Uhuru wetu hautoki kwa Kikwete au Rais yeyote; Rais hawezi kuwa "Dikteta kidogo"

Uhuru wa uhuru wa maoni unatokana na katiba lakini Rais dikteta anaweza ku-tamper na katiba na kuwaondolea watu uhuru wao, ndicho alichokuwa anamaanisha JK. Alikuwa na pointi katika hilo na wala hujamkosoa chochote hapo. Kwani wewe MMM unataka kusema nchi zenye madikteta hazina katiba nzuri? Usitake kukosoa kitu kisichokosolewa hapo ila badala yake mwambie Mbowe ajibu kwanini alimsifia JK bungeni halafu baadaye anaanza kumgeuka kuwa hana haki ya kuunda tume ya katiba.
Mshauri a-tampe na katiba... aone kitachotokea. hawezi akawa anaongea na Vilaza wa CCM kwa kutumia TV station zote bongo, anaongea bla bla tu.. its shame to you and RIZ et al
 
Uhuru wa uhuru wa maoni unatokana na katiba lakini Rais dikteta anaweza ku-tamper na katiba na kuwaondolea watu uhuru wao, ndicho alichokuwa anamaanisha JK. Alikuwa na pointi katika hilo na wala hujamkosoa chochote hapo. Kwani wewe MMM unataka kusema nchi zenye madikteta hazina katiba nzuri? Usitake kukosoa kitu kisichokosolewa hapo ila badala yake mwambie Mbowe ajibu kwanini alimsifia JK bungeni halafu baadaye anaanza kumgeuka kuwa hana haki ya kuunda tume ya katiba.

kwa hiyo mtu akisifiwa alafu akabadika aendelee kujisifu kisa alishasifiwa awali?
 
Mkuu jmushi1, mie nilitabiri hapa jana kabla hata msanii hajazungumza baada ya kufuatilia hotuba zake za nyuma kwamba hakutakuwa na lolote la maana katika hotuba hiyo zaidi ya blah blah ambazo hazina kichwa wala miguu. Na utabiri wangu ukawa kweli. Yaani unasikia hata uvivu kumsikiliza akiendeleza usanii wake halafu huku wakithubutu kuita Serikali yake eti ni "Serikali Sikivu" Sijui ni lini walianza kuwa wasikivu.
Ni kweli mkuu,mimi nilijuwa tu ataanzisha choko choko.

Kwa jinsi alivyoongea,sijui kama katiba mpya itapatikana chini ya utawala wake.
 
Ninaendelea kuonesha makosa ya kimantiki na kifalsafa ya hotuba ya Rais Kikwete jana. Mojawapo ya mambo ambayo aliyadai akikanusha kuwa yeye si Dikteta ni kauli hii ambayo sidhani kama watu waliielewa uzito wake. Rais alidai kitu kingine ambacho nacho pia hana!

Rais amedai vitu ambavyo vinahitaji kukataliwa mara moja kwa sababu tukivukubali tu tunampa nguvu ambazo hana.

1. Rais ndiye anayetoa uhuru wa kutembea, vyombo vya habari na hata kuwa (the freedom to be)
2. Rais ndiye anayetoa uhuru kwa watu, vyama vya siasa tena "mkubwa mno"
3. Anaweza kuingilia kati uhuru huo kwa kuwa "dikteta" kidogo.

Ndugu zangu, Uhuru wa Watanzania hautoki kwa Rais - awe Kikwete au yeyote mwingine. Katiba yetu inasema hivi kuhusu uhuru wetu: (Ibara ya 12:1)

Maneno hayo yanaweza kuonekana ni shallow au hollow lakini ni makubwa sana. Yanatueleza kwamba kila Mtu (mimi, wewe, mtoto, mzee, kijana, msomi, mjinga, kichaa, mwenye akili sana, mlevi, mzinzi hata shoga!) huzaliwa 'HURU NA SAWA'! Kwa maneno mengine uhuru wetu hautokani na rais au chama cha siasa unatokana na kuzaliwa kwetu kama BINADAMU. Ndio maana tunasema "binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa".

Kwa hiyo, hoja ya kuwa uhuru wetu unatoka kwa rais au kwamba RAis anafikiria kuwa sisi tuko huru kwa sababu kaamua kutugea uhuru haina msingi, ni ya kukataliwa na kwa mara nyingine haina msingi wa Kikatiba (lacks constitutional basis whatoever).

NI kutoka katika kutambua kuwa sote tunazaliwa huru ndipo Katiba sasa inatambua uhuru huo na kuuhakikisha (the constitution recognizes and guarantee that freedom). Kumbe wananchi wanazaliwa wakiwa huru na kwa kutumia katiba yao wanajihakikishia uhuru huo - Rais hatoi wala kuhakikisha uhuru huo bali anasimamia kuwa uhuru huo hauondolewo - iwe na maadui wa ndani au wa nje - na hii ina maanisha hata na yeye mwenyewe!

Je ni uhuru gani tunazaliwa nao ambao hauwezi kuondolewa kiholela kama Rais alivyoashiria? Nitataja tu kama Katiba inavyoanisha sasa:

Uhuru wa kuwa hai (rais hawezi kuja na kumwambia polisi 'mpige huru risasi' halafu mtu akapigwa risasi kwa vile 'rais kasema'). Ili kuhakikisha hili Katiba imeweka wazi kuwa "itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake". Kwa maneno mengine ni kuwa kauli ya Rais anaweza kuwa dikteta kidogo na kuzuia uhuru wawatu haina msingi ni ya kuikataa kwani hana madaraka wala uwezo huo (nililisema hili siku ile aliposema Bungeni kuwa angeweza kuagiza Dr. Slaa akamatwe na akakamatwa)!

Uhuru wa mawazo na maoni - kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna mtu anayeweza kumlazimisha mtu mwingine kufikiri au kuwa na maoni anayoyataka yeye! Kiila mtu anahaki ya kufikiri na kujenga maoni ayapendayo yeye bila kulazimishwa. Hii ina maana kuwa uhuru huu hautoki kwa Rais. Rais hawezi kutuambia kuwa sote tunatakiwa kufikiria hivi au vile na tukifikiri tofauti basi ni makosa!

Uhuru wa imani
- Katiba inatambua kuwa kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutoamini dini yoyote. Na katiba yetu inaenda mbali zaidi na kusema kuwa mtu anayo haki ya kubadilisha imani yake. Kwa maneno mengine mtoto aliyezaliwa katika familia ya kikristu akiamua kuwa Muislamu serikali au mtu yeyote hawezi kwenda na kumlazimisha abadili. Wanaweza kumshawishi au kumuonesha makosa lakini mwisho wa siku uamuzi ni wake. Na mtu akiamua kutoamini Mungu au akiamini minazi hakuna mtu wa kumlazimisha kuwa abadili imani! Rais hawezi kulazimisha watu waamini vyovyote apendavyo yeye.

Hiyo ni mifano michache tu. Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais kuwa yeye ndiye anatoa uhuru na kuwa anaweza kuuondoa uhuru huo wa kuwa "dikteta kidogo" haina msingi. Uhuru wetu hautoki kwa Rais. Period.
Layman aliyeandika hotuba ile na msoma hotuba mwenyewe wana alarge na codes.
 
Ni kweli mkuu,mimi nilijuwa tu ataanzisha choko choko.

Kwa jinsi alivyoongea,sijui kama katiba mpya itapatikana chini ya utawala wake.

Mkuu jmushi1..Ni lazima awe tayari kusoma alama za nyakati na kuwasikiliza watu mbali mbali akiwemo SAS, Warioba, Kitine na wengineo ndani ya chama chao cha magamba waliompa ushauri kwamba hii ni katiba ya Watanzania na si ya CCM hivyo ni lazima akae chini na CHADEMA ili kuhakikisha katiba inayopatikana ni ile ambayo itaungwa mkono na Watanzania wote na ambayo pia itakakikisha tunakuwa na tume huru ya uchaguzi na siyo hii tuliyonayo hivi sasa, vinginevyo akiendelea kujifanya kichwa ngumu kwa kuwa yeye ni jemadari mkuu basi maafa yoyote yale yatakayotokea ndani ya nchi yetu kufuatia vurugu za kuipata katiba mpya kutakuwa hakuna wa kumlaumu ila ni yeye Kikwete.
 
Nina wasiwasi atajiongezea muda wa kukaa ikulu kwasababu sioni ni kwa vipi hiyo deadline yake ya kuipata katiba mpya 2014 inatokana na mahesabu gani kama utaratibu wenyewe ndo huu.
 
Nina wasiwasi atajiongezea muda wa kukaa ikulu kwasababu sioni ni kwa vipi hiyo deadline yake ya kuipata katiba mpa 2014 inatokana na mahesabu gani kama utaratibu wenyewe ndo huu.

.....Inawezekana akafanya hivyo, lakini kwa maoni yangu atafanya kosa kubwa sana ambalo anaweza kulijutia kwa muda mrefu.
 
kinachotokea sasa ni kuwa hata ukilinganisha maneno na matendo ya Katibu Mkuu kama Jairo na Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari ya kata ambaye katika mazingira magumu ameweza kufaulisha wanafunzi kwa kiwango cha madaraja ya kwanza, la pili utaumia sana kichwa kwa kuwa unaishia kujiuliza hivi kiongozi huyu mkubwa wa nchi anawezaje kuwa kilaza namna hii? matendo na hata maneno yake ni vijembe tu vya ku-buy time ili siku nyingine ianze.....tutaendelea kukosoa mpaka tuwapate wanaotugusa katika maisha yetu kwa dhati....
 
Ukisoma hii hotuba yake ni mbaya kuliko alivyokuwa anaongea. Nadhani Rais na team yake walitaka ku-spin mambo, kugeuza madai ya Mbowe, Lissu ili ionekane kama hawana hoja, lakini ukweli ni kuwa imemfanya yeye (rais) aonekane kama haeweli nini hawa wabunge wa CHADEMA wanasema!
 
Tuwe wakweli kwa hili la speech ya jana ni hakuna kitu,kwanza mbaya zaidi tuliambiwa ni wazee wa DAR kumbe ni wanachama wa CCM,Maana kulikuwa hata na vijana humo lakini wa CCM,na kingine DAR wazee ni wana CCM tu?hakuna wazee wrngine?Tukirudi kwenye speech yenyewe yale aliyoyakosoa MMM ni kweli wala hajakosea,kwani siku zote tunajua speech za raisi wetu hasa anapokuwa ameibuka katika msingi wa kujibu pigo,hii inaonekana nchi nzima ilichanganyikiwa kwa hotuba ya Mh Lissu,maana hata bungeni wabunge wote A na B CCM walishindwa kujadili mswaada badala yake wakajadili CDM na Lisu,vivyo hivyo na JK.na mwisho wa siku akaanza kuteleza viu ambavyo nashangaa mnapotetea.
 
kama hajui dikteta ni nani basi ajiulize tena kwa nini wananchi wanaona hayuko page moja nao. sikujua kuwa rais anatuongoza kwa hisani kama ili hali hakuomba kazi hii kwa udi na uvumba kwa miongo miwili eti leo anataka tuishi kumtukuza. yeye aendelee kutoa hotuba za kizushi za kila mwezi(uncontent literature)...kikwete hana uwezo wa kutufanya watu tuishi kwa kumuhofia yeye, kikwete ataua kumi lakini mia watazaliwa wako against naye na familia yake kama anadhani watu wenye ngozi nyeusi ni tofauti na waarabu basi amekalia kuti kavu. hizi mali alizojipatia kwa high speed will be burn to ashes trust me.
if ndugu kikwete thinking he is doing this in sake ya favor kwa watanzania waliotaliwa na muundo wa rushwa anahitaji haraka kumbadilisha anayemjengea hoja za kuongea na hao wazee sijui waliopigania uhuru au ni ndugu zetu waliodhulumiwa elimu. honestly, aangalie ghadafi na mubaraka.
kwa nini watu wanaanza kumuona ni dikiteta? sababu ni pale wahujumu wa uchumi wa nchi hii ni gang yake...awaulize East Germany na STASI walivyo melt na nguvu ya umma. kama ana dini basi amurudie mungu wake...basi kama hana Mungu wa kweli eendelee kuabudu nguvu za kiza.
 
tumewazoea kwani kuna siku mliwahi kusifu hotuba

Ukweli ni kwamba hotuba ya raisi imewasaidia wale ambao walikuwa hawamjui vizuri ni mtu wa namna gani wamemjua sasa. The guy showed his true colors i.e. his way or no way. Nafikiri hata ile katiba aliyoapa kuilinda na kuitetea aliiisahau kabisa kwenye mazungumzo yake. Sitaki kurudia kwani yote yameelezwa vizuri na wengine. Lakini JK kila anapozungumza mfano mzuri ni jana; anazidi kuwagawa watanzania badala yakuwaunganisha. Kwenye hii hotuba amewakera wengi sio wapinzani tu bali pia Wana-CCM na wasio na vyama. Nasema hivi na ninasema kila siku; hawa viongozi waliopata vyeo jeshini leadership zao ni kero tu huku uraiani. His leadership style does not work kwenye hii karne labda huko jeshini tu.
 
Wakubwa wanapofika mahala waka-amini, tena kwa dhati kabisa kwamba, uhuru wetu unatoka kwao, yaani ni kama zawadi yao kwetu, amabayo wanaweza kutupatia wakitaka, au wakaiondoa wakitaka, basi mjue siku zimekaribia. Lakini ilikwisha semwa tangu zamani za kale, zama za a-kina Kant kwamba: "freedom is independennce of the compulsory will of another, and in so far as it can co-exist with the freedom of all according to universal law, it is the one sole original inborn right belonging to every man in virtue of his humanity". Kwa maneno mengine, uhuru ni haki tunayozaliwa nao na kwa hilo nadhani Mwanakijiji yuko sahihi.
 
Ninaendelea kuonesha makosa ya kimantiki na kifalsafa ya hotuba ya Rais Kikwete jana. Mojawapo ya mambo ambayo aliyadai akikanusha kuwa yeye si Dikteta ni kauli hii ambayo sidhani kama watu waliielewa uzito wake. Rais alidai kitu kingine ambacho nacho pia hana!

Rais amedai vitu ambavyo vinahitaji kukataliwa mara moja kwa sababu tukivukubali tu tunampa nguvu ambazo hana.

1. Rais ndiye anayetoa uhuru wa kutembea, vyombo vya habari na hata kuwa (the freedom to be)
2. Rais ndiye anayetoa uhuru kwa watu, vyama vya siasa tena "mkubwa mno"
3. Anaweza kuingilia kati uhuru huo kwa kuwa "dikteta" kidogo.

Ndugu zangu, Uhuru wa Watanzania hautoki kwa Rais - awe Kikwete au yeyote mwingine. Katiba yetu inasema hivi kuhusu uhuru wetu: (Ibara ya 12:1)

Maneno hayo yanaweza kuonekana ni shallow au hollow lakini ni makubwa sana. Yanatueleza kwamba kila Mtu (mimi, wewe, mtoto, mzee, kijana, msomi, mjinga, kichaa, mwenye akili sana, mlevi, mzinzi hata shoga!) huzaliwa 'HURU NA SAWA'! Kwa maneno mengine uhuru wetu hautokani na rais au chama cha siasa unatokana na kuzaliwa kwetu kama BINADAMU. Ndio maana tunasema "binadamu wote huzaliwa huru na wote ni sawa".

Kwa hiyo, hoja ya kuwa uhuru wetu unatoka kwa rais au kwamba RAis anafikiria kuwa sisi tuko huru kwa sababu kaamua kutugea uhuru haina msingi, ni ya kukataliwa na kwa mara nyingine haina msingi wa Kikatiba (lacks constitutional basis whatoever).

NI kutoka katika kutambua kuwa sote tunazaliwa huru ndipo Katiba sasa inatambua uhuru huo na kuuhakikisha (the constitution recognizes and guarantee that freedom). Kumbe wananchi wanazaliwa wakiwa huru na kwa kutumia katiba yao wanajihakikishia uhuru huo - Rais hatoi wala kuhakikisha uhuru huo bali anasimamia kuwa uhuru huo hauondolewo - iwe na maadui wa ndani au wa nje - na hii ina maanisha hata na yeye mwenyewe!

Je ni uhuru gani tunazaliwa nao ambao hauwezi kuondolewa kiholela kama Rais alivyoashiria? Nitataja tu kama Katiba inavyoanisha sasa:

Uhuru wa kuwa hai (rais hawezi kuja na kumwambia polisi 'mpige huru risasi' halafu mtu akapigwa risasi kwa vile 'rais kasema'). Ili kuhakikisha hili Katiba imeweka wazi kuwa "itakuwa ni marufuku kwa mtu yeyote kukamatwa, kufungwa, kufungiwa, kuwekwa kizuizini, kuhamishwa kwa nguvu au kunyang'anywa uhuru wake". Kwa maneno mengine ni kuwa kauli ya Rais anaweza kuwa dikteta kidogo na kuzuia uhuru wawatu haina msingi ni ya kuikataa kwani hana madaraka wala uwezo huo (nililisema hili siku ile aliposema Bungeni kuwa angeweza kuagiza Dr. Slaa akamatwe na akakamatwa)!

Uhuru wa mawazo na maoni - kila mtu yuko huru kuwa na maoni yoyote na kutoa nje mawazo yake, na kutafuta,
kupokea na kutoa habari na dhana zozote kupitia chombo chochote bila ya kujali mipaka ya nchi, na pia ana uhuru wa
mawasiliano yake kutoingiliwa kati.
Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna mtu anayeweza kumlazimisha mtu mwingine kufikiri au kuwa na maoni anayoyataka yeye! Kiila mtu anahaki ya kufikiri na kujenga maoni ayapendayo yeye bila kulazimishwa. Hii ina maana kuwa uhuru huu hautoki kwa Rais. Rais hawezi kutuambia kuwa sote tunatakiwa kufikiria hivi au vile na tukifikiri tofauti basi ni makosa!

Uhuru wa imani
- Katiba inatambua kuwa kila mtu ana uhuru wa kuamini au kutoamini dini yoyote. Na katiba yetu inaenda mbali zaidi na kusema kuwa mtu anayo haki ya kubadilisha imani yake. Kwa maneno mengine mtoto aliyezaliwa katika familia ya kikristu akiamua kuwa Muislamu serikali au mtu yeyote hawezi kwenda na kumlazimisha abadili. Wanaweza kumshawishi au kumuonesha makosa lakini mwisho wa siku uamuzi ni wake. Na mtu akiamua kutoamini Mungu au akiamini minazi hakuna mtu wa kumlazimisha kuwa abadili imani! Rais hawezi kulazimisha watu waamini vyovyote apendavyo yeye.

Hiyo ni mifano michache tu. Kwa ufupi ni kuwa kauli ya Rais kuwa yeye ndiye anatoa uhuru na kuwa anaweza kuuondoa uhuru huo wa kuwa "dikteta kidogo" haina msingi. Uhuru wetu hautoki kwa Rais. Period.

Udikteta tumeuacha zamani, wakati unarundikwa ndani bila hata kujuwa lini utatoka, mpaka apende Nyerere.

Udikteta tumeuacha wakati gazeti ni Daily news na la chama.

Hivi ni nani anaopinga kuwa zama za Udikteta tumeshaondokana nazo huko, chama kilikuwa kimoja, magazeti anayotaka nyerere tu. Radio anazotaka nyerere tu. TV hakuna. Jela unafungwa kwa amri tu ya Nyerere, au unapotezwa na hujulikani umeenda wapi? Nani asiojuwa kisa cha kuadhiriwa Hanga uwanjani na Nyerere na hajaonekana tena baada ya hapo> kama si udikteta ni nini ule?
 
Udikteta tumeuacha zamani, wakti unarudikwa ndani bila hata kujuwa lini utaoka, mpaka apende Nyerere.

Udikteta tumeuacha wakati gazeti ni Daily news na la chama.

Hivi ni nani anaopinga kuwa zama za Udikteta tumeshaondokana nazo huko, chama kilikuwa kimoja, magazet anayotaka nyerere tu. Radio anazotaka nyerere tu. TV hakuna. Jela unafungwa kwa amri tu ya Nyerere, au unapotezwa na hujulikani umeenda wapi? Nani asiojuwa ksa cha kuadhiriwa Hanga uwanjani na Nyerere na hajaonekana tena baada ya hapo> kama si udikteta ni nini ule?
Naona hukumu yako ya miaka miwili imekuwa siku mbili.

Hopefully umejifunza na utajirekebisha.
 
Hii sredi hata mantiki yake siioni.
Kwani hao marais ambao ni madikteta, kwa mfano Hitler, katiba yao ilikuwa haithamini utu?
Udikteta ni abuse of power, and can be practised by any leader.
Haimaanishi kuwa unafanywa kikatiba.
Nadhani waku mmekosa points za kuongea, mnaanza kutia aibu sasa.
 
Hapana,kuna viongozi wanaoruhusiwa na katiba kuwa madikteta,mwalimu alishalisema hili huko nyuma na watu wakatafsiri wanavyojuwa.

Hata hivyo ndiyo maana halisi ya sisi kutaka katiba mpya na si kuendelea na maboresho.
 
Back
Top Bottom