Uhusiano wa elimu ya darasani na uhalisia wa maisha

loupa

Senior Member
Jul 22, 2016
124
78
Eti wadau elimu anayopata mtu darasani inamfanya mtu kufikia malengo? Au kuwa na maisha mazuri? Maana wengi waliosoma maisha yao ni ya kuunga tu.
 
Elimu ya Darasani msaada wake ni hukohuko class! Watu hawafikirii,wanasoma halafu wanataka waajiriwe ila wangejua idadi ya watu wanaomaliza chuo kila mwaka halafu wote waajiriwe hiyo haipo dunia nzima.
 
TeamKUJILIWAZA Poleni.
IMG_20170307_094432.JPG
 
Wanaofanikiwa maishani ni wale wenye elimu ya msingi ambayo hii inatoka kwa wazaz toka ukiwa tumboni,,,

Elimu ya darasani inakufundisha tu uwajibikaji,,haina kazi nyingine zaid ya kuwajibika
 
Eti wadau elimu anayopata mtu darasani inamfanya mtu kufikia malengo? Au kuwa na maisha mazuri? Maana wengi waliosoma maisha yao ni ya kuunga tu.
Acha kitu inaitwa elimu ni muhimu tofauti na unavofikiria, ukiona mtu hafaidiki na elimu yake ujue kuna tatizo mahali, wewe siku utakayoona mishahara ya maexpert utaenda kurudia form two.
 
Eti wadau elimu anayopata mtu darasani inamfanya mtu kufikia malengo? Au kuwa na maisha mazuri? Maana wengi waliosoma maisha yao ni ya kuunga tu.
Fanya utafiti mdogo. Angalia na kufananisha kwenye ukoo wenu walioenda shule na wasioenda shule, jibu utalipata. Kama wewe umeenda shule kidogo angalia nyuma wale wenzako walioishia darasa la saba na upime. waswahili husema kama elimu ni gali jaribu ujinga uone. Bado inabaki elimu ni ufunguo wa maisha uwe umaeajiriwa au kujiajiri. Shule itakufanya utumia nguvu kidogo akili nyingi, wakati ukilaza utakufanya utumie nguvu nyingi akili kidogo.
 
Back
Top Bottom