Uhusiano kati ya kuibiwa vioo vya gari na eneo la gerezani Kariakoo

Carina

Senior Member
Jan 4, 2011
190
65
Wana JF,
Kuna issue moja hapa huwa siielewi elewi hivi .... ni pale mtu anapoibiwa vioo vya gari kama labda site mirros na ambapo ukienda eneo la Gerezani (huwa wanaita mnadani) unavikuta vioo vyako safi kabisa ila ukionekana mtata mtata wanavivunja mbele yako, otherwise ukionekana mwema, basi itabidi uvinunue tu kwa gharama.

Cha kushangaza ni kwanini polisi wanashindwa kufuatilia na kujua mzizi uko wapi? kwani inavyoonekana polisi wanajua issue nzima kama si wanashirikiana nao.

Nakumbuka niliwahi kuibiwa site mirrors wakati naenda kutafuta Kariakoo, polisi wakanikamata kwamba naendesha gari bila site mirros, nikawaambia ndio kwanza natafuta nyingine kwani niliibiwa jana usiku, cha kushangaza polisi hao hao wakanishauri niende Gerezani kwani vipo vingi.

Sasa sijui inakuwaje hapo wajameni ...
 
Pale panajulikana sana, hata mkulu wa nchi gari yake enzi akiwa mambo ya nje gari yake iliibwa site mirrors...kwa sababu ni mtoto wa mjini na enzi zile hayati Ditopile alikuwa hai...mara moja vilipatikana.
Taarifa zilimfikia Mahita ambapo IGP huyo alitoa nusu saa tu na vikapelekwa kituo kidogo cha polisi pale msimbazi vikiwa ni salama salmini.
Ni kweli...ukiwa mtata wanavivunja tena mbele yako,
 
Mkuu unanitonesha moyoni,umenikumbusha mwaka jana walipopora power window za gari yangu,nlishauriwa kwenda pale,jaman nkakutana nazo. Zilinishinda bei yan power window za mbele mbili sh.lak4. Nlilazimika kutumia kiyoyozi mpaka nkaagiza zingne. Jaman bongo noma!
 
nisahihishe. Siyo 'site mirrors' ni side mirrors.
Hata mie niliwahi kuibiwa kkoo. Na siku hizi wanaiba hata side mirrors zenye maandishi ya namba za gari. So sad. Wanaiba hata kwenye foleni kama pale ubungo n.k.
Lini tz tutapata kiongozi atakayepunguza uhalifu wa kipuuzi kama huu?!
 
nisahihishe. Siyo 'site mirrors' ni side mirrors. Hata mie niliwahi kuibiwa kkoo. Na siku hizi wanaiba hata side mirrors zenye maandishi ya namba za gari. So sad. Wanaiba hata kwenye foleni kama pale ubungo n.k. Lini tz tutapata kiongozi atakayepunguza uhalifu wa kipuuzi kama huu?!
Kwani tatizo lilianza lini
 
Mimi waliniibia mara mbili hadi nilipoamua kuwapa shekeli in advance na kuwaomba wasiniibie tena.
 
Yaap bro yale mataa kama unatoka mitaa ya Cort yard hotel tena mida ya saa tisa jioni sina hamu napo


M-R,
Jitahidi weka ki-tented maana hao jamaa huwasumbua sana wadada na hasa wakikuona upo peke yako ndani ya gari, wadada huibiwa sana.
 
nisahihishe. Siyo 'site mirrors' ni side mirrors.
Hata mie niliwahi kuibiwa kkoo. Na siku hizi wanaiba hata side mirrors zenye maandishi ya namba za gari. So sad. Wanaiba hata kwenye foleni kama pale ubungo n.k.
Lini tz tutapata kiongozi atakayepunguza uhalifu wa kipuuzi kama huu?!

AGUSTINE L. MREMA (mb) NDIYE JIBU PEKEE MPAKA SASA AKITAFUTIWA NA WATU MAKINI WA KUTENDA NAO KAZI ....ISIJALISHE HATA KAMA WAMESTAAFU
 
Mimi nimewahi kuibiwa mara 2 na mara zote nikaenda PALE gerezani nikapata ila mimi sikununua nilienda na mdogo wangu ni mjeshi akabaki kwenye gari yenye tinted sasa walipovileta tu wakaweka akashuka wacha tulianzishe wale waswahili ni waoga sana tuliwapa mfueni wa nguvu na kuondoka saafi, tangu siku hiyo sijaibiwa tena
 
Nani kakwambia nji hii ina polisi. Serikali imewatelekeza wamebaki kujitafutia wenyewe kama kuku wa kienyeji. Wanakula na waharifu. Kazi kupiga watu mabomu hata wale wanaowatetea wapate maslahi mazuri. Nji hii sasa imeharibika kwa kukosa polisi, watu wanajifanyia wanavyotaka tu! si tunaona jamani. Polisi wasindikiza misafara ya wakubwa tu.Wamekata tamaa wanashindwa tu kujiuzulu.
 
Kimsingi wale jamaa hawawezekani wakati fulani niliibiwa kioo cha mbele cha gari yangu maeneo ya temeke, nilisikitika sana maana siku hiyo nilikuwa na safari muhimu hivyo tukio hilo likawa limeathiri mpango mzima wa safari, nilichukuwa uamuzi wa kwenda gerezani ambapo nilipofika nilitakiwa nieleze eneo kioo kilipoibiwa baada ya kutoa maelezo yangu kwa hao wahusika niliambiwa nirudi baadae maana ilikuwa bado hakijapelekwa, baada ya masaa matatu nilirudi nakuelezwa kuwa tayari mzigo upo. niliambiwa nikodi taxi hadi keko ambapo nilipofika maeneo hayo mtu niliyekuwa naye ambaye ni fundi wangu wa gari aliamriwa ashuke ili tuendelee na safari mimi na hao wenye mzigo, alishuka baada ya kuingia mitaa kadhaa ndani kabisa eneo la Keko niliambiwa nisubiri ambapo baada ya dk kadhaa kioo changu kililetwa nami nikatoa kiasi cha pesa kilichodaiwa. Kabla sijakabidhiwa nilielezwa kabisa kuwa kama nitaleta ubishi wa aina yeyote nitakosa kioo na sitakwepa kipigo!!!!! chakusikitisha ni hata vyombo vya dola vinajua kuwa hiyo ndiyo sehemu ambayo huwezi kukosa vitu vya wizi
 
mimi jamani nimeibiwa juzi tu pale ubungo mataa na gari ipo kwenye foleni side mirrors zote mbili, nilipata na hasira sikuwa na jinsi ila waliharibu programme zangu zote siku hiyo. na vina namba kabisa nikaenda mnadani wakasema vikiwa na namba huwa haviji pale basi nikauziwa vingine kwa shs 90,000 mbwa kabisa nina hasira na wezi sasa hivi hatari nimeamua kushighulikia gun sasa hivi liwalo na liwe.tumefikia pabaya sana
 
Mimi nimewahi kuibiwa mara 2 na mara zote nikaenda PALE gerezani nikapata ila mimi sikununua nilienda na mdogo wangu ni mjeshi akabaki kwenye gari yenye tinted sasa walipovileta tu wakaweka akashuka wacha tulianzishe wale waswahili ni waoga sana tuliwapa mfueni wa nguvu na kuondoka saafi, tangu siku hiyo sijaibiwa tena
Hiyo ndiyo dawa yao, haki ya mtu haiombwi wala hainunuliwi bali huchukuliwa kwa nguvu.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom