Uhusiano wa CHADEMA, Tundu Lissu na Ubelgiji: Kwanini Tundu Lissu alikimbia ubalozi wa Ujerumani?

Leslie Mbena

Verified Member
Nov 24, 2019
207
1,000
UHUSIANO WA CHADEMA, TUNDU LISSU NA UBELGIJI: KWA NINI TUNDU LISSU ALIKIMBILIA UBALOZI WA UJERUMANI?​

Leo 20:30hrs 14/11/2020

Ilani ya CHADEMA ikinadiwa na mgombea wao wa Urais, Tundu Lissu, walizunguka Tanzania nzima wakipiga mbiu kuwa watatumia rasilimali za madini kama dhamana kwa ajili ya kugharamia huduma za kijamii na maendeleo ya wananchi wa Tanzania, kwa maneno mengine, CHADEMA wangegawa bure madini yetu kwa Wabelgiji ili Wabelgiji wafidie madini hayo kwa kutoa fedha za mkopo wenye riba ili kuboresha huduma za jamii kama maji, afya, elimu na kadhalika, ilihali tukishindwa kulipa basi migodi yetu yenye Madini inakuwa ya Wabelgiji,

Ndugu zangu Watanzania, sera na hoja iliyo katika ilani ya CHADEMA inawafedhehesha watanzania kama watu ambao hawawezi kujisimamia kwenye mambo ya msingi kama huduma za jamii, kitu ambacho si kweli, kwa maana tumeona Mh Rais John Magufuli amejenga Zahanati na vituo vya Afya 400 akigusa kila kata na Wilaya, Mh Rais John Pombe Magufuli amefufua Shirika la Ndege la ATCL na amenunua Ndege kubwa mpya kumi na moja na ndege tano ameziagiza, Mh Rais John Magufuli amejenga barabara, Madaraka ya majini na kutengeneza meli kubwa mpya tano katika Ziwa Tanganyika, Ziwa Victoria na Ziwa Nyasa, Je sera za CHADEMA za kugawa madini yetu Ubelgiji ili wapate hela ya kutengeneza huduma za jamii na miundo mbinu ni sawa?

CHADEMA kwa kujua au kwa kutojua wakifanya kama alivyofanya Chifu Mangungo wa Msovero kuuza ardhi ya Pwani na Morogoro kwa Karl Peter's Mkono wa damu, Karl Peter's akimtumia Dalali maarufu Ramazani. Sasa Wazungu wakimtumia Tundu Lissu alitamka hadharani kuwa Watanzania hawawezi kujiendeleza bila msaada wa mkoloni mzungu, kwa kutaka wawekezaji wachukue madini kisha waboreshe huduma za jamii, CHADEMA walitoa picha kuwa sisi watanzania hizi huduma zimetushinda kuzitoa, hivyo bora wampe Mzungu dhahabu na almasi halafu atujengee barabara na kutumunulia ndege, hili ni tusi kubwa sana CHADEMA kuwatukana Watanzania. CHADEMA wakiongozwa na Tundu Lissu wamefanya usaliti mkubwa sana kwa uhuru wetu sisi Watanzania, Shukrani zangu za dhati ziende kwa Watanzania kwa kuwakataa makanjanja awa,

- Madini ya Congo yanavyotawaliwa na Makampuni ya Kibelgiji.

Migodi mingi ya madini huko mashariki ya Congo inadhibitiwa na vikundi vya waasi na kuendeleza unyonyaji wa hali ya juu kwa wananchi wa kawaida, Vikundi hivyo vinavyodhaminiwa na makampuni ya nchi za Magharibi, vina mtiririko mbaya wa upataji madini ambao unaleta athari kwa umma. Mara kadhaa Umoja wa Mataifa umetakiwa kuweka vikwazo kwa makampuni hayo ili kuweza kukomesha vitendo viovu vinavyofanywa kwa Wananchi wa Congo. Makubaliano ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakieleza kuwa yeyote anaetoa silaha kwa vikundi vya waasi kwa ajili ya kujinufaisha kwa rasilimali za Madini ya Dhahabu katika nchi ya DRC atawekewa vikwazo, vikiwemo vya kuzuiwa kusafiri na kuzuiliwa mali zake. Makampuni hayo ya Kibelgiji yamekuwa yakijinufaisha sana na madini ya Dhahabu ya nchi ya Kongo.

Sasa katika muktadha huu Tundu Lissu na ilani ya CHADEMA kutaka kugawa dhahabu na almasi zetu kwa Wabelgiji ili wahudumie huduma za jamii kwa kuwapa madini ni usaliti. Ni usaliti kwa sababu hizo huduma za jamii hazitushindi kuzigharamia wenyewe, hata sasa Rais John Pombe Magufuli anajenga hospitali za Wilaya nchini kote, matibabu ya kibingwa kama upasuaji wa kichwa, upandikizaji figo na nyingine nyingi zimeanza kutolewa kwenye hospitali zetu hapa hapa Tanzania Shule ya msingi hadi sekondari wanafunzi wanasomeshwa bure (kwa gharama za Serikali), Miradi ya maji pia inaendelea, sasa kipi kimetushinda jamani hadi tuwape madini yetu Wabelgiji!?

- Kwa nini Tundu Lissu alikimbilia Ubelgiji.

Kwenye kampeni CHADEMA walitaka kumdhuru wapate kiki, Serikali ikamlinda mwanzo hadi mwisho kwa gharama za Serikali, baada ya Uchaguzi Serikali ikawithdraw ulinzi kwa kuwa sasa Lissu ni mwananchi ataishi kama Wananchi wengine, Lissu kuona hivyo akakimbilia Ubalozi wa Ujerumani, mbinu za CHADEMA ziligonga mwamba, kiki ikagonga mwamba, mtoa kiki Lissu nae akagonga mwamba, karudi Ubelgiji.

Nimalizie kwa lugha ya beberu ili Tundu Lissu na mababeru waliomtuma waweze kunielewa, maana Tundu Lissu kila akifanya Jambo amekuwa akiripoti kwa Wazungu waliomtuma. If I may advise you Tundu Lissu perhaps you Zitto Kabwe too. We need to have a strong opponent to face the ruling party. That opponent must be deliberately built, for the sake of national interest, not for your sake and your children or rather the whitemen who have sent you. We should not allow the opportunists into getting to form the parties that are opposing, as in other parts of Africa,

We have seen Congo, Libya the results have been a disaster, whenever you see people decided it is time to make changes and that time was 2015, the two Men Edward Lowassa and John Magufuli were the Men to make that changes, and We have seen changes from John Pombe Magufuli. We dont know what the future holds,the generations to come may decide to make Tanzania Greatest of All by changing the status quo, legally. It would be a mistake if their decision is not supported by the proper, reliable party of their choice like the one you have that supported by Western Countries,I hope you have understood and put that into your heads.

Nikiishia hapa,Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854

-Bachelor of Business Administration in International Business.
-Master of Leadership and Management.

Recent Publication;
-Assessment on the Effects of Micro-Financing on Poverty Reduction.
 

Rutorial k

JF-Expert Member
Jun 8, 2014
934
1,000
Uchaguzi umekwisha!
Uchaguzi umekwishaaaa!
Nasema, uchaguzi umekwishaaaa!
Nadhani mmenielewa!
 

Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
10,036
2,000
Lissu kila akihutubia kuharibu amani alikua anatumia msemo fulani hivi, mwanzoni sikua namuelewa ila leo mleta mada hii umenifanya nielewe. Alipenda kusema tutafanya hili na lile mpaka "Dunia ituelewe" kumbe dunia yake ni Ubelgiji na Marekani!! Loh!! huyu baba ana roho mbaya sana, hafai hata kua mtendaji wa kijiji.
 

Gatekalii

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
286
500
Lissu kila akihutubia kuharibu amani alikua anatumia msemo fulani hivi, mwanzoni sikua namuelewa ila leo mleta mada hii umenifanya nielewe. Alipenda kusema tutafanya hili na lile mpaka "Dunia ituelewe" kumbe dunia yake ni ubelgiji na marekani! Loh!! huyu baba ana roho mbaya sana, hafai hata kua mtendaji wa kijiji.
Kama kuna watu wa hovyo wamewahi tokea Tanzania Basi Lissu namba Moja.
 

Thomas10

JF-Expert Member
Mar 9, 2017
600
1,000
Siku CHADEMA wakiamua kuwapeleka Mahakamani mkathibitishe tuhuma zenu dhidi yao, mtamaliza airtime kuwapigia kuwaomba msamaha, na mtamaliza soli za viatu kuwafuata muwaombe msamaha.
 

Eng. Zezudu

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
4,627
2,000
Dogo bado unaota uteuzi unaweka hadi namba ya simu.
Madc wametosha hateui tena.
Ukweli utamuweka huru sio maneno mengi ambayo hayana Mana , omba kazi direct like this,
 

Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
2,549
2,000
Bweka mbwa bweka, watakusikia tu. Ila sitarajii kwa hii reasoning, ukapewa nafasi yoyote. Labda atakayekupa hiyo nafasi labda awe mjinga kuliko wewe. Paragraph tu ya kwanza imekuanika, haijabakiza kitu kuhusu IQ yako.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 

Econometrician

JF-Expert Member
Oct 25, 2013
11,809
2,000
Kwamba Rais akiwa Magufuli atawafanya hao unaowaita mabeberu kutoweza kuchuma hizo Rasilimali zako?

Kwa taarifa yako there's nothing to take in Tanzania, kama kipo wakiamua hata angekuwepo Nyerere sasa hivi wangechukua na hamna cha kufanya.
 

Getang'wan

JF-Expert Member
Apr 9, 2015
2,549
2,000
Kwamba rais akiwa magufuli atawafanya hao unaowaita mabeberu kutoweza kuchuma hizo rasilimali zako??.

Kwa taarifa yako there's nothing to take in Tanzania,kama kipo wakiamua hata angekuwepo nyerere sasa hv wangechukua na hamna cha kufanya.
Huyu jamaa ni kujipendekeza tu mwanzo mwisho. Hana weledi wala uelewa wowote juu hicho anachokihorojoa hapo. Hawezi kujenga hoja kwasababu hana anachokijua kuhusu mifumo ya utawala wala uchumi wa nchi.

Hajui hata punctuation, angalia alama za kiuandishi anazotumia mwanzo mwisho. Anadhani kwa utopolo huu anaoandika na kuweka na namba ya simu, naye watamkumbuka.

Sent from my SM-A505F using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom