Uimara wa Rais Magufuli na uthabiti wa ngome ya Andrew Chenge bungeni ni siri iliyojaa nyufa

Mwabhleja

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,351
2,061
"Mhe. Magufuli aina ya kiongozi anayestahili kukiongoza Chama Cha Mapinduzi (CCM)" Hii ni sehemu ya kauli aliyoitoa Prof. Mark Mwandosya mwaka jana akieleza zaidi kwamba hajawahi kuwa hata Mwenyekiti chama ngazi ya shina.

Pamoja na hayo, ni dhahiri Mhe.Magufuli amethubutu kuonyesha nia ya kuondoa ombwe la uongozi serikalini lakini bado haibatilishi ukweli kuhusiana na misimamo tofauti waliyonayo vigogo, washauri na wadau muhimu wa CCM hususani wafanyabiashara wakubwa.

Inasadikika kuwa, CCM Original walibaini mapema kuingiliwa kwa maslahi ya chama na serikali ikiwemo kubanwa kwa wafabiashara ambao ni wafadhili wakubwa wa chama jambo ambalo halisadiki sana Mhe.Magufuli. Hicho ndicho kilikuwa kiini cha Mhe.Chenge kukabidhiwa kiti cha heshima bungeni licha ya kujaa tuhuma rushwa na ufisadi.

Hii ina maana kwamba endapo Mhe. Magufuli atatingisha kibiriti cha chama kinacholindwa na Mtemi Chenge serikali yake itadhibitiwa na Team CCM Original na pengine kupoteza mwelekeo.

Je, Magufuli ataivana na Mhe.Chenge?
 
JPM akienda kwa mwendo wa dini, kabila na ukanda anaweza akaendana na Mtemi Chenge. Lakini akienda kwa HAPA NI KAZI TU, Kazi itafanyika na Mtemi Chenge hataweza kuyumbisha Mkuu wa nchi na Amri Jeshi Mkuu wa Majeshi yote.
 
Kila kitabu na mda wake. Chenge zama zake zimekwisha. Atulie afanye mambo yake. He is no longer needed in public service!
 
Mwisho wa siku kwa Tanzania Amri jeshi mkuu analindwa na kusaidiwa na vyombo vyote vya ulinzi na usalama ....HAKUNA wa kushindana na hili ....hao mafisadi original wanajua hili na RA aliwahi kukiri "siwezi kushinda na Amri jeshi mkuu"
 
Mwisho wa siku kwa Tanzania Amri jeshi mkuu analindwa na kusaidiwa na vyombo vyote vya ulinzi na usalama ....HAKUNA wa kushindana na hili ....hao mafisadi original wanajua hili na RA aliwahi kukiri "siwezi kushinda na Amri jeshi mkuu"
Rost tamu wa azizi....Yu wapi huyu Muajemi? Siku nyingi.Kapotea kama Mukama aliyemukamua...
 
Ndo kwanza kumekucha, aliyesema mi mpiga ramli akae mkao wa kuelewa
 
Back
Top Bottom