Uhusiano gani kati ya kuota meno na kuharisha kwa mtoto mdogo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Uhusiano gani kati ya kuota meno na kuharisha kwa mtoto mdogo

Discussion in 'JF Doctor' started by Mgombezi, Aug 30, 2012.

 1. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Katika malezi yangu, kuna wakati mtoto huharisha (kinyesi kilichochanganyika na ute mzito au malenda) na nimekuwa nikiambiwa nisimpe dawa na hiyo hutokana na kuota meno; hawa waliokuwa wakitoa ushauri huu nilishindwa kuwauliza sababu, bali leo nimeamua kuleta katika jukwaa hili, kwamba kuna uhusiano gani wa kitabibu au maumbile kwa mtoto kuota meno na kuharisha.
   
 2. Nivea

  Nivea JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2012
  Joined: May 21, 2012
  Messages: 7,449
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  kwakweli hata wangu ameugua kuhara hivi karibuni then nikaona meno hayo ,nilimpeleka hsptal hakupewa dawa
   
 3. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Mkuu, turudi kwenye mila, mfunge jino la mbuzi alivae shingoni, hata uguwa wala kuharisha na meno yataota faster huwezi amini, so its up to you! YES to buy my idea or ignore!:A S 465:
   
 4. C

  CAY JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 501
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Jino la mbuzi linapatikana wapi?Kwenye nyama choma?Si watanishangaa sana wale jamaa?
   
 5. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Tuma kijan akakuombe ni bonge ya dawa unless mtoto atawasumbua sana ile ni bonge ya tiba, tuma kijana yapo mengi tu mtaani siyo issue kivile hakuna atakaeshanga bhana!
   
 6. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Du wewe ni wa pande za kule kwetu nini, hahaha umenikumbusha mbali sana
   
 7. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  wakukaya ha ha ha ha ha ha ha ha haaaaa
   
 8. A

  Andrew Jr JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Nnachofahamu wakati meno ya mtoto yanaanza kuota ..yeye mwenyewe huwa anahisi yanawasha. Kukabiliana na hilo kila anachoona kinamfaa anaingiza mdomoni ili ajikune, sasa mazingira ya mikono mara nyingi sio safi sana ndo yanamsababishia hali hyo.
   
 9. Mahmetkid

  Mahmetkid JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2012
  Joined: Apr 20, 2012
  Messages: 557
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 45
  Katika kipindi mtoto anaota meno huwa inaambatana na homa kali, mafua, kukooa na wakati mwingine mtoto uharisha. Katika kipindi hiki mtoto umaliza kinga ya mama yake aliyokuwa anahitumia na kuanza kujitengenezea yeye mwenyewe ya kwake. Vitu vingi sana huwa vinamdhuru katika kipindi hiki na kwa sababu muda huu uota meno, huwa zinahusishwa na teething symptoms.
  Cha muhimu ni kumpeleka katika kituo cha tiba ili aweze kupata matibabu yaliyo sahihi na yenye uhakika wa kutibu magonjwa yanayoambatana na uotaji wa meno.
   
 10. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wazazi wetu waliishi kwa imani zaidi, kwani maarifa yalikuwa bado hayajakuwa kama wakati tulionao sasa, swali langu ni kwamba kuna uhusiano gani kati ya kuota meno na kuharisha. Mtoto wangu ameharisha juzi kwa siku moja tu, na hata tulipojaribu kutafuta dawa tulishauriwa kuangalia hali inavyoendelea kwa siku ile, kweli siku ya pili hakuendelea kuharisha; hii inanipa tafsiri kwamba haukuwa ugonjwa so what is the logic.
   
 11. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mtoto wangu aliharisha siku moja tu na bila tiba yeyote aliacha kuharisha siku inayofuata, hii imenipa tafsiri ya kwamba hakuwa na infection yeyote na kama alikuwa na infection, je kinga yake tu ya mwili ilitosha kumaliza tatizo.
   
Loading...