Uhusiano mbaya kati ya bosi na mtumishi wake

Equation x

JF-Expert Member
Sep 3, 2017
29,323
40,174
Nilitembelea mgahawa x kupata chakula ili nisijekufa kwa njaa, akatokea jamaa mmoja mtu wa miraba minne naye akawa amekuja kupata huduma ya chakula...kama mnavyojua tena, kula ni muhimu ili kuupa mwili afya na nguvu; akaagiza mahitaji yake naye akahudumiwa.

Mbaya zaidi alikuja na dereva wake, lakini dereva hakuhudumiwa bali yeye alibaki kwenye gari huku akipiga mihayo ya uchovu na njaa. Kilichotusikitisha wengi, ni kwa nini bosi anajihudumia yeye mwenyewe bila kumjali mfanyakazi wake? Huo sio uhusiano mzuri.
 
Ungemuuliza huyo Boss ungetusaidia na sisi kuifahamu sababu.. Sasa tutabakia tunabashiri tu,

Huenda Dereva alikuwa kwenye mfungo..
Mfungo huwa ni kisingizio mkuu,jaribu kuwatizama wanaokuzunguka unaweza kugundua hii hali
 
Ungemuuliza huyo Boss ungetusaidia na sisi kuifahamu sababu.. Sasa tutabakia tunabashiri tu,

Huenda Dereva alikuwa kwenye mfungo..
Kabisa angemuuliza Boss kwann anafanya mambo ya ajabu kama haya kwa dereva wake.
 
Kama mgahawa vyakula ni bei utamlazimisha dereva ale hapo wakati hana uwezo? Au unataka boss amlipie?
Anatakiwa amlipie hata chakula standard ya kawaida,huo ndio utu na uhusiano mzuri
 
Hivi inawezekana kola bosi atakapoenda kula amnunulie na dereva wake kweli? Sijui unafanya kazi sehem gan lakini bosi anamshahara wake na posho zake na dereva ana msahara wake na posho zake sio rahisi bosi kutoa Huduma ya chakula kwa dereva wake kila wanapotoka huyo anaweza kufanya siku moja moja kwa kujisikia tu!
 
Kwani ni lazima kwa Boss kununulia chakula dereva?? Wewe kama ni dereva na unalipwa vizuri sio lazima udekezwe na kununuliwa chakula na boss. Vile vile kuna nidhamu za kazi, sio lazima ukale hoteli moja na boss wako au kukaa nae kwenye migahawa/bar bila sababu maalumu za kikazi. Kizazi cha dot com hamtaelewa ninaloongea hapa, kila kazi ina maadili yake!
 
Maadili yapo; ila uhusiano mzuri pia ni muhimu. Ndio maana kuna baadhi ya sehemu...kuna wengine wanapenda kufanya kazi na mtu fulani kutokana aina ya uongozi anaoutumia.
 
Nakuunga mkono 100% na huwa ipo hivyo kwa madereva wengi na huwa hawalipi cash mda huo huo(wanakula kwa order wanalipa kwa wiki au mwezi).
Boss anao uhuru wa kula popote anapotaka
Ile hali ya bosi anakula,huku dereva akimsubiri kwenye gari...imekaaje hii?
 
Poem: BUILDING THE NATION
Poet: Henry Barlow

Today I did my share in building the nation.
I drove a Permanent Secretary to an
important, urgent function
In fact, to a luncheon at the Vic.

The menu reflected its importance
Cold bell beer with small talk,
Then fried chicken with niceties
Wine to fill the hollowness of the laughs
Ice-cream to cover the stereotype jokes
Coffee to keep the PS awake on the return journey

I drove the Permanent Secretary back.
He yawned many times in the back of the car
Then to keep awake, he suddenly asked,
Did you have any lunch friend?
I replied looking straight ahead
And secretly smiling at his belated concern
That I had not, but was slimming!
Upon which he said with a seriousness
Which amused more than annoyed me,
Mwanachi, I too had none!
I attended to matters of state.

Highly delicate diplomatic duties you know,
And friend, it goes against my grain,
Causes me stomach ulcers and wind,
Ah, he continued, yawning again,
The pains we suffer in building the nation!

So the PS had ulcers too!
My ulcers I think are equally painful
Only they are caused by hunger
Not sumptuous lunches!
So two nation builders
Arrived home this evening
With terrible stomach pains
The result of building the nation – in different ways”
 
Maadili yapo; ila uhusiano mzuri pia ni muhimu. Ndio maana kuna baadhi ya sehemu...kuna wengine wanapenda kufanya kazi na mtu fulani kutokana aina ya uongozi anaoutumia.

Kwenda kula chakula na boss ndio uhusiano mzuri?? Ukitaka kuwa na mahusiano mazuri na waliochini yako kuna baadhi ya vitu jiepushe navyo ikiwa ni pamoja na kula/kunywa nao. Kwa mfano mimi ni boss wako nahakikisha unapata mshahara mzuri, huduma zote unazostahili unapata, unapokuwa na shida mahitaji nahakikisha unapata ila sikai na wewe tukala wote hotelini utajiona sina uhusiano mzuri na wewe dereva wangu?
 
Nakuunga mkono 100% na huwa ipo hivyo kwa madereva wengi na huwa hawalipi cash mda huo huo(wanakula kwa order wanalipa kwa wiki au mwezi).
Boss anao uhuru wa kula popote anapotaka
Yaap na ndio maana ikitokea bosi amesafiri hata kulala hulala mahari tofauti, sasa kwa asiyeelewa anaweza kuona kama bosi hamtendei haki dereva bila kujua wote wanalipwa per diem lakini viwango tofauti so bosi hawezi kulipwa 120,000/100,000 per diem na dereva alipwe 80,000 utegemee watakula au kulala sehemu sawa ingawa mala chache bosi mstaarabu anaweza kumpa offer dereva wake
 
Maadili yapo; ila uhusiano mzuri pia ni muhimu. Ndio maana kuna baadhi ya sehemu...kuna wengine wanapenda kufanya kazi na mtu fulani kutokana aina ya uongozi anaoutumia.
Pamoja na hiyo bado sio rahisi bosi na dereva kula pamoja, chukulia wamesafiri wiki tatu je bosi atamnunulie chakula dereva wiki zote tatu
 
Back
Top Bottom