Uhusika wa waandishi wa habari kwenye vifo vya watanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhusika wa waandishi wa habari kwenye vifo vya watanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Nyalotsi, Jan 28, 2012.

 1. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #1
  Jan 28, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  Ikumbukwe kuwa hili suala lilianza kwa interns waliofukuzwa muhimbili kuhitaji warudishwe lakini serikali ikadinda. Na tarehe 19 mat kwenye kikao chao wakaiagiza serikali kuwarudisha interns wote bila masharti yoyote vinginevyo wangetangaza mgogoro na serikali kutokana na kuwa na madai mengi ambayo haijayatimiza.

  Hii ndiyo siku ambayo wao waliambiwa wasiingie kwenye kikao kwani wataletewa kilichojadiliwa ili waripoti,wakachukulia wamedharauliwa na kuacha kutangaza habari hizo. Kwenye vikao vya vyama hata wakifukuzwa huwa wanawatumia hata walio ndani kutafuta habari. Tar 20 mat wakatangaza mgogoro na serikali na kuendelea na vikao vyao visivyo na kikomo,hapa wakaingiza na madai mengine yanayohusu utendaji wa kazi na maslahi yao.

  Hii ndo siku ambayo huduma mnh na haspitali za jirani zilianza kuzorota na ndo siku ambayo naibu waziri aliwakwepa madaktari na kuwaamuru wafike kwenye ukumbi aliosema yeye una usalama ndani ya nusu saa. Kulikuwa na watu zaidi ya 500 ukumbini,kuondoka pale kuelekea ukumbi uliotajwa wangeonekana wanaandamana hivyo kuitiwa polisi na kuambiwa wanaandamana bila kibali.

  Ni magazeti machache na mlimani tv na bbc ndio walitoa uhalisia wa nini kinaendelea kwenye utoaji wa huduma,wengine wote waliripoti kwamba huduma zinaendelea kama kawaida bila hata kufanya uchunguzi.

  Siku zikasogea mpaka tar 24 ambapo mgomo rasmi ukatangazwa na vyombo vya habari vingi kesho yake wakatangaza kwamba mambo yako safi. BBC walitoa hali halisi na kufikia kuwahoji watendaji wa wizara kwa kile kinachoendelea Wizara ya afya ikawa inawaita na kuwapa taarifa za uongo na bila kuzichunguza wao wanaripoti kama zilivyo.

  Hali ilipozidi kuwa ngumu ndipo wakaanza kutangaza hali halisi ndo wizara ikaanza kutafuta suluhu baada ya watu wengi kufa au kupata vilema. Kumbukeni mgomo wa wafanyakazi hautokei ghafla kbma wanachuo wanaokutana sehemu moja na kuanandama barabarani. Delay ya response na majibu ya dharau ya wizara yalitokana na wao kutosema hali halisi ya huduma hospitali.
   
Loading...