Uhusiano wa Njaa iliyopo na mahindi yaliyokauka kipindi hili.

Rodney01

JF-Expert Member
May 14, 2013
827
829
Habari zenu wakuu?ni kweli katika kipindi hiki kumekuwa na upungufu wa mvua ktk baadhi ya maeneo ya nchi na hivyo kupelekea mazao mengi kunyauka tena hasa mahindi

Kulingana na uelewa wangu kuhusu zao hili la mahindi huwa linavunwa mwezi wa tano na wa sita tu katika mwaka ingawa kuna baadhi ya maeneo ambayo huwa wanapanda sehem zenye unyevu nyevu kama pembezon mwa mito na huvuna kipindi cha kiangazi lkn mavuno yanakuwa na madogo sana ambayo hayawezi kuwa tegemeo.

Nashindwa kuelewa kunauhusiano gani kati ya haya mahindi machanga yaliyokauka shamban kwa sasa na njaa iliyopo kwasasa kwamaana hata kama kungekuwa na mvua basi mavuno yake yangekuwa mwezi wa tano na wa sita,hivyo basi upungufu tulionao sasa hv unatokana na mahindi machache ambayo tuliyavuna mwaka Jana.

Sasa ni nani aliyetuamunisha kuwa njaa ya sasa hv inatokana na kukauka kwa mahindi haya machanga yaliyokauka mashambani kipindi hichi?ni nani anayepotosha watu?anafanya hivyo ili kumkomoa nani?
 
Back
Top Bottom