Uhusiano baina ya Uingereza na Tanzania

kondoowasufi

Senior Member
Aug 19, 2014
190
169
Uhusiano wa Uingereza na Tanzania ulianza rasmi 1919 wakati wa mkutano wa Versailles Peace Treaty ambapo iliamriwa kuwa Tanganyika itakuwa chini ya Mwingereza ili kuiandaa Tanganyika kupata uhuru! Kikao hiki kilizaa pia Ligi ya Mataifa (The League of Nations).

Baadae Vita ya pili ya dunia kutokea 1939-1945 kukaanzishwa Umoja wa Mataifa (UN) kutokana na kufeli kwa LNs kwa maana ilishindwa kulinda amani ya dunia! UN wakaunda kamati iloitwa Trusteeship Council kutekeleza agizo la nchi makoloni ya Mjerumani kama Tanganyika, Togo, Cameroon, Rwanda, Burundi na Namibia kupata uhuru wake mapema.

Kamati hii ikaitembelea Tanganyika mwaka 1954 Baada ya kuanzishwa kwa TANU na wakakutana na Nyerere kuzungumzia mstakabari na mchakato mzima wa uhuru!

1961 tukapata uhuru
1964 Muungano
1965 mfumo wa chama kimoja -TANU
1967 Ujamaa na Azimio la Arusha, mfumo ambao ulikuwa kinyume na Ubepari kwa Marekani na Uingereza. Wazungu wakachukia.
1985 Ujamaa ukakoma
1992 vyama vingi
9.9.1999 Nyerere akalazwa St. Thomas hospital -London na kufariki 14.10.1999

Ikumbukwe Uingereza ni wataalam wa kada ya afya!

Sifa ya fundi wa ujenzi ni kuweza kujenga na kubomoa.

Mungu ibariki Afrika
Mungu ibariki Tanzania
 
Back
Top Bottom