Uhusiano kati ya CHADEMA na ACT-Wazalendo ni tete sana

Mara nyingi ACT-Wazalendo wamekuwa wakituonyesha as if wana uhusiano mzuri sana kisiasa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiasi cha kutaka kusimamisha mgombea mmoja kwenye uchaguzi ujao kwa nafasi za Uras, Ubunge, na Udiwani.

Ukweli ni kuwa vyama hivyo vimekuwa na misigano ya muda mrefu kutokana na kuwa kila chama kimekuwa kikiangalia maslahi yake binafsi badala ya umoja wao. Kila chama kina lengo la kujitangaza na hivyo kuwa chama kikuu cha upinzani, hivyo kumekuwa na marumbano ya nani hasa asimamishwe kuviwakilisha vyama hivyo hasa kwa nafasi ya Urais. Wakati ACT-Wazalendo wakimnadi Bernard Membe, CHADEMA wao wanamnadi Tundu Lissu kuwa ndiye mtu sahihi kwa nafasi hiyo ya juu kabisa.

Ikumbukwe kuwa Viongozi wa ACT-Wazalendo walisusia tukio la kupokelewa kwa Lissu katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere (JNIA) hapo tarehe 27/07/2020 akitokea nchini Ubelgiji. Aidha ACT-Wazalendo hawakushiriki uhuni uliotaka kufanywa na Chadema pale Uwanja wa Uhuru kwenye Tukio na kumuaga Rais Mstaafu Benjamin Mkapa. Wakati CDM wakishindwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali kwa lengo la kumpaisha Lissu kisiasa, ACT-Wazalendo wao waliufuata utaratibu huo na viongozi wao walikaribishwa vizuri kabisa, akiwemo Mwenyekiti wao wa Taifa Ndugu Maalim Seif.

Vyama hivyo vimekuwa vikipeana ushauri ambao kimsingi una lengo la kukiua chama kingine kisiasa. Vilikubaliana wafuasi wao wajitokeze pale JNIA kumpokea Lissu, lakini ACT-Wazalendo wao wakashindwa kufika. Pia wakaweka mipango ya namna ya kuingia Uwanja wa Uhuru ambayo itamtangaza Lissu, wao ACT-Wazalendo wakafuata utaratibu wa Serikali. Kimsingi vyama hivi havina uhusiano mzuri, vimekuwa vikihujumiana kwa kiasi kikubwa.
Misuguano ni kawaida sana kwenye siasa na ACT soon wataungana na CDM na vyama vingine kuing’oa CCM.
 
Hawa ACT sijawahi kuwaamini, hasa zito kabwe
Kama ulimuamini LOWASA ukataka kumpeleka IKULU sembuse usimuamini Zitto , hapo wafuasi wa vyama ndio huwa mnaniacha hoi, mimi binafsi kama mjenzi huru nchi hii naamini watu wawili tu kwa sasa Lisu na Zitto hawa wengine waliobaki wapo kwenye siasa kujinufaisha.
 
Mara nyingi ACT-Wazalendo wamekuwa wakituonyesha as if wana uhusiano mzuri sana kisiasa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kiasi cha kutaka kusimamisha mgombea mmoja kwenye uchaguzi ujao kwa nafasi za Uras, Ubunge, na Udiwani.

Ukweli ni kuwa vyama hivyo vimekuwa na misigano ya muda mrefu kutokana na kuwa kila chama kimekuwa kikiangalia maslahi yake binafsi badala ya umoja wao. Kila chama kina lengo la kujitangaza na hivyo kuwa chama kikuu cha upinzani, hivyo kumekuwa na marumbano ya nani hasa asimamishwe kuviwakilisha vyama hivyo hasa kwa nafasi ya Urais. Wakati ACT-Wazalendo wakimnadi Bernard Membe, CHADEMA wao wanamnadi Tundu Lissu kuwa ndiye mtu sahihi kwa nafasi hiyo ya juu kabisa.

Ikumbukwe kuwa Viongozi wa ACT-Wazalendo walisusia tukio la kupokelewa kwa Lissu katika Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere (JNIA) hapo tarehe 27/07/2020 akitokea nchini Ubelgiji. Aidha ACT-Wazalendo hawakushiriki uhuni uliotaka kufanywa na Chadema pale Uwanja wa Uhuru kwenye Tukio na kumuaga Rais Mstaafu Benjamin Mkapa. Wakati CDM wakishindwa kufuata maelekezo yaliyotolewa na Serikali kwa lengo la kumpaisha Lissu kisiasa, ACT-Wazalendo wao waliufuata utaratibu huo na viongozi wao walikaribishwa vizuri kabisa, akiwemo Mwenyekiti wao wa Taifa Ndugu Maalim Seif.

Vyama hivyo vimekuwa vikipeana ushauri ambao kimsingi una lengo la kukiua chama kingine kisiasa. Vilikubaliana wafuasi wao wajitokeze pale JNIA kumpokea Lissu, lakini ACT-Wazalendo wao wakashindwa kufika. Pia wakaweka mipango ya namna ya kuingia Uwanja wa Uhuru ambayo itamtangaza Lissu, wao ACT-Wazalendo wakafuata utaratibu wa Serikali. Kimsingi vyama hivi havina uhusiano mzuri, vimekuwa vikihujumiana kwa kiasi kikubwa.
Huwa unalipwa shilingi ngapi huko sisiemu kwa kuandika ujinga?
 
Nasema huwa mnalipwa bei gani kwa kutetea Ushetani wa kuiba rasilimali za nchi huko ccm?

Naona mizuka ndio imekuwa ikikutawala zaidi kuliko uhalisia wa Mambo. Mbona mnaowaitwa wezi wakiondoka CCM mnawaishia kuwasafisha?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom