Uingereza: Chris Whitty asema hakuna haja ya lockdown, wataishi na Corona kama mafua

Huko ni kuishiwa hoja mkuu, mimi hata sijakutusi.

Nasema hivi: "Mwenye akili hupima kina cha maji kwa fimbo na sio mguu".

Na kipimo cha akili ya mtu kujua ikoje ni matusi.
Huko walikochukua precautions, idadi ya vifo na wanaougua ni tofauti na huku mnakodai hatuchukui hizo precautions?
 
Huko wanakofuata hizo precautions, idadi ya vifo na wanaougua ni tofauti na huku ambako mnadai hatufuati hizo precautions?
NImekuambia huko wanakofuata precaution walifanya hivyo wakati gani! Aidha angalia nchi ambazo walishituka mapema kama vile Vietnam na hata China yenyewe! So, issue sio precautions bali mlifanya precautions wakati gani! Lakini kwa upande mwingine, Tanzania hatuna legitimacy ya kusema "wao wanakufa na kuugua zaidi kuliko sisi" wakati hata wewe mwenyewe hapo nikikuuliza over the past 1 week Tanzania kuna cases ngapi, huwezi kutoa jibu!!!
 
Huko walikochukua precautions, idadi ya vifo na wanaougua ni tofauti na huku mnakodai hatuchukui hizo precautions?

Mkuu, shida ni hii:- kina cha maji, sikuzote unapotaka kuvuka mto, huwa hakipimwi kwa mguu, ni ama utumbukize fimbo au uchukue kitu kirefu na utumbukize, Magu alitumbukiza Mguu na bahati tu mguu ukatua kwenye floor, sasa huwezi sema kwamba amefaulu katika hili.
 
Siku hizi zile thread za viongozi,mapadre,maaskofu,wahadhiri wanao kufa sizioni au nao siku hizi hawafi?

Kenya Bibi yake Obama kafa hawaja taja chanzo,nikasema wacha nisome ktk website ya BBC swahili nao hawaja taja chanzo,zaidi ya kusema kuugua kwa mda mrefu.Ila yule bibi kama ange ugulia Tanzania Wakenya,wale oya oya na wanaharakati wa mitandaoni wangesema kafa kwa Corona.

Askofu wa Uganda amekufa tu baada ya kumaliza ibada,kaenda kulala mauti ikamkuta usingizini,huyu askofu angefia Tanzania wakenya ,wale oya oya na wanaharakati uchwara wa mitandaoni wangesema kafa kwa Corona.

Kuna watu humu magonjwa mengine wanaona yapo likizo hayaui kwa sasa,kwao ugonjwa unao ua kwa sasa ni Corona.
 
NImekuambia huko wanakofuata precaution walifanya hivyo wakati gani! Aidha angalia nchi ambazo walishituka mapema kama vile Vietnam na hata China yenyewe! So, issue sio precautions bali mlifanya precautions wakati gani! Lakini kwa upande mwingine, Tanzania hatuna legitimacy ya kusema "wao wanakufa na kuugua zaidi kuliko sisi" wakati hata wewe mwenyewe hapo nikikuuliza over the past 1 week Tanzania kuna cases ngapi, huwezi kutoa jibu!!!
Ndo unauliza sasa, huko walikochukua precautions, na hapa Tz mnapodai kwamba hatujachukua hizo precautions, kuna utofauti wa idadi wa vifo?
 
Mkuu, shida ni hii:- kina cha maji, sikuzote unapotaka kuvuka mto, huwa hakipimwi kwa mguu, ni ama utumbukize fimbo au uchukue kitu kirefu na utumbukize, Magu alitumbukiza Mguu na bahati tu mguu ukatua kwenye floor, sasa huwezi sema kwamba amefaulu katika hili.
Na mimi ndio nauliza, huko walikochukua precautions na huku ambako mnadai tumepuuzia, kuna tofauti ya idadi ya vifo?

........
........
Hivi unamuoneaje wivu marehemu? Yaani we mtu kafariki halafu umuonee wivu..
 
Ndo unauliza sasa, huko walikochukua precautions, na hapa Tz mnapodai kwamba hatujachukua hizo precautions, kuna utofauti wa idadi wa vifo?
Hivi ni kipi usichoelewa?! NImekuambia huko unakosema wanachukua precautions na wenyewe walileta kiburi kile kile cha JPM, kiasi kwamba walipoanza kuchukua ilishakuwa too late! Swali unalotakiwa kujiuliza, ikiwa wanachukua precautions tu hali ipo vile, what kama wasingechukua?! Na nimeshasema Tanzania hatuna uhalali wa kujigamba kwa sababu hatujui hali halisi! Italia kwa mfano, yenye idadi ya watu karibu sawa na sisi, wanafanya testing kwa zaidi ya watu 50M. Tanzania tumepima wangapi hadi sasa? Ikiwa wakati tunapima tulikuwa hatujafikisha hata 3000 testings lakini bado kukawa na cases 560, ulishawahi kujiuliza hali ingekuwaje endapo tungepima angalau watu 5M tu?!

Nchi ZOTE zinazoonesha maambukizi makubwa na vifo vingi vinaweka takwimu in daily basis wakati Tanzanai takwimu za mwisho zilitoka mwaka mmoja uliopita!!! Sasa utajifananishaje na wao? Utafahamu vipi idadi ya vifo TZ wakati hatuweki records? Utafahamu vp maambukizo ya TZ kisha tukajilinganisha na wenzetu wakati hatufanyi testing?
 
Halafu nyie watu mna vituko ile mbaya!!! Ni kipi hicho wanachotaka kuwaiga UK?! Ni kwamba kabla ugonjwa haujaeleweka au hayo yalitokea baada ya kuona idadi ya wagonjwa ina-shoot from 52 to 509 within a week, na ili kuwajaza watu ujinga na kuficha ukweli wa ukubwa wa tatizo, ndipo akaanza kusema corona ni kagonjwa kadogo na kanaweza kutoweka kwa maombi!
Acheni kushikwa akili,katika hili ngosha alikua sahihi na leo hii wanamuiga ila hawawezi kiri sababu tu ni mtu mweusi.
Waendelee kujifungia tena ndani mwaka huu wote kama hujasikia wananchi wao kwa maelfu wameingia barabarani
 
Jibu swali nililouliza vinginevyo wewe ndo umeshikiwa akili na Ngosha! Hivi kwa akili yako UK waache kuiiga Sweden ambayo na yenyewe haikuweka lockdown halafu unaamini wanaiiga Tanzania? Nyie watu akili zenu sijui zipo vipi!!! Unajua kwavile mlilishwa ujinga na watawala, ndo mnadhani ni Tanzania peke yake ndiyo haikuweka lockdown!!! And FYI, duniani ukisikia watu wanapiga mfano kuhusu lockdown, wanaizungumzia Sweden na sio Tanzania ya Magufuli iliyojaza watu ujinga kwamba corona itatoka kwa maombi!

Halafu aliyewadanganya kwamba UK wanataka kuachana na lockdown sijui ni nani!!
 
Jibu swali nililouliza vinginevyo wewe ndo umeshikiwa akili na Ngosha! Hivi kwa akili yako UK waache kuiiga Sweden ambayo na yenyewe haikuweka lockdown halafu unaamini wanaiiga Tanzania? Nyie watu akili zenu sijui zipo vipi!!! Unajua kwavile mlilishwa ujinga na watawala, ndo mnadhani ni Tanzania peke yake ndiyo haikuweka lockdown!!! And FYI, duniani ukisikia watu wanapiga mfano kuhusu lockdown, wanaizungumzia Sweden na sio Tanzania ya Magufuli iliyojaza watu ujinga kwamba corona itatoka kwa maombi!
Kwa nini wasiige Tanzania?au ww unawaona hao wao ni almasi sana kuliko Tz.
Huu ukoloni wa kujiona nyie si bora utaisha lini?
Eeh ni kweli imetoka kwa Maombi,huko wanavaa barakoa tatu tatu na lockdown mwaka mzima lakini wanatuambia millions of people wamekufa.
Wanatushangaa sisi tunaendelea tu
 
Ripoti ambayo imetoa last week ni hii-

What are the latest rules in England?​

  • People can meet outside - including in private gardens - in groups of up to six, or as two households
  • The stay-at-home rule has ended, although the government asks that people "minimise travel"; holidays are still not allowed
  • Outdoor sport facilities can reopen, including golf courses, tennis and basketball courts, and outdoor swimming
  • Formally organised outdoor sports can restart
  • Weddings can take place, attended by up to six people
Kwa maelezo zaidi, BBC wame-outline hapa! Haya ni kipi kati ya hivyo unachoamini wameiga kutoka Tanzania?

Na kwanini wamepunguza restrictions, jibu ni hili hapa:-
UK.png

Ukiangalia hiyo curve, utaona maambukizi yanapungua!

Kwamba kwanini wasiige Tanzania, jibu ni simple! Hawezi kuwaiga viongozi mazwazwa wanaoaminisha watu uzwazwa hadi wanafikia kuweka nyungu kwenye hospitali ya taifa yenye watu ambao ungetarajia wangeongozwa na sayansi badala ya blah blah za wanasiasa!!!
 
Na mimi ndio nauliza, huko walikochukua precautions na huku ambako mnadai tumepuuzia, kuna tofauti ya idadi ya vifo?

........
........
Hivi unamuoneaje wivu marehemu? Yaani we mtu kafariki halafu umuonee wivu..

Shida ni hii kwamba huwezi kupima kina cha maji kwa kutumia mguu.

Hii inafanana na historia moja ambapo askari wawili walipewa mtihani wa kuvuka eneo lililokuwa limepandwa mabomu (landmines), askari mmoja akaanza kuvuka tu kwa ujasiri na kwa bahati akavuka salama lakini yule mwingine akachukua metal detector instrument akaitanguliza kila mahali alipokuwa akikanyaga na akavuka salama japo alichelewa kuvuka kulinganisha na yule askari wa kwanza.

Tz tulikuwa kama yule askari wa kwanza na nchi zingine zilikuwa kama yule askari wa pili aliyetumia metal detector.

Yupi mwenye akili katika hao askari???.
 
Hivi ni kipi usichoelewa?! NImekuambia huko unakosema wanachukua precautions na wenyewe walileta kiburi kile kile cha JPM, kiasi kwamba walipoanza kuchukua ilishakuwa too late! Swali unalotakiwa kujiuliza, ikiwa wanachukua precautions tu hali ipo vile, what kama wasingechukua?! Na nimeshasema Tanzania hatuna uhalali wa kujigamba kwa sababu hatujui hali halisi! Italia kwa mfano, yenye idadi ya watu karibu sawa na sisi, wanafanya testing kwa zaidi ya watu 50M. Tanzania tumepima wangapi hadi sasa? Ikiwa wakati tunapima tulikuwa hatujafikisha hata 3000 testings lakini bado kukawa na cases 560, ulishawahi kujiuliza hali ingekuwaje endapo tungepima angalau watu 5M tu?!

Nchi ZOTE zinazoonesha maambukizi makubwa na vifo vingi vinaweka takwimu in daily basis wakati Tanzanai takwimu za mwisho zilitoka mwaka mmoja uliopita!!! Sasa utajifananishaje na wao? Utafahamu vipi idadi ya vifo TZ wakati hatuweki records? Utafahamu vp maambukizo ya TZ kisha tukajilinganisha na wenzetu wakati hatufanyi testing?
Labda nikuulize kivingine, kwa mujibu wa data za wasajili wa vizazi na vifo(RITA), idadi ya watu waliokufa kabla ya Corona kwa mwaka na idadi ya watu waliokufa baada ya corona kwa mwaka, ina utofauti?
 
Shida ni hii kwamba huwezi kupima kina cha maji kwa kutumia mguu.

Hii inafanana na historia moja ambapo askari wawili walipewa mtihani wa kuvuka eneo lililokuwa limepandwa mabomu (landmines), askari mmoja akaanza kuvuka tu kwa ujasiri na kwa bahati akavuka salama lakini yule mwingine akachukua metal detector instrument akaitanguliza kila mahali alipokuwa akikanyaga na akavuka salama japo alichelewa kuvuka kulinganisha na yule askari wa kwanza.

Tz tulikuwa kama yule askari wa kwanza na nchi zingine zilikuwa kama yule askari wa pili aliyetumia metal detector.

Yupi mwenye akili katika hao askari???.
Sasa kuna ugumu gani basi wa kumpa heshima zake kwa umahiri wake, marehemu JPM? Wivu wa nini sasa hadi uite bahati? Kwanini tu usikubali kwamba alitumia common sense na alikuwa na maono?
Labda nikurahisishie hili swali, kwa mujibu wa Data za za wasajili wa vizazi na vifo (RITA), idadi ya watu waliokufa kabla na baada ya ujio wa Corona, ina utofauti? Ukishajua hili, nduo utafahamu kama alitumia common sense au ilikuwa bahati
 
Labda nikuulize kivingine, kwa mujibu wa data za wasajili wa vizazi na vifo(RITA), idadi ya watu waliokufa kabla ya Corona kwa mwaka na idadi ya watu waliokufa baada ya corona kwa mwaka, ina utofauti?
Are you serious?! We unazo hizo data?! Ni vifo vingapi Tanzania vinakuwa recorded na hao RITA? Unazungumzia watu wanaotafuta death certificate kwa ajili ya urithi ndo iwe reference yako?! Anyway, mimi sina hizo data labda wewe ndo utuwekee hapa! Lakini hata ukiziona sidhani kama utaweza kufahamu ni vifo vingapi vimetokana na corona!! Hivi unajifanya umesahau kwamba serikali na taasisi zake imebadilisha hata hilo jina la corona na kuita changamoto ya kupumua, au?! Ni mara ngapi, kwa kutotaka tu kutumia neno corona/covid-19 serikali imekuwa ikisema "magonjwa ya kupumua ambayo yapo tangu zamani"?!
 
Basi nadhani, no research, no right to speak, kaa kimya, acha kutupigia kelele, research kwanza.
 
Sasa kuna ugumu gani basi wa kumpa heshima zake kwa umahiri wake, marehemu JPM? Wivu wa nini sasa hadi uite bahati? Kwanini tu usikubali kwamba alitumia common sense na alikuwa na maono?
Labda nikurahisishie hili swali, kwa mujibu wa Data za za wasajili wa vizazi na vifo (RITA), idadi ya watu waliokufa kabla na baada ya ujio wa Corona, ina utofauti? Ukishajua hili, nduo utafahamu kama alitumia common sense au ilikuwa bahati

Heshima kwa jambo lipi???, watu wengi wanekufa kutokana na Corona na akawazuia watu kuita Corona bali matatizo ya upumuaji, mtu ukitangaza Corona tu basi unalo, watu tukakosa uhuru wa hata kujisema kwamba unaumwa Corona, dunia ikadanganywa kwamba Tz hakuna Corona huku watu tukiteketea.

WHO ikahitaji takwimu za Corona TZ wakanyimwa, kifupi tulikuwa tunaelekea kuwa a failed state kama North Korea lakini Mungu si Athumani kasikia kilio cha Watz, watz tulikuwa kama mbuzi chini ya huyo mchungaji aliyetupelekesha atakavyo akijiita eti kiongozi wa Malaika mara Jiwe nk, alijiona kama Mungu mtu asiyeambilika na kusikia chochote kutoka nje, yeye ni yeye akiamka na chochote akilini mwake basi ataamrishwa kifanywe.

Mtu mvurugaji wa aina hiyo anahitaji heshima gani???.
 
Ndivyo unavyojidanga wewe siyo? Una ule ujinga wa kudhani ugali ndiyo chakula chenye nguvu. Unajua life span ya wazungu vs sisi? Wenzako karibu wanamaliza nchi nzima kuchanja.
We mwenzangu unajidanganya zaidi.hiv unaelewa uhalisia wa hizo chanjo zenyewe.unawajua hao wanaoendesha hiyo kampeni ya covax.

Tafuta taarifa sahihi.mimi sikuwa namkubali Hayati,lakini kwa hili la chanjo nilimkubali sana.

Waulize hao wanao hamasisha hizo chanjo je ,itakuwa ni mwisho wa kuvaa barakoa na socialdistance baada ya chanjo.

Umesema wamekaribia kumaliza kuchanja watu wao,unauhakika gani chanjo inayotolewa ndiyo hiyo hiyo utakayoletewa wewe,pili unajuaje kama ni chanjo ya covid
 
Back
Top Bottom