George Kahangwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2007
- 547
- 147
Wakuu,
Mojawapo ya masuala ya kiuongozi ambayo yamegusiwa sana hivi karibuni, ni uwezo wa mtu kuongoza. Wapo wanaohoji endapo kuna uhusiano kati ya umri alionao mtu na uwezo wake wa kuongoza. Jambo hili limegusa hata mijadala ya nini kiwemo katika katiba mpya tarajiwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kwamba pengine kwa mfano, umri wa mtanzania kuruhusiwa kugombea nafasi ya juu kabisa ya uongozi nchini, unaotajwa katika katiba ya sasa, upunguzwe, uongezwe au ubakie vile vile. Sijasikia sana hoja zikijengwa kwa misingi ya kisayansi. Nimepata hata kumsikia mwanasiasa mmoja (jina naomba nisimtaje), akidai kwamba hakuna ushahidi wowote wa kisayansi kwamba umri una uhusiano na uongozi. Ni kiasi gani mwanasiasa huyu na watanzania kwa ujumla tumefanya pitio la tafiti zilizokwishafanyika kuhusu suala hili, sijui. Ni kwa sababu hiyo, natoa hoja hapa jukwaani kwamba hebu tafiti na zituambie kitu, ili hatimaye tukifanya maamuzi tusibahatishe au 'tusiingie mkenge'.
Baadhi ya maandiko ya watafiti yanaonesha kwamba, viongozi wenye umri mkubwa wamekomaa, wanatambua changamoto kwa wepesi, na wana mitazamo inayoona mbali katika kuongoza watu. Hii ni tofauti na vijana zaidi ambao sifa yao kubwa wana ari ya ushindani (soma kwa mfano; Kakabdse, 1999; Mitchell, 2000; Kabacoff & Stoffey, 2011).
Tafiti pia zimeonesha kuwa viongozi wenye umri mkubwa hutumia zaidi autokrasia katika kufanya maamuzi ya mwisho. Hata hivyo katika mchakato wa kuelekea kuamua, hupenda kuwauliza na kutafuta ushauri wa waongozwa, na utendaji wao ni wa ushirikishaji, kuliko viongozi damu changa. Lakini, wenye umri mkubwa na vijana hawatofautiani katika viwango wa kutumia mfumo wa uongozi wa 'ruksa' (rejea; Maciejewski na wenzake, 2012).
Pengine changamoto tuliyonayo watanzania, ni kufanya tafiti katika muktadha wa nchi yetu. Matharani kwa kuwachunguza viongozi wetu vijana na wale wa umri mkubwa. Kundi gani ni bora katika kipengere kipi, na akina nani ni ovyo katika uwanja upi.
Naomba kutoa hoja/kuchokoza mada.