Keynez
JF-Expert Member
- Feb 12, 2007
- 2,397
- 3,884
Huwa napenda kuushughulisha ubongo wangu kwa fikra mbalimbali, nikiwaza na kuwazua mambo kwa muda wa kutosha kabla sijaongea lolote. Ruksa kutofautiana na mimi kimtazamo.
Rais Kikwete alikuwa na maelewano mazuri sana na wale ambao leo wanaitwa 'Mabeberu'. Ukaja uchaguzi wa 2015 wakasema Kikwete ametoa jina la Magufuli kutoka mfukoni. Ikaonekana kama Magufuli amepata Urais kwa bahati-bahati tu lakini sidhani kama ilikuwa ni bahati-bahati kama wengi mnavyodhani.
Nitajikita katika kujibu swali moja. Je maslahi ya 'mabeberu' yameathirika kiasi gani katika utawala wa Magufuli kulinganisha na kipindi cha Kikwete?
Let us follow the money.....
Ukweli ni kuwa maslahi ya mabeberu siyo tu yamelindwa kwa kiasi kikubwa lakini pia yameboreshwa kipindi cha utawala wa Rais Magufuli.
Ndege, Ununuzi wa ndege mpya kwa ajili ya ATCL unaingiza si kiasi kidogo kwenye makampuni ya mabeberu huko Canada. Tena sisi tunalipa kwa CASH MONEY hakuna mambo ya kulipana kwa miaka 20 hapa!!
Madini, Wakati wengine wanashangilia songombingo lile la Acacia, dili mpya linaweza kuwa na manufaa zaidi kwa kampuni ya Barrick kuliko hata mkataba wa zamani.
Kwa kuongezea, hivi mmewahi kujiuliza nchi zingine ambazo nazo zilikuwa chini ya Acacia Mining yaani Kenya, Burkina Faso na Mali mbona hazikuwa zinapiga kelele kama sisi? Je wao wameathirika vipi na dili mpya au wamechukua direction ipi ya kibiashara na Barrick baada ya Acacia kufa?
Bagamoy,. Mahusiano yaliyopo kati ya Marekani na China yanaathiri maamuzi ya kiuchumi pia katika nchi zilizoko nje ya nchi zao husika. Mkataba mkubwa wa bandari ya Bagamoyo ungeipa China fursa na access kubwa ya kibiashara katika ukanda huu. Magufuli amekuja ameupiga stop.
Sitashangaa huu mkataba ukaja kubadilishwa ili Mabeberu wawe pia sehemu ya mkataba pamoja na China.
Usalama, Mabeberu huwa wana mtindo wa kusupport au kufumbia macho matendo ya viongozi wanaoonekana kupigiwa kelele kama viongozi wale watafanya mambo yanayowapendeza. Sera za Mabeberu zimejikita kwenye mambo makuu mawili - Access na Stability na Magufuli bado anawapa vyote hivyo kwa adabu na heshima.
Kwa kuwa zama hizi tumerudi nyuma sana kwenye uwazi serikalini, mengi yanayofanyika hayajulikani wazi. Imefikia hadi viwanja vya ndege vikubwa vinajengwa na haijulikani hela imetoka wapi, manunuzi yamefanyikaje, wapi vilijadiliwa, nk.
Mwana historia maarufu wa Marekani Noam Chomsky aliwahi kuandika kuwa Marekani wana zaidi ya military bases 800 duniani. Sijui toka ameandika hivyo kama idadi hiyo imeongezeka au kupungua.
Hizi bases zinatofautiana ukubwa na mifumo yake. Baadhi zinajulikana na baadhi zinahisiwa (suspected). Baadhi zina wanajeshi wa special operations na baadhi zinatumika tu kwa ajili ya drones na surveillance flights.
Wengi wamejenga mitizamo yao kuhusu uhusiano wa mabeberu na Rais Magufuli kwa kuangalia sababu zisizo na uzito sana. Mfano, Rais Magufuli kutozitembelea nchi hizo za Mabeberu, au kauli za kisiasa za majukwaani, au nyaraka za kibalozi ya 'kutoridhishwa na hili au lile' lakini mwisho wa siku ni muhimu turudi kwenye FACTS.
Ni muda tu kabla hatujajua ukaribu au umbali wa serikali ya Rais Magufuli na Mabeberu uko vipi lakini usidharau uwezekano kuwa Rais Magufuli ana sapoti yote ya Kikwete kwa yote ayafanyayo.