Uhusiano uliopo kati ya manabii (viongozi wa dini) waongo na viongozi waovu

bigmukolo

JF-Expert Member
Mar 6, 2012
519
1,000
Manabii wa uongo au viongozi wa dini wanaotumikia maslahi binafsi na watawala waovu ni mihimili ya uovu isiyoweza kutengana. Manabii wa uongo huwatumia watawala waovu ili kupata ulinzi na uhalali wa uovu wao. Ukaribu wao na watu wenye nguvu ya kimamlaka katika jamii huwasaidia katika mikakati yao katika kuupumbaza umma uliopofushwa macho ambao huangalia uhalali wa mambo kwa kuona ushiriki na ukaribu wa wenye nguvu katika taasisi au dini husika.

Watawala waovu hunufaika na uwepo wa manabii wa uongo ambao hufanya kazi ya kuwapofusha macho watu wasiweze kuhoji wala kujitambua. Jamii isiyohoji wala kujitambua ni mtaji mkubwa kwa watawala waovu.

Unaweza kusoma tena kwa umakini kuhusu uhusiano uliokuwepo kati ya Mfalme Ahabu na viongozi wa dini 400 katika Biblia Takatifu katika kitabu cha 1Wafalme 22:1-40. Utaona jinsi makundi haya mawili yalivyokuwa yakifaidiana. Ye yote aliyejitokeza kuwakemea na kuwakosoa waliungana pamoja kumshughulikia.

Makundi haya yako tayari kushirikiana hata kwa lengo la kutoa uhai wa mtu ye yote anayekwenda kinyume na mitazamo yao, muono wao, mipango yao, na matarajio yao! Silaha za makundi haya mawili ambazo ni miujiza ya uongo (inayofanywa au kutangazwa na manabii wa uongo) na propaganda chafu (zinazoendeshwa na watawala waovu) zote zinalengo moja nalo ni kuwapofusha macho watu ili waendelee kuwanyonya, kuwakandamiza na kuwatala. Ikumbukwe kuwa sio kila nabii wa uongo huhusika na miujiza, la hasha! Wapo pia viongozi wa dini ambao ni manabii wa uongo ambao hawafanyi miujiza lakini wana mambo mengine ikiwemo ushirikina, ukandamizaji, nk.

Katika mazingira kama haya ukweli unageuka kuwa bidhaa adimu na ghali sana kwa sababu watu wachache wanaojitokeza kuusema ukweli hujikuta wakiandamwa, wakichafuliwa, na hata kuuawa. Hayo yanapotukia wengi hurudi nyuma na kukaa kimya. Lakini kama kweli tumeitwa kwa ajili ya kushuhudia kweli kwa nini tuogope matusi, kuchafuliwa, kufilisiwa, na hata kifo? Kamwe hatuwezi kuogopa na tunatiwa moyo zaidi na Neno la Mungu kutoka Biblia Takatifu kitabu cha Warumi 8:28:39
 
battawi

JF-Expert Member
Mar 29, 2014
2,112
2,000

Ni Mungu pekee anayetuma manabii na Mitume,
Wafusi wa mitume waliokutana na mtume pia huweza kuwa na sifa za Utume ,lakini sio hawa wa leo.
Suala la Unabii au utume halipo tena duniani ,wanaojitokeza wote ni Wongo.
Kwa dini zote za Vitabu. Qur an, Injilii,Taurati na Zburi.
 
client3

JF-Expert Member
Aug 6, 2007
2,261
2,000
Sijasoma yote ila ni kweli, na hakuna anayeweza kumkemea mwenzie sababu wote wamesimama kwenye misingi miovu na batili.Ujasiri huo haupo kabisa.
 
mwanadome

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,720
2,000
Naishi kawe karibu na anaye jiita mtume mwamposaa, yanayoendelea hapa ni anguko kwa jamii yetu.

Yes, hawa manabii na mtume wa uongo njia pekeee inayowapa nguvu kuendeleza girba zao ni kufunga mana kwao na dola.

Gwajima alijaribu kujitenga na dola, misukosuko aliyokua akiipata ilitishia uwepo wake. Sasa kawapigia magoti ana uhakika wa kuendeleza harakati zake.

Najaribu kuwaza vifo vilivyotokea kwa mwamposaa vingetokea kwa "nabii /mtume"asie upande wa serikali sijui kama angekua huru muda huu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom