Uimara wa Uchumi na kuachana na manyanyaso ya kisiasa ndiko kutakakoisalimisha Pemba.

maramia

JF-Expert Member
Jul 17, 2015
2,030
1,345
Kusema kweli sasa naanza kuwaonea huruma wananchi wa kisiwa cha Pemba kwa sababu naamini hakuna watakachojiamria kikaamrika bila Tanzania bara kupenda.

Kwa sababu wamebanwa kila upande, kutoka Unguja, kutoka viongozi wa juu wa bara, kutoka viongozi wa juu wa serikali ya JMT kutoka Pemba kwenyewe, kutoka CCM na kutoka vyama vya upinzani wenzake na CUF, hivyo sioni mahala salama pa wapemba hawa kuweza kupumulia.

Kwa msemo wa wahenga "Adui yako akikushinda ungana naye" nadhani ifike mahala wapemba wawe wapole kwa sababu kama ni siasa hizi za kiafrika wataendelea kupiga kelele mpaka mwisho wa dunia na hakuna watakachoambulia, Pemba itakuwa sawa na Palestina kwa Israel na migogoro isiyoisha.

Kwa vile upinzani ulishindwa kuiangusha CCM kwenye uchaguzi wa 25 Oktoba CCM ilipokuwa legelege, sioni tena uwezekano wa vyama vya upinzani kuiangusha katika kipindi cha miaka 20 ijayo. Kwa hiyo busara ya kawaida ni kwa serikali ya JMT kupitia kwa Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuuimarisha uchumi wa Pemba, kujenga mahusiano mazuri na kuwahudumia wapemba kwa moyo wa kindugu. Na kwa kufanya hivyo nina imani wapemba watarudi kwenye msitari kwa kuona kuendelea kuitegemea CUF ni kupoteza muda maana kwa jinsi ilivyodhibitiwa ni kazi bure kuitegemea.
Ikibidi wataamua kujisalimisha CCM.
 
Na iwe mpaka kiyama CCM haitotakiwa Pemba na Unguja yake ,na kama kuwaonea huruma basi waonee hao waliojipachika misalaba na minyororo kwenye shingo zao, si umewasikia wengine wameshaanza kuweweseka ,eti CUF ni chama kikubwa na hakikushiriki na sisi tulioshiriki hakuna hata mmoja alieambulia asilimia kumi kwa maana hio hatuwezi kutoa makamo angalau tungeambulia muwakilishi ,na mambo bado si Unguja si Pemba CCM haikuchaguliwa na Mzanzibari yeyote yule ,hilo naliaminia kabisa ,kwa sababu yaliyotangazwa sio yaliyotokea kwenye visanduku ,ni aibu na subiri utayasikiaa na wenyewe watayatumbua,

Haya subirini Raisi wa Zanzibar atakuja kuwatembelea Tanganyika mzidi kudumisha muungano na ikibidi ile ahadi ya kuelekea serikali moja isipite miezi sita.
 
Pemba ikikosa utulivu wa kisiasa hata huyo Shein hatatawala kwa amani. Wapemba hawaepukiki.
 
Back
Top Bottom