Uhusiano wa CCM na kaptula la Marx

swagazetu

JF-Expert Member
Nov 28, 2013
4,251
1,467
marx ni mwanazuoni maarufu anayesifika sana kwa kutete mfumo wa ujamaa kote ulimwenguni.
katika miaka ya nyuma kidogo nyerere akawa mpaka anakufa alikuwa muumini mzuri wa ujamaa hata kama hakiweza kufaulu kwa kiwango alichotarajia hasa baada ya misingi ya kijamaa kuijengea kwenye Azimio la arusha kabla halijatunguliwa huko Zanzibar sehemu ya zanzania.
Nyerere na wapigania uhuru jama Sokonne walipigana ndani na nje kupigania ujamaa lakini je walifaniliwa kujenga misingi ya ujamaa imara kwa mjibu wa marxism?
katika kujiuliza swali kwamba je walifaulu au la akatokea mwandishi mmoja aliyeandika kitabu na kukiita KAPTULA LA MARX.
Nini lengo la kukipa jina hil?swali hilo ndio msingi wa mada yangu.
kwanza alimaanisha kuwa kaptula la marx liliwakilisha imani ya marx ya ujamaa yaani marxism.anaonesha na kujadilo jinsi ccm ilivyojaribu kuvaa kaptula la marx yaani kubeba imani na sera ya ujamaa jakini wakajikuta wamevaa KAPTULA lisilowaenea kwa maana kwamba ccm na serikali yake umarx unawpwaya hawauwezi kwa lugha ya mtaani kaptula lilikuwa linatela.
Hii ilionesha kuwa ccm saizi yake siyo ujamaa kwani walishindwa kabisa.
sasa kwa leo ccm haioni kama bado imevaa kaptula la marx?lipi?
ccm sera nyingi zinaanzishwa lakini inakuja kudhihirika kwamba haiwezi kuzitekeleza yaani zinapwaya,kila wakijaribu kuvaa sera inapwaya inaishia kushuka haishiki kiuno sawa sawa.baadhi ya sera zilizoishia njiani na kudhihirisha kuvaa saizi kubwa inaweza kuwa baadhi ni:
-maisha bora kwa kila mtanzania
-vua gamba
-kilimo kwanza
-mashamba ya ujamaa
-tokomeza ujangili
-kasi mpya nguvu mpya
-maisha bora kwa kila mtanzania
ni baadhi unaweza kuongezea.je.zimefanikiwa? au CCM wamevaa kaptula la MARX?
je nini mwisho wa kuvaa kaptula la marx yaani kuunda sera na kuzitekeleza?tunaenda wp?
 
2010129000154.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom