Uhusiano wa chama cha mapinduzi na majeshi yetu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhusiano wa chama cha mapinduzi na majeshi yetu

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzito Kabwela, Jan 7, 2010.

 1. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Mwenyekiti.......Luteni Kanali Jakaya Kikwete
  Katibu Mkuu......Luteni Yusuph Makamba
  Katibu Itikadi.....Capteni George Mkuchika

  Wapo 1. Brigedia Gen. Hassan Ngwilizi
  2.Kanali Abdulrahman Kinana
  3. Kanali Anatori Tarimo
  4. Kanali Simbakalia
  5. Kanali Enos Mfuru
  6. Kapteni James Yamungu
  7. Luteni KANALI Issa Machibya
  8
  9
  and so on.....
  Hivi Karibuni nilisikia kua Mzee Mhita ambaye ni former IGP akikanusha kutaka kugombea Ubunge kwa tiketi ya CCM (Hakukana uanachama ila amekana kugombea Ubunge)

  Tibaigana naye nasikia anataka ubunge huko kwao Kagera.

  List ni ndefu...Ninachojiuliza mimi ni hiki...

  Majeshi yetu ni Mashina ya Wakereketwa wa CCM?

  Na kama hali ni hiyo, hatuoni kuwa sio rahisi kwa jeshi letu kukubali ushindi wa chama kikingine (kwenye nafasi ya Urais ikitokea) mbali na CCM?

  Kama ni hivyo, hatuoni kuwa sisi tunaotaka mageuzi tunapoteza muda kujaza threads wakati piga ua upinzani hautashika nchi?

  Demokrasia ipo wapi?

  I stand to be corrected endapo nitakuwa nimepotoka....
   
 2. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2010
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Mzittokabwela,kimtizamo upo sawa ila majeshi yetu kabla ya mwaka 1992,yalikuwa chini ya chama tawala na ilikuwa ili uajiriwe huko ni lazima uwe mwanachama wa YOUTH LEAGUE AU TANU,ASP/CCM.Hivyo hawa waheshimiwa walilelewa hivyo.Baada ya vyama vingi majeshi yote yalitolewa kwenye siasa kwa maana ya hakuna mwanajeshi kuwa na kadi za chama chochote cha siasa lakini waliokuwa na kadi waliambiwa ama waziweke kwenye kumbukumbu zao za utumishi ili wakistaafu waweze kuendelea na siasa au wazichane.Pia ktk wanajeshi hao hasa JWTZ kulikuwa na makada wa CCM ambao tofauti na wanachama wa kawaida,wao walikuwa wanahamasisha na kukiimarisha chama,hao waliambiwa na CCM ama wachague siasa au UANAJESHI ndipo JK na baadhi wakaacha/kustaafu jeshini na kuingia zaidi kwenye siasa.
  Kuna ambao wameteuliwa kwenye nyadhifa za kisiasa wakiwa hawajastaafu kwenye jeshi,hapo nadhani ndio makada ambao hawakuchana kadi zao na RAIS AMEONA WANAMFAA KWENYE NYADHIFA HIZO.
  Nadhani kuna kanali mmoja likuwa chadema baada ya kustaafu.
   
 3. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu heshima mbele sana, naomba kukuuliza hivi jeshi letu lina wanajeshi wangapi? Maaana uliowataja kwangu ni namba ndogo sana kulinganisha na ukubwa wa jeshi tulilonalo yaani JWTZ, unless kuna something sielewi hapo!

  - Halafu by the way tunaongelea jeshi lipi hilo ambalo Tibaigana na Mahita wamewahi kulishiriki?

  Respect.


  FMEs!
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Mkuu, kwenye title nimesema Uhusiano wa MAJESHI sio JESHI

  Kikubwa hapa ambacho ndicho hasa kinanipa mashaka ni kuwa wote wanaotajwa ni Luteni, Knali, Brigedia,Capteni na Hata General Mboma naye alitaka kugombea Ubunge Mbeya vijijini. Unaweza kuona iwapo watu influential wa rank hizo ni viongozi waandamizi wa chama hawa wengine unaowasema wako weeeengi (nakubali kuwa wapo wengi) watawajibikaje kwenye kulinda demokrasia (iwapo watatakiwa kufanya hivyo) wakati mabosi wao tayari intrests zao zipo CCM
   
 5. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2010
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,523
  Likes Received: 1,704
  Trophy Points: 280
  Code:
  
  
  Code:
  
  
  Mimi nadhani, kwakuwa vyeo vyao ni vya kisiasa sana na karibu vyone ni vya kuteuliwa (sio vya kupigiwa kura) kulikuwa na haja ya hao wateuaji kuacha kabisa kuwateua wanajeshi ili kuifuta hiyu dhana kwamba CCM ni chama kinachohusiana na MAJESHI yetu. Tukumbuke kuwa majeshi yetu yapo kwa Mujibu wa KATIBA il hali CCM ipo kwa mujibu wa SHERIA!
   
 6. Facts1

  Facts1 JF-Expert Member

  #6
  Jan 7, 2010
  Joined: Dec 23, 2009
  Messages: 308
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni namba ndogo sawa lakini kwanini wote wawe serikalini ma-DC, ma-RC mawaziri, Makatibu wakuu wengi ni wanajeshi nk ina maana hiyo sehemu ndogo ndiyo yenye uwezo zaidi ya raia wengine?

  Katika suala la uhusiano wa Majeshi na CCM, katika mwonekano wa nje kikatiba majeshi yanatakiwa si kwamba yawe neutral ila yasijihusishe na siasa kabisa maana neutral ni relative term. Lakini kinyume chake ndicho tunachokiona, siombei vita lakini historia inaonesha kuwa vyama vya upinzani hukumbukwa zaidi wakati wa vita, majeshi huhitaji msaada pia toka kwa upinzani na historia inaonesha kuwa vyama vya upinzani huwa havina kinyongo.

  Kuhusu ni jeshi lipi mimi nafikiri amesema majeshi yote inclusive TPDF , Polisi, JKT, Magereza nk.
   
 7. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #7
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  haya mambo ni historical tu, yataisha. umesahau historia a siasa yetu ilikotokea?
   
 8. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #8
  Jan 8, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Kaka hawa si wanajeshi by Professional, hawa waliingia tu CTU Monduli intake maalum ya chama cha mapinduzi at that time kama makada wa chama cha mapinduzi.

  JK alikuwa anafundisha Siasa na kina Makamba na Mnauye walikuwa vinara wa kutunga nyimbo za uhamasishaji.

  Mwana JF aliyekuwa intake moja ha hawa makada anaweza kumwaga hapa jamvini.
   
 9. pius-ndiefi

  pius-ndiefi Member

  #9
  Jan 8, 2010
  Joined: Dec 11, 2009
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Code:
  
  
  Code:
  
  
  Msirahisishe mambo namna hiyo. Viumbe hawa ni very influential. Acheni utani nyinyi....Na General Mboma aliyeutaka Ubunge Mbeya mjini naye alikuwa mhamasishaji? List ya wana CCM wanajeshi ni kubwa mno, inagusa hadi hawa walioingia nineteen ninety!
   
 10. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #10
  Jan 8, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Demokrasia ndiyo nini? hata marekani wanaomchagua Rais wao ni watu kama mia tano hivi. Uliwahi kusikia kuna uchaguzi wa head of state au uchaguzi mkuu china?

  Hiyo ndiyo demokrasia ya bongo. hata wapinzani ni wana ccm sawa na viongozi wa klabu zingine za mipira utakuta either ni shabiki la yanga au simba.
   
Loading...