Uhusiano uliopo kati ya wasukuma na wanyamwezi

medicine

JF-Expert Member
Feb 28, 2015
216
137
Habari zenu wanajukwaa ninaomba kufahamishwa vizuri juu ya haya makabila makubwa mawili ya Tanzania wasukuma na wanyamwezi yanauhusiano gani kihistoria , nawasilisha .
 
Wote ni wamoja sema kuwa scattered ndo yakazuka haya matabaka!
Atakachoongea mnyamwezi na msukumu ni 99.99 equal. Tamaduni na mila ni zilezile...
Au kwa maana nyingine hakuna kabila la wasukuma bali wote ni wanyamwezi isipokuwa wao hujibagua wa dakama(tabora-nyamwezi), wa sukuma, wa ng'hweli, wa kiya etc etc
Watakuja wengine kukuelewesha hapa..
 
Origin yao ni moja toka huko west Africa, walipofika pwani ya Afrika Mashariki walitapakaa maeneo ya kaskazini magharibi mwa Tanganyika(Kwasasa Mwanza,Shinyanga,Simiyu,Geita na Tabora). Jamii hii ilikuwa ni ya wafugaji kama shughuli kubwa ya uchumi lakini pia miongoni mwao walikuwepo wakulima. Nyamwezi empire chini ya mtemi Milambo na wenzake waliomtangulia ndiyo iliyokuja kutenganisha wasukuma na wanyamwezi kwa maana ya waliokuwa chini ya himaya ya Milambo walikuwa wanyamwezi.

Hivyo ndiyo nilivyosimuliwa na marehemu babu yangu.

Mwisho na declare interest kuwa mimi ni Mnyamwezi.
 
Kwanza kabisa lazima kujua maana ya maneno haya yaani Sukuma na Nyamwezi.
Mpaka leo ukienda kwenye jamii hizo wao wanaitana kama Nsukuma na Ndakama, maana ya SUKUMA ni upande wa Kasikazini yaani wale walio upande wa kasikazini kuanzia Shinyanga hadi Mwanza. DAKAMA maana yake ni KUSINI yaani walioupande wa kusini kuanzia wilaya za Nzega, Kahama mpaka mwisho wa mkoa wote wa Tabora. Haya ndio majina yaliyotumiwa kuitana wao jamii hizo, wale wa Mashariki na Magharibi nao waliitwa majina yao mfano WASHASHI wakimaanisha makabila ya mkoa wa Mara n.k.
Neno nyamwezi lilikuja kutokea baada ya wale WADAKAMA-Wa kusini kutawaliwa na utemi wa UNYANYEMBE, ndio hapo yalionekana kama makabila mawili!
 
Brief and clear, safi sana mtegamasikio. Me pia mnyamwezi mwenzio.
 
Origin yao ni moja toka huko west Africa, walipofika pwani ya Afrika Mashariki walitapakaa maeneo ya kaskazini magharibi mwa Tanganyika(Kwasasa Mwanza,Shinyanga,Simiyu,Geita na Tabora). Jamii hii ilikuwa ni ya wafugaji kama shughuli kubwa ya uchumi lakini pia miongoni mwao walikuwepo wakulima. Nyamwezi empire chini ya mtemi Milambo na wenzake waliomtangulia ndiyo iliyokuja kutenganisha wasukuma na wanyamwezi kwa maana ya waliokuwa chini ya himaya ya Milambo walikuwa wanyamwezi.

Hivyo ndiyo nilivyosimuliwa na marehemu babu yangu.

Mwisho na declare interest kuwa mimi ni Mnyamwezi.
nikusahihishe kidogo...Mirambo hakuwa na Empire kama inavyoeleweka..
Isipokua alikua Mtemi kwa maana ya Ubabe tu...
 
Kwanza kabisa lazima kujua maana ya maneno haya yaani Sukuma na Nyamwezi.
Mpaka leo ukienda kwenye jamii hizo wao wanaitana kama Nsukuma na Ndakama, maana ya SUKUMA ni upande wa Kasikazini yaani wale walio upande wa kasikazini kuanzia Shinyanga hadi Mwanza. DAKAMA maana yake ni KUSINI yaani walioupande wa kusini kuanzia wilaya za Nzega, Kahama mpaka mwisho wa mkoa wote wa Tabora. Haya ndio majina yaliyotumiwa kuitana wao jamii hizo, wale wa Mashariki na Magharibi nao waliitwa majina yao mfano WASHASHI wakimaanisha makabila ya mkoa wa Mara n.k.
Neno nyamwezi lilikuja kutokea baada ya wale WADAKAMA-Wa kusini kutawaliwa na utemi wa UNYANYEMBE, ndio hapo yalionekana kama makabila mawili!
Unyamwezini wangesema "You nail it"

Ahahaaaaa...

Umejazia Nyama vizuri kwenye hoja
 
Kwanza kabisa lazima kujua maana ya maneno haya yaani Sukuma na Nyamwezi.
Mpaka leo ukienda kwenye jamii hizo wao wanaitana kama Nsukuma na Ndakama, maana ya SUKUMA ni upande wa Kasikazini yaani wale walio upande wa kasikazini kuanzia Shinyanga hadi Mwanza. DAKAMA maana yake ni KUSINI yaani walioupande wa kusini kuanzia wilaya za Nzega, Kahama mpaka mwisho wa mkoa wote wa Tabora. Haya ndio majina yaliyotumiwa kuitana wao jamii hizo, wale wa Mashariki na Magharibi nao waliitwa majina yao mfano WASHASHI wakimaanisha makabila ya mkoa wa Mara n.k.
Neno nyamwezi lilikuja kutokea baada ya wale WADAKAMA-Wa kusini kutawaliwa na utemi wa UNYANYEMBE, ndio hapo yalionekana kama makabila mawili!
Yawezekana jina Wanyamwezi lilitoka kwa Wagogo, yaani "wa Magharibi".
 
nikusahihishe kidogo...Mirambo hakuwa na Empire kama inavyoeleweka..
Isipokua alikua Mtemi kwa maana ya Ubabe tu...
hahahahaaa mkuu umenichekesha sana.... mtemi kwa kisukuma anaitwa Ntemi yaani mtawala wa eneo husika. so milambo na Isike walikuwa na empire zao... na sio ubabe kama ulivotafsiri
 
labda hujanielewa sawasawa..
Isike alikua Mtemi sawa..haina shida..
Lakini Mirambo hakua Mtemi, Kwa maana ya Utemi wenye kuongoza nchi (kipindi hicho hizo tawala zikiitwa nchi)...
Isipokua alikua mbabe mwenye kikundi cha wafuasi watiifu kwake..
 
Habari zenu wanajukwaa ninaomba kufahamishwa vizuri juu ya haya makabila makubwa mawili ya Tanzania wasukuma na wanyamwezi yanauhusiano gani kihistoria , nawasilisha .
Mkuu kifupi kabila la wanyamwezi ni watu waliotoka magharibi mwa afrika,Niger-Congo,kabila mama ni Wanyamwezi,wasukuma ni tabaka lilikotoka kwenye kabila kubwa la wanyamwezi.Katika kabila kubwa la wanyamwezi kuna mashina(makabila matano) yametoka humo,na yanafanana kitabia,asili,lugha,desturi nk.Mashina hayo ni kabila la Wanyamwezi,wakonongo,wakimbu,wasumbwa na wasukuma.Wanyamwezi walipotoka magharibi mwa afrika waliweka makazi Tabora kabla ya kuanza kusambaa kuelekea kaskazini magharibi(ukanda wa ziwa).Hivyo mpaka sasa Tanzania kabila linaloongoza kuwa na watu wengi ni Wasukuma,wakifuatiwa na kabila la pili kwa ukubwa ni wanyamwezi.Makabila haya kwa kifupi yanaongoza kwa kuchapa kazi na ukarimu..ndio maana toka Enzi wanasema 'mzigo mzito mpe mnyamwezi',na hata marekani(ambayo inasifika kwa watu wake ukarimu wa kusaidia watu wengine inaitwa 'unyamwezini',hela yao ya dola inaitwa 'mnyamwezi', au mtu akiwa anamzungumzia rafiki yake wa ukweli utasikia akisema 'mnyamwezi wangu'. Lakini pia ndio makabila yanaongoza kwa ushujaa na mapambano,ndio maana machifu wao ni maarufu zaidi kuliko wa makabila mengine kama chifu mirambo na jeshi lake la wavuta bangi 'maarufu kama warugaruga',chifu Isike,chifu Mihayo,chifu Fundikira nk. Makabila haya yanasifika kwa kilimo na ufugaji,pia kwa ukarimu wa hali ya juu hususani wasukuma.Hakuna kabila wakarimu kama wasukuma,labda ndio maana Mungu nae amewazidishia katika ardhi yao kuna kila aina ya neema,chakula cha kutosha,masamaki,madhahabu,mapamba,mang'ombe,maasali,mahela... nk. Ila pia hawako nyuma kwenye uchawi na mizimu hasa kama umewaonea au umewaibia.Inawezekana ni mauchawi waliyotoka nayo huko afrika magharibi na njiani walipopitia congo kuingia Tanzania.So take care
 
Mkuu kifupi kabila la wanyamwezi ni watu waliotoka magharibi mwa afrika,Niger-Congo,kabila mama ni Wanyamwezi,wasukuma ni tabaka lilikotoka kwenye kabila kubwa la wanyamwezi.Katika kabila kubwa la wanyamwezi kuna mashina(makabila matano) yametoka humo,na yanafanana kitabia,asili,lugha,desturi nk.Mashina hayo ni kabila la Wanyamwezi,wakonongo,wakimbu,wasumbwa na wasukuma.Wanyamwezi walipotoka magharibi mwa afrika waliweka makazi Tabora kabla ya kuanza kusambaa kuelekea kaskazini magharibi(ukanda wa ziwa).Hivyo mpaka sasa Tanzania kabila linaloongoza kuwa na watu wengi ni Wasukuma,wakifuatiwa na kabila la pili kwa ukubwa ni wanyamwezi.Makabila haya kwa kifupi yanaongoza kwa kuchapa kazi na ukarimu..ndio maana toka Enzi wanasema 'mzigo mzito mpe mnyamwezi',na hata marekani(ambayo inasifika kwa watu wake ukarimu wa kusaidia watu wengine inaitwa 'unyamwezini',hela yao ya dola inaitwa 'mnyamwezi', au mtu akiwa anamzungumzia rafiki yake wa ukweli utasikia akisema 'mnyamwezi wangu'. Lakini pia ndio makabila yanaongoza kwa ushujaa na mapambano,ndio maana machifu wao ni maarufu zaidi kuliko wa makabila mengine kama chifu mirambo na jeshi lake la wavuta bangi 'maarufu kama warugaruga',chifu Isike,chifu Mihayo,chifu Fundikira nk. Makabila haya yanasifika kwa kilimo na ufugaji,pia kwa ukarimu wa hali ya juu hususani wasukuma.Hakuna kabila wakarimu kama wasukuma,labda ndio maana Mungu nae amewazidishia katika ardhi yao kuna kila aian ya neema,chakula cha kutosha,masamaki,madhahabu,mapamba nk. Ila pia hawako nyuma kwenye uchawi na mizimu hasa kama umewaonea au umewaibia.Inawezekana ni mauchawi waliyotoka nayo huko afrika magharibi na njiani walipopitia congo kuingia Tanzania.So take care
Unataka kuniambia wanyamwezi na wasukuma sio watanzania halisi Bali wazamiaji,? Sasa kina Bashe na kina rostam Kila siku tunawasema bure kumbe hakuna mwenye nchi yake,
Nakubaliana na wewe kuwa wasukuma Ndio Kabila lenye ukarimu kuzidi makabila yote Tanzania, na wanawake wao wanaweza kushika nafasi ya Kwanza kwa nidhamu pia
 
Nafikiri watanzania wengi ni wazamiaji,tumetoka nchi mbalimbali kwa sababu mbalimbali...Mfano Waha ni waburundi,Wamanyema ni wakongo,Wahaya ni waganda,Wajaluo ni wakenya,Wachagga ni Wakikuyu wa Kenya,Wamakonde ni wamsumbiji..the list goes on and on...
 
Mkuu kifupi kabila la wanyamwezi ni watu waliotoka magharibi mwa afrika,Niger-Congo,kabila mama ni Wanyamwezi,wasukuma ni tabaka lilikotoka kwenye kabila kubwa la wanyamwezi.Katika kabila kubwa la wanyamwezi kuna mashina(makabila matano) yametoka humo,na yanafanana kitabia,asili,lugha,desturi nk.Mashina hayo ni kabila la Wanyamwezi,wakonongo,wakimbu,wasumbwa na wasukuma.Wanyamwezi walipotoka magharibi mwa afrika waliweka makazi Tabora kabla ya kuanza kusambaa kuelekea kaskazini magharibi(ukanda wa ziwa).Hivyo mpaka sasa Tanzania kabila linaloongoza kuwa na watu wengi ni Wasukuma,wakifuatiwa na kabila la pili kwa ukubwa ni wanyamwezi.Makabila haya kwa kifupi yanaongoza kwa kuchapa kazi na ukarimu..ndio maana toka Enzi wanasema 'mzigo mzito mpe mnyamwezi',na hata marekani(ambayo inasifika kwa watu wake ukarimu wa kusaidia watu wengine inaitwa 'unyamwezini',hela yao ya dola inaitwa 'mnyamwezi', au mtu akiwa anamzungumzia rafiki yake wa ukweli utasikia akisema 'mnyamwezi wangu'. Lakini pia ndio makabila yanaongoza kwa ushujaa na mapambano,ndio maana machifu wao ni maarufu zaidi kuliko wa makabila mengine kama chifu mirambo na jeshi lake la wavuta bangi 'maarufu kama warugaruga',chifu Isike,chifu Mihayo,chifu Fundikira nk. Makabila haya yanasifika kwa kilimo na ufugaji,pia kwa ukarimu wa hali ya juu hususani wasukuma.Hakuna kabila wakarimu kama wasukuma,labda ndio maana Mungu nae amewazidishia katika ardhi yao kuna kila aian ya neema,chakula cha kutosha,masamaki,madhahabu,mapamba nk. Ila pia hawako nyuma kwenye uchawi na mizimu hasa kama umewaonea au umewaibia.Inawezekana ni mauchawi waliyotoka nayo huko afrika magharibi na njiani walipopitia congo kuingia Tanzania.So take care
umesahau mang'ombe, maasali na matobolwa.
 
Unataka kuniambia wanyamwezi na wasukuma sio watanzania halisi Bali wazamiaji,? Sasa kina Bashe na kina rostam Kila siku tunawasema bure kumbe hakuna mwenye nchi yake,
Nakubaliana na wewe kuwa wasukuma Ndio Kabila lenye ukarimu kuzidi makabila yote Tanzania, na wanawake wao wanaweza kushika nafasi ya Kwanza kwa nidhamu pia
Ukiuchukulia huu mfano wa Wasukuma na Wanyamwezi ni kama USA wakazi wake wa kwanza ni red Indians, wazungu wote wamehamia tu. Huwezi kulinganisha hayo na Bashe na Rostam.
 
Waliitwa wanyamwezi Na jirani zao wagogo,walimaanisha watu wanaotoka upande wa mwezi
 
Back
Top Bottom