji wa chuma ili kutafakari kwa kina historia ya vitu hivyo.

Baadhi ya vitu vilivyokuwa vimeshikiliwa na mataifa ya Ulaya na vimerudishwa Afrika
T anzania : Barakoa ya Makonde, iliwasili Musée Barbier-Mueller, Geneva , na mwaka 1985 ilirudishwa nchiniTanzania tarehe 10 mwaka 2010.

Afrika K usini : masalio ya Saartjie Baartman (Hottente Venus), yalichukuliwa kwenye kijiji kimoja kilichoko Afrika Kusini mwaka 1810. Lakini jumba la maonyesho la Musée de l'Homme, Paris uliurudisha mwaka 1994.

Angola: Sanamu ya ''Lwena'' kutoka ilitwaliwa na polisi wa Ufaransa katika mnada uliofanyika Saint-Germain-en-Laye, tarehe 24 mwezi Machi mwaka 1996 na kurudishwa nchini Angola mnamo 28 Oktoba, 1997.

Mali: Sanamu ya kondoo aliyokabidhiwa Jacques Chirac mwaka 1991, aliyekuwa ametwaliwa kutoka kwa wachimbuaji wa vitu vya kale nchini Mali ilirejeshwa nchini humo Januari 1998.

Bbc Swahili
 
Badala warudishe na walipe fidia, wanarudisha kwa Mkopo?????? hivi AU haiwezi kusimamia kudai Mali za Africa zilizoporwa ambazo mpaka Sasa zipo na zinaingiza kipato huko ulaya!!
 
Yaani hawna tofauti na wale wezi wa vifaa vya magari,wanakuibia wao alafu kesho enaenda Gerezani K/koo unavinunua vitu ulivyo ibiwa,kweli mzungu si mtu mzuri
 
Hata mi nashangaa, yaani mwizi wa vitu vyako anakukopesha ...Waafrika tutaamka lini? Yaani wao ndio walipaswa kuvirejesha, kulipa compensation na kuomba msamaha.

Tukitaka turudishiwe Mjuzi wetu uliyo ibiwa na Wajerumani huko Mtwara na kupelekwa Ujerumani, basi tuta ambiwa watatu azima kwa muda - tutapewa masharti kwa mali zetu za asili.!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom